Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,472
dada, ukiamua unaweza kumpeleka ustawi au mahakamani. ila kuna scenario moja nilishawahi kuiona, hii issue huwa inaleta ugomvi mkubwa sana kama mwanaume ana mke mwingine kiasi kwamba baba wa mtoto aliona kama yule mtoto ni kauzibe fulani, akafikia hatua ya kumuua yule mtoto, ili awe huru;ushirikina upo na issue kama hii nilishawahi kuiona. hivyo, kama hauna namna yeyote kabisa fuatilia, ila kama una means nyingine kumtunza uyo mtoto, achana na uyo mwanaume mpende mwanao usije kumkosa, kwasababu uyo baba yake kama anawatoto wengine na mke ujue hana uchungu sana na mtoto wako, hata mtoto wako akifa hawezi kuona uchungu zaidi ya kushukuru kama umekuwa ukimsumbua na kama mke wa ndani anamsumbua kuhusu uyo mtoto wako. ya nini umkose mwanao, uyo mtoto wako ndiye atakaye kusaidia wewe baadaye, pima halafu ukiona kuna usalama endelea, ila ukiona kuna walakini achana naye tunza mwanao mungu amekupa zawadi hiyo, la sivyo wanaume wengine huwa wanaweza kumtoa kafara ili kujikomboa na usumbufu. nimeshakutana na issue kama hizi tatu. moja walifikishana mahakamani, na mtoto alikufa kifo cha mashaka ajabu na baba hakushiriki hata msiba.Hali zenu wadau wa jukwaa hili....
Mwenzenu mie ni mama wa mtoto mtoto mmoja... (single mother) sasa huyu mzazi mwenzangu kiukweli naeza sema kanitelekeza kabisaaa... Kwani majukumu yoote ya kumlea mwanetu nayabeba mie includes school fees, uniform, vitabu, madaftari, kalamu, chakula, malazi na hata mavazi. Kama mjuavyo English Medium School ada zake ni 1m+ per year.
Nimekuwa nikilipa ada hiyo huu ni mwaka wa sita (6) sasa. Huyu baba si kwamba hana uwezo, mshahara wake ni mara 4 ya mshahara wangu ila sijui ni kwanini hataki kumsomesha mwanaye. Kila nikimueleza anadai majukumu ni mengi aliyonayo. Hata mimi pia nina majukumu sio kwamba ninaishi peke yangu.
Hapa ninachoomba ushauri, ni kwamba nifanyeje ili awe responsible kwa mwanaye. Make mwisho wa siku mtoto huyooo atamfuata baba yake na hatojali kama baba yake alikuwa na mchango katika maisha yake. Sishindwi kumsomesha ila ninachotaka na yeye achangie kumsomesha mwanaye. Nifanyeje wadau...
Asanteni