Uvumilivu unanishinda jamani....

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,296
Reaction score
12,972
Hali zenu wadau wa jukwaa hili....

Mwenzenu mie ni mama wa mtoto mtoto mmoja... (single mother) sasa huyu mzazi mwenzangu kiukweli naeza sema kanitelekeza kabisaaa... Kwani majukumu yoote ya kumlea mwanetu nayabeba mie includes school fees, uniform, vitabu, madaftari, kalamu, chakula, malazi na hata mavazi. Kama mjuavyo English Medium School ada zake ni 1m+ per year.

Nimekuwa nikilipa ada hiyo huu ni mwaka wa sita (6) sasa. Huyu baba si kwamba hana uwezo, mshahara wake ni mara 4 ya mshahara wangu ila sijui ni kwanini hataki kumsomesha mwanaye. Kila nikimueleza anadai majukumu ni mengi aliyonayo. Hata mimi pia nina majukumu sio kwamba ninaishi peke yangu.

Hapa ninachoomba ushauri, ni kwamba nifanyeje ili awe responsible kwa mwanaye. Make mwisho wa siku mtoto huyooo atamfuata baba yake na hatojali kama baba yake alikuwa na mchango katika maisha yake. Sishindwi kumsomesha ila ninachotaka na yeye achangie kumsomesha mwanaye. Nifanyeje wadau...

Asanteni
 
Nenda ustawi wa jamii mamii watakusaidia hilo mara moja
 
Uko sawa kabisa ni lazima achangie kwa ajili ya elimu ya mwanaye. Kwa uzoefu watoto wengi wanapofanikiwa kwa asilimia kubwa huwa huegemea sana kwa Mama na huyo ndiyo anayefaidi matunda ya mtoto.
 


Mkome kujishikisha mimba ili muolewe.
 
Mwambie Kwanza Anavyofanya Sio Vzuri, Akizingua Nenda Ustawi Wa Jamii. Mbona Atakoma Watakavyompangia Gharama Za Matunzo Ya Mtoto
 
charminglady pole. Huyo anayejibu kwa uwazi huo kuwa anayo majukumu mengi ni wazi kuwa either anakufanyia makusudi akijua kuwa utatunza au hajitambui kuwa Baba hajitambulishi wa jina bali majukumu kwa mwanaye. Hiyo "nina majukumu mengi" ni lazima ajue kuwa ndani yake ni kumtunza huyo mtoto. Kuna mawili unayoweza kufanya, 1. Forgo msomeshe mwanao mwenyewe naye atakushukuru akikua na sio kweli kuwa atakusahau ikiwa atajua wazi kuwa ni wewe uliyegharamia maisha yake; hata akijakwenda kwa babake akikua, akiwa anajua kuwa wewe ndie uliyemsomesha katu hatosahau kukuthamini. Pili nenda Ustawi wa Jamii kama alivyoshauri mdau hapo juu. Ila tu tambua kama ni mbaba mkorofi atavizia mtoto atomize miaka yake aje amchukue kwa madai kuwa analea but kama ukimwacha asitunze hata hiyo guts ya kuja kumdai atakapojisikia kuja kumchukua itakuwa mbinde kidogo. Chaguo ni lako.
 
Last edited by a moderator:

Duh.... Hapo kwenye red ndipo hasa panaponitia wazimu... Yan hanisaidii kuela afu aje kumchukua!!!!!!
 
Duh.... Hapo kwenye red ndipo hasa panaponitia wazimu... Yan hanisaidii kuela afu aje kumchukua!!!!!!

Ndio mama kuna ile miaka ambayo mtoto akishaitimiza anaruhusiwa kuchukuliwa na babake (nakumbuka ilikuwa ni 7 years) sijui kama kuna mabadiliko. Sasa ukiamua mpeleke ustawi alazimishwe kulea (wengi huwa wanapelekewaga barua kwa maHr wao so mshahara wake unakatwa juu kwa juu). Sasa mwingine anawezakuja kuona kama anakufaidisha wewe, especially ukianza kuwa na mahusiano mengine, basi ataamua kumchukua mwanae ili mshahara usiwe diverted tena. Ni kizungumkutu mamii yangu acha tu.
 
Hatukomi mpaka Yesu aje, tena mwaka huu nina mpango wa kujibebesha tena....

Njoo huku nikubebeshe! Ila mie nitamsomesha - hata huyo wakwanza ikibidi. On a serious note; nenda ustawi wajamii watalishughulikia kikamilifu suala lako.
 
sio vizuri kumwambia mtoto wa mwenzio hivyo, kama huna coment si unyamze tu!! kumbuka na wewe una watoto, subiri uone!

si ndo hapo? May be anawatoto wakiume watupu!!
 
Pole my dada,nenda ustawi akili itamkaa sawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…