Uvumilivu wa kisiasa usio na ukomo ni sumu ya uvumilivu wa kisiasa

Uvumilivu wa kisiasa usio na ukomo ni sumu ya uvumilivu wa kisiasa

Makini-Zaidi

New Member
Joined
Jul 31, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Uvumilivu wa kisiasa ni miongoni mwa kanuni kuu katika dhana ya demokrasia. Hata hivyo katika jamii yetu bado tunahitaji kuukubali ukweli huu ili kuwa na demokrasia yenye kuchochea utawala bora katika nyanja zote.

Kuna umuhimu na ulazima mkubwa wa kutambua kuwa, si kila mtu atakuwa na mawazo/fikra sawa na mtu mwingine. Hata kama watu husika watakuwa katika itikadi au imani moja, bado si kila wakati watu hao watakuwa na mtazamo sawa.

Kwa kuzingatia ukweli huu, katika nyaja za siasa kwa mfano, uvumilivu wa kisiasa katika jamii ni moja wapo ya kanuni kuu na muhimu sana katika dhana ya demokrasia (Encyclopedia.com).

Eger na Hjerm wanaainisha maelezo/maana tatu za uvumilivu zifuatazo:​
  1. Kukubali kutofautiana​
  2. Kuheshimu kutofautiana, na​
  3. Kutambua kuwa kutofautiana ni uhalisi wa ulimwengu.​
Uvumilivu wa kisiasa ni utayari wa kuruhusu haki za msingi na uhuru wa kiraia miongoni mwa watu wenye mitazamo tofauti tofauti.

Hatahivyo, Karl Popper anashauri kuwa, wakati tukitambua uvumilivu wa kisiasa ni miongoni mwa kanuni muhimu sana katika kujenga demokrasia, uvumilivu wa kisiasa usiokoma unaweza kuwa sumu ya uvumilivu wa kisiasa. Hivyo lazima kuwe na ukomo.

Kwa mujibu wa Karl Popper, kipimo cha ukomo wa uvumilivu wa kisiasa ni kutowavumilia wale wote wasio kuwa na uvumilivu wa kiasa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kuwavumilia wasio na uvumilivuwa kisiasa kunaweza kusababisha kupotea kwa uvumilivu wa kisiasa.

Mwandishi Kasika aliwahi kusema, wakati mwingine kuna matatizo yanatokea kwa sababu tu uvumilivu wa kisiasa haujapewa nafasi ili uweze kufanya kazi yake kwa ajili ya kuweka mambo sawa. Kuna manufaa makubwa sana iwapo uvumilivu wa kisiasa utapewa nafasi pale unapotokea mgogoro. Wakati mwingine tatizo linaweza kuwa dogo lakini likakuzwa kwa kukosekana tu uvumilivuwa kisiasa.
  • Kwa muhtasari, mambo ya msingi katika hoja hii ni kwamba:
  1. Uvumilivu wa Kisiasa ni miongoni mwa kanuni kuu katika dhana ya demkrasia.
  2. Mtu mwenye sifa ya uvumilivu wa kisiasa ni yule aliyetayari kuruhusu haki za msingi na uhuru wa kiraia kwa watu wenye mtazamo tofauti na ule wa kwakwe.
  3. Uvummilivu wa kisiasa ni bora ukawa na ukomo. Ukomo wa uvumilivu wa kisiasa ni kutuwavumilia wale wote wasio na uvumilivu wa kisiasa kwa kuwa kuendelea kuwavumilia kutasababisha kupotea kwa uvumilivu wa kisiasa. Iwe katika ngazi ya jamii, chama cha siasa au taifa.
  4. Wasiokuwa na uvumilivu wa kisiasa ni wale wote wasio na utayari wa kuruhusu haki za msingi na uhuru wa kiraia kwa watu wenye mitazamo tofauti na mitazamo yao.
 
Back
Top Bottom