Uvumilivu wa wana JAMIIFORUMS VS Ubabe wa CCM:JE mwisho wake ni nini?

Uvumilivu wa wana JAMIIFORUMS VS Ubabe wa CCM:JE mwisho wake ni nini?

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Posts
2,483
Reaction score
164
Heshima Mbele,

Ndugu Watanzania wenzangu,Kwa muda wa mwezi sasa nimekuwa mtazamaji wa Jf Bila kuchangia maada yeyote na hii ilitokana na Hotuba aliyoitoa Muungwana pale Dodoma,Pia kufuatia na Ripoti ya utekelezaji wa serikali katika ripoti ya RDC.

Mie nadhani imetosha sasa,sababu tumeshindwa kuwajadili kwa hoja na sasa inabidi tujipange kisera.Tuzungumzie jinsi ya ssisi kuwakomboa watanzania wenzetu.Na ningependa tusitishe mijadala ya Ufisaid na tuanze kuwabana katika habari za maendeleo.

Tupitie Jimbo hadi jimbo kueleza uozo wa wabunge ambao wamewshindwa kutekeleza ahadi zao kwa wananchi.Tueleze nini kifanyike.Mafisadi wana nguvu kuu ambayo haiwezi kuvunjwa hata kama mwanakijiji akilala masaa matano tu kwa siku.
 
Heshima Mbele,

Ndugu Watanzania wenzangu,Kwa muda wa mwezi sasa nimekuwa mtazamaji wa Jf Bila kuchangia maada yeyote na hii ilitokana na Hotuba aliyoitoa Muungwana pale Dodoma,Pia kufuatia na Ripoti ya utekelezaji wa serikali katika ripoti ya RDC.

Mie nadhani imetosha sasa,sababu tumeshindwa kuwajadili kwa hoja na sasa inabidi tujipange kisera.Tuzungumzie jinsi ya ssisi kuwakomboa watanzania wenzetu.Na ningependa tusitishe mijadala ya Ufisaid na tuanze kuwabana katika habari za maendeleo.

Tupitie Jimbo hadi jimbo kueleza uozo wa wabunge ambao wamewshindwa kutekeleza ahadi zao kwa wananchi.Tueleze nini kifanyike.Mafisadi wana nguvu kuu ambayo haiwezi kuvunjwa hata kama mwanakijiji akilala masaa matano tu kwa siku.

Mkuu Gembe,

Wengine tunaona bado haijatosha!Na si kweli luwa tumeshindwa kuwajadili kwa hoja, labda kama mtazamo wako wa hoja ni tofauti na wengine.
Hapa JF zimekuwa zikitolewa hoja nyingi sana tena nzito!tatizo ni kuwa serikali ya ccm imekuwa sio sikivu kwa wanachi wake hata kidogo.
nadhani tuendelee kuelimishana na kuhamasishana hapa JF kadri iwezekanavyo ili wale tunaopata nafsi ya kufika vijiweni kuzungumza na watanzania wenzetu wasiofika hapa tuweze kuhabarishana kile kinachoendelea nchini.Lazima wanachi wa kawaida hasa wale wasiokuwa na uhakika wa mlo japo wa siku moja watambue usanii tunaofanyiwa na serikali yetu.Serikali inayowakumbatia mafisadi wachache na kuwatelekeza wanachi wengi.
Sera wanatunga wao wenyewe, kwahiyo dawa hapa ni kuendelea kuwasema na kuwasema hadi watanzania wote wafumbuke macho.
 
Hii ni vita.
Wewe pigana hapo ulipo na sisi tutapigana huku tuliko.

Lowassa na timu yake wamekwenda chini siyo kwa sababu tulichagua kupigana naye kwanza yeye na kuacha mapambano mengine.

Anzisha thread, jenga hoja, tutachangia. Lakini hatuwezi acha suala la ufisadi kwa mtaji wowote ule.
 
Mtafutaji hachoki na akichoka keshapata. Usijali Mzalendo Gembe nyanyuka beba silaha na zana zako tusonge mbele bado mji mmoja tu - UFISADI- tumalize vita kwa ushindi.

Waliokufa tayari ni Balaahili ambao walikuwa amiri jeshi wakuu wa BOT na wengine wamejeruhiwa vibaya. Inasikitisha sana, inadhalilisha sana na inafedhehesha sana kuona umechoka wakati amebaki mtu mmoja amka Comrade Gembe huyo anakuja upande wako!

Imekaaje hiyo? Kipichapicha na kimatukiotukio!
 
Lets not hide around the bush

correct header ingekuwa Uvumilivu wa wana CHADEMA V/S Ubabe wa CCM


sasa sijui mwandhishi kaona noma gani kusema hilo ilihali sasa iwazi kuwa JF iko biased when it comes to CCM v/s CHADEMA na kila mmoja anajua wapi JF inasimama kwenye hili


my 2 cents
 
Mimi naona mambo ya vyama vingi yafutwe...Haya ni ya kutugawa tu na ndio maana halisi ya mkaburu!
Toka haya mambo ya ukabila na upuuzi wa kidini yashamiri...Ni wazi vyama vingi ni USHETANI...Wananchi wapate UHURU kwanza na ELIMU.
Baada ya hapo watajuwa kusoma kati kati ya mistari....Tukifanya tofauti basi watauza silaha wee....Huku tukiendelea kufa tu na njaa na umasikini na huku michanga ya almasi na dhahabu ikichotwa.
Vyama vingi vije baada ya ujinga kufutwa...Zaidi ya hapo ni Utumwa wa akili.
NI MUDA WA KUIJENGA NCHI NA KUACHA UPUUZI WA KUGOMBEA MALI ZA WANANCHI,SIFA,MADARAKA NK...Dhamana ya nchi si ya kifamilia wala kikabila...Ni ya kitaifa na ya Kiafrika.
Afrika time is NOW!
 
kuna ukombozi wa aina nyingi wananchi wanahitaji sio nyanja moja tuu ya kisiasa sasa tusio wanasiasa tuwakomboe wananchi kwa yapi?

Uongozi umekuwa maslahi makubwa sana....Na wananchi wanadhani uongozi ni usomi na utajiri!
Hawajui ni kipaji kwanza na usomi ni baada ya hapo.....Kwamba kwanza awe na kipaji...Ila wanajuwa utajiri zaidi ni baada ya uongozi!
Ni vizuri kumpata kiongozi msomi...Ila wasomi hawapewi heshima na hawana maslahi hadi wawe wanasiasa ama wawe na ushawishi kwa wanasiasa.
Na kuwa na ushawishi kwa wanasiasa si lazima uwe umesoma...Unaweza kuwa ndugu ama kabila moja ama chama kimoja...Sasa si unaona migawanyiko hapo?
Wasomi watakaotumia taaluma zao ipasavyo kama wakipewa nafasi na wanasiasa....Then ndio hao watakaolikomboa Taifa!
Ila tunataka Kiongozi mpenda watu na msomi asiye na tamaa binafsi.
Kwanza hata maslahi makubwa ya kioungozi ndiyo yanaharibu kwasababu ukiwa na pesa ikulu ndiyo yako...Na kama huwezi kwenda wewe...Basi unaweza kununua Rais.
 
Lets not hide around the bush

correct header ingekuwa Uvumilivu wa wana CHADEMA V/S Ubabe wa CCM


sasa sijui mwandhishi kaona noma gani kusema hilo ilihali sasa iwazi kuwa JF iko biased when it comes to CCM v/s CHADEMA na kila mmoja anajua wapi JF inasimama kwenye hili


my 2 cents

Gt Ningeweza kufanya hivyo,ila nilijua naamaanisha CHADEMA kwa maana yako..juzi nilijaribu kuongelea ile thread ya Mtikila ambayo sasa wameamua kuimaliza ila linawahusu.
 
Kuna tatizo ambalo tunalo watanzania wengi hasa tunapokuja katika suala zima la kutatua matatizo.Wengi wetu uwa hatujui lengo kuu la kile tunachokifanya.I mean we don't know the goal most of the time though we pretend to know it.You know what is the result,most of the time we work on the objectives rather than on the goal which make you find yourself helpless after time t and think about to change the route to archieve the goal you don't know.

Na hiki ndicho kinachotokea katika vita hii dhidi ya ufisadi,you can see inaanza kupoa na wapiganaji wengi wameanza kukosa nyimbo huku wakirudia yale yale yaliyokwisha semwa,vita inapoteza flavor.Unajua kwa nini? Kwa sababu wengi wetu tuliamini vita dhidi ya ufisadi itamkomboa mtanzania hivyo kumuondolea matatizo aliyonayo kama si kumpunguzia,kitu ambacho si kweli.Vita dhidi ya ufisadi ilikuwa one of the objective for attaining the goal of liberating tanzanians,sisi tukaweka nguvu zetu huko tukasahau kuzifanyia kazi objectives zingine.

Muheshimiwa Gembe,amegundua vita hii ni ngumu na mbaya zaidi hata kama umeshinda inaweza isiskupe matokeo unayoyategemea.Ebu fikiria,tangu Lowasa amejiuzulu mtanzania wa kawaida amefaidika nini au kuvunjwa kwa mkataba wa richmond kumemnufaisha nini yule mtanzania anaekaa manzese,kinyume chake maisha ndo yanazidi kupanda.Simaanishi vita dhidi ya ufisadi haina maana,la asha.Ninachotaka kutaadharisha tusitegemee vita dhidi ya ufisadi pekee yake itamkomboa mtanzania.

Muheshimiwa Gembe alichofanya ni kuleta objective nyingine,tuwe makini tusije tukahama wazima wazima na kulifanya ndo lengo.

Haya ni mawazo yangu
 
Lets not hide around the bush

correct header ingekuwa Uvumilivu wa wana CHADEMA V/S Ubabe wa CCM


sasa sijui mwandhishi kaona noma gani kusema hilo ilihali sasa iwazi kuwa JF iko biased when it comes to CCM v/s CHADEMA na kila mmoja anajua wapi JF inasimama kwenye hili


my 2 cents

Duh! Mshkaji naona una BIFU la maisha na JF. JF imekufanyia nini mzee?, urudishiwe u moderator nini!!! LOL

Wewe kuwepo humu, ES, Mimi, Masatu ni dalili tosha kuwa sio wana Chadema ndo tu wapo humu.

Kama unaona Chadema wamezidi humu kwa uwingi kwanini husi recruit wana CCM kwa wingi tupeane TAFU kuwapiga vita au kujibu hoja za CHADEMA?

Do something acha majungu na kuchochea yasiyokuwapo humu JF. Pia ukiona vipi unaweza tu kuishia kimya kimya kuliko kupika majungu ambayo hayatoiva.
 
Mimi naona wana JF mapambano haya dhidi ya ufisadi yanatakiwa yapigwe kwa kila kona. Bwana Gembe wazo lako la kwenda jimbo hadi jimbo ni zuri lakini resources hakuna. Dawa ni moja tu, na historia inatuambia kuwa mapinduzi yoyote ya nchi hayafanywi na watu wa vijijini isipokuwa wa mijini. Hakuna njia nyingine tupaswayo kuokolewa kwayo isipokuwa kuishinikiza serikali ya ccm kwa maandamano na mogomo. Kuendelea kujadili tu hapa JF bila vitendo haisaidii kitu, ni lazima imani iendane na vitendo. Na lazima tukubali kuwa hakuna ukombozi unaokuja bila watu kutolewa kafara, sasa wana JF na watanganyika kwa ujumla tuache woga tuingie barabarani tuindoe serikali hii ya kisanii. CUF wameitisha maandamano makubwa mwezi October kudai mafisadi wafikishwe mahakamani kwa nini sote tusiungane nao kuandamana hata kama Kova atakataa sisi twende tu. Nina imani kuwa kama watu 100,000 watajitokeza barabarani hata kama jeshi lote litakuja halitatuweza. Maandamano yafanywe katika miji yote ya Tanzania na hapo ukombozi utapatikana.

Mimi nasema kama tutaendelea kujadili tuhumu na kudhani kuwa kwa kufanya hivyo tutawakomboa watanganyika tunajidanganya wenyewe. Siasa za magazetini na kwenye mitandao ccm wamezizoea na haziwastui. Ni barabarani tu. Napendekeza CUF iandae vizuri mikakati yake, na makundi yote ya watu wahusishwe, makongamano yafanywe kila sehemu mpaka mashuleni ili tuikomboe nchi yetu.

Vinginevyo tusidanganyane
 
Maisha magumu, wananchi wameambiwa wavumilie, halafu fleet ya msafara wa muungwana sasa hivi ni BMW tupu, yaani magari karibu kumi.......!!!! Zile benzi kazichoka ndani ya miaka miwili tu!!!!
 
Maisha magumu, wananchi wameambiwa wavumilie, halafu fleet ya msafara wa muungwana sasa hivi ni BMW tupu, yaani magari karibu kumi.......!!!! Zile benzi kazichoka ndani ya miaka miwili tu!!!!

Tatizo la viongozi wetu ni priority zao ..wanaona ni bora wanunue X5 na waache kabisa kuwalipa walimu na wastaafu.

Kwa maana nyingi kiburi ,ubabe ndiyo umetawala
 
Back
Top Bottom