Uvutaji wa sigara 'unaozesha' ubongo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Kuvuta sigara “kunaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo wa kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini Uingereza.



Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.

Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.

Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na kiharusi.

Shirikisho la kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha Cholesterol au

kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri ubongo.

"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…