Uvivu ni chanzo cha umasikini, piga vita uvivu

Uvivu ni chanzo cha umasikini, piga vita uvivu

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Uvivu ni hali ya kutokuwa na hamasa, umakini, bidii, kujituma katika kufanya jambo.

Unaweza kuwa mvivu wa kufanya kazi za mikono, mvivu wa kusikiliza, mvivu wa kutembea, mvivu wa kujieleza, mvivu wa kusoma, mvivu wa kufikiri, mvivu wa kupika, mvivu wa kuamka, mvivu wa kula, mvivu wa kutimiza wajibu wako wowote.

Uvivu ni tabia ambayo hujijenga taratibu na kisha huota mizizi na kuanza kuathiri mwenendo wa maisha. Uvivu katika namna zake zote ni tabia mbaya sana na ni chanzo kikuu cha umaskini na hali ngumu.

Watu wengi ni wavivu na hawajatambua kwamba ni wavivu. Wanafikiri wamefikia ukomo wa uwezo wao kumbe ni wavivu. Ili uweze kupiga hatua katika maisha lazimu umshinde adui uvivu.

Je, unawezaje kuacha uvivu? Hatua ya kwanza ni kutambua kwamba uvivu ni mbaya. Hatua ya pili ni kutambua kwamba ili upige hatua lazima ushinde uvivu.

Yako mambo mengi unaweza kufanya ili kubadili tabia yako. Kabla ya kuanza kufanya mambo hayo inabidi kwanza utambue aina tatu kuu za uvivu unaokusumbua na kuathiri mwenendo wa maisha yako na hali yako itakavyokuwa iwapo utashinda udhaifu huo

Tujadili kwa pamoja namna ambavyo tunaathtiriwa na uvivu na jinsi tunaweza ukabili katika maisha yetu.
 
Thread bora ya siku.

Bravo.

Ki msingi uvivu mbaya kuliko aina zote za uvivu duniani ni uvivu wa kufikiri.

Mara tu mtu anapokuwa mvivu wa kufikiri basi anakuwa sawa na mwanafunzi ambaye yupo likizo na ameamua ku down tools zote za masomo akisubiri shule ifungue aanze upya.
 
Mkuu hii nadharia ya kufanya kazi sana ndo kufanikiwa ni uwongo kabisa...kuna watu wanafanya kazi kweli kweli lakini wameishia kuwa masikini. "Eti fanya kazi kama mtumwa ili uishi kama mfamle" huu ni uwongo wa wazi kabisa...
 
Mkuu hii nadharia ya kufanya kazi sana ndo kufanikiwa ni uwongo kabisa...kuna watu wanafanya kazi kweli kweli lakini wameishia kuwa masikini. "Eti fanya kazi kama mtumwa ili uishi kama mfamle" huu ni uwongo wa wazi kabisa...
Mkuu hakuna mafanikio bila kufanya kazi?Bili kujituma,Bila bidii,bila maarifa.Tatizo labda ni tafsiri tu ya Kufanya kazi kama mtumwa ndo inaleta ukakasi.
 
Back
Top Bottom