uvumilivu...



ndugu yanu blackwoman soma post #59 ndipo utakapo jua namaanisha nini.
 
Last edited by a moderator:
nimefika mwisho wa akili zangu nimemwachia mungu maisha na ndoa yangu ailinde mimi siwezi na anailinda kweli kweli ,things are sometimes inevitable only god can,thats why i love him
nivea soma ushuhuda wangu post #59. ndipo utakapojua nisemapo vumilia namaanisha nini.
 
Last edited by a moderator:

Uvumilivu ni kitu kikubwa na ukijijengea uwezo wa kuvumilia utaweza kukabiliana na changamoto nyingi sana kwenye maisha. Ukiona mtu anapandisha kelele kwenye kila kitu ujue bado hajakua...kasheshe akianza kukua when 70 birthday is around the corner. atakuwa amechelewa kwenye kila kitu
 
mhh!! kwanza pole kwa jaribu hilo, hakika mie nisingestahimili.
naona kuwa upendo wako kwa mumeo ni mwingi na ukaamini ukilipa mabaya yake kwa kumtendea mema hatimaye atabadilika. nashukuru kwa hii post, ni watu wachache mno wangeweza kuchukua uamuzi wako kwenye hii situation. umeonesha love conquers all 😀. Mungu akuzidishie moyo huo
 
ndugu yanu blackwoman soma post #59 ndipo utakapo jua namaanisha nini.

nimesoma ndugu yangu nampa hongera mwanamke huyo.......... uvumilivu kwa macho/mawazo ya kibinadamu utabaki kuwa msamiati nithubutu kusema ni kwa nguvu za muumba wetu.
 

duh mpaka mchozi kwa kweli.........hata mama yangu mkubwa yaliyompata yanaelekea kufanana na yako...........mpaka alikuwa kichaa na sasa hivi anatumia dozi na kuhudhulia clinic ingawa anaendelea vizuri lakini muda mwingine anakuwa hajielewi.

Mungu ni mkubwa kwa kweli amemsaidia kwa kiasi kikubwa na sasa anaendelea vizuri na watoto wameshakuwa wakubwa wanaume wameoa na wanawake wanatarajiwa kuolewa hivi karibuni.

Daima tutayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu.
 

ni

ma bro baine n kurt nimejikuta nalia sijui kwanini nimeyasema haya hapa yamenikumbusha mbali sana mimi na wanangu lakini pia nafurahi sana yamebaki historia sasa.
 
Last edited by a moderator:

nashukuru sana sister binafsi nimejikumbusha those days nikaishia kulia palikuwa pagumu sana ndio maana huwaga nasema humu jamvini mara kwa mara makosa ya mume wewe jipe raha tu muda wote watu wanaona natania ni ukweli kabisa. ninaamini hata mama yako mkubwa kama angekuwa anajipa raha kwa kutoka na friends, asingepata msongo mkali kama huo.

nilijifunza kuvumilia kwa kukaa kimya na kushtaki kwa Mungu lakini sikujifungia ndani, nilikuwa natoka naenda kuburudika na marafiki pasi kuwaambia langu la ndani hadi Mungu aliponijibu.
 
Last edited by a moderator:

dah..nimekosa cha kuchagia hapa....
duh....
 
nimesoma ndugu yangu nampa hongera mwanamke huyo.......... uvumilivu kwa macho/mawazo ya kibinadamu utabaki kuwa msamiati nithubutu kusema ni kwa nguvu za muumba wetu.

@blaki woman ni kweli ni Mungu tu siyo nguvu za kibinaadamu ila pia ustahimilivu na hekima vilitumika.
 

Ni kweli kabisa uvumilivu muhimu sana ktk mahusiano but utavumilia untill when? let me give u this story nina rafiki yangu kipenzi ameolewa miaka 3 iliyopita,mume anaishi uingereza akaja kumuoa tanzania baada ya ndoa mume kamwambia vumilia naenda kukushughulikia maswala visa akaondoka akamuacha na mimba ya miezi 2, akarudi tena tz mimba ikiwa miezi 6 still anamwambia vumilia nashughulikia visa yako sasa toka ailivyoondoka mpk mtoto anazaliwa na sasa ana miaka 2 hajamuona tena na kila siku wakiwasiliana anachomwambia mke wangu vumilia! swali avumilie untill when? na visa gani inayoshughulikiwa kwa miaka 3?
kwa mimi uvumilivu ungenishinda.
 
ni

ma bro baine n kurt nimejikuta nalia sijui kwanini nimeyasema haya hapa yamenikumbusha mbali sana mimi na wanangu lakini pia nafurahi sana yamebaki historia sasa.
Amen to that. ukiandika kitabu cha maisha yako utapata wateja, watu wengi hupata moyo wakifahamu mahasibu wanayoyapata yamepitiwa na watu wengine ambao wameyashinda. inatupatia ujasiri wa ziada wa kukabiliana na maisha yetu 😀

 
dah..nimekosa cha kuchagia hapa....
duh....

basi nisemapo vumilia boss simaanish kuwa ni unafiki namaanisha manake i lived that life for about 4 yrs zaid ya sala na kutoka na friends au watoto hujui raha ya ndoa. lakin leo nimesahau huwez kuamini.
 
Last edited by a moderator:

kweli msongo wa mawazo ndo ulimpelekea uko...........hata mimi nilishasema daima ntatabasamu hata nikiudhiwa vipi ...............mana wewe unajipa presha wakati mwenzako anakula raha..........

hakimu sahihi wa hii kesi za ndoa ni Mungu pekee ila kuwajulisha mashost ni mwiko..............yakwangu moyoni atayajua Mungu.

umenikumbusha zaburi pale juu kiukweli uwa zinafariji na kueleza kila kitu........... zaburi ya 138 ni ya shukrani uwa napenda kuitumia hii kama sala yangu ya kushukuru kila siku.
 

hiyo ndiyo suluhu tu ya ndoa sister. nilichoguundua ni kwamba ukileta wanakamati wengi kwenye ndoa yako unaiharibu na pia ukipenda kusikiliza shuhuda za watu za kushindwa manake jamani maisha hayana comaparison
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…