Uvunjifu wa amani

Uvunjifu wa amani

Mtanzanika

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
2,389
Reaction score
1,131
hili neno 'uvunjifu' ni sahihi wakuu wangu?!
Nimekua nikilisikia mno kwenye vyombo vya habari!
Nijuzeni tafadhali!
 
Kwani wewe una mashaka gani na neno hilo? Bainisha tatizo lako wako wanagenzi nguli hapa jamvini watadadavua suala lako kindakindaki.
 
shaka niliyonayo ni hii '-ifu' katika neno uvunjifu.
mimi nilijua 'uvunjaji' tu ndo sawa kumbe mpaka 'uvunjifu' linajuzu!?
nahisi nakosea kila ninapojaribu kulitia katika matumizi.
 
Ni sahihi na linatumiwa mara kadha kuonesha umiliki wa kitendo.
kuna mifano hai mfano: Kaka yule ni mkamilifu (kamili) wa kipato na muadilifu (adili)wa tabia mana si mbadhilifu
Hahaa kiswahili kina raha ....
 
Ikiwa bado hujatosheka kutokana na 'mhadhara' wa sheng, sema ili tubadili mbinu ya uwasilishaji!
 
Ikiwa bado hujatosheka kutokana na 'mhadhara' wa sheng, sema ili tubadili mbinu ya uwasilishaji!

Ahsanteni kwa somo! kwa hivyo pia naweza sema: Kaka yule ni mvunjifu, ama hawa vijana ni wavunjifu wa amani!!
 
Back
Top Bottom