Uvutaji wa sigara

Uvutaji wa sigara

Tairus

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
676
Reaction score
1,056
Naomba kuhoji
Ivi unapomuuzia mtu sigara na unajua ina madhara kwa afya huoni unatenda dhambi.

Labda hujanielewa.
Naanzia nyuma kidogo;
Unapoamua kuanzisha biashara ya kusambaza au kuuza sigara kimsingi unaipromote izidi kukuwa.
Najua unatafuta hela sawa but in expense of someone's life.Haijakaa sawa.

Utanielewa tuu.
Unapoona mtu anasumbuliwa na mapafu tuseme yametoboka au kalazwa unajisikiaje.
Umesema haujisikii chochote alitaka mwenyewe au tuseme umesema kila mtu atakufa.
Tuanzie apo,angekuwa mwanao au baba yako ungejisikiaje na wewe ndo muuzaji na msambazaji mkuu.
Huna huruma unachowaza ni pesa tuu kwani hakuna biashara nyingine?

Kodi
Sawa mnalipa kodi lakini kodi hiyo hiyo ndo inatumika kununua madawa ya kuja kuwatibia wagonjwa of which was absolute unnecessary.

Ajira
Sijafanyia utafiti kuhusu proportion ya ajira zinazotolewa nilinganishe na idadi ya vifo lakin nadhan kiujumla nguvu kazi ya taifa inatakiwa iwe protected at all cost.

Kabla sijawakilisha
Dhumuni la huu uzi ni kutaka kujua wahusika halisi wa hii biashara huwa conscious yenu iko vipi.Ni kuwa mmejitoa akili au namna gan??

Povu ruksa kuna watu najua wako addicted so watakuwa offended kwa namna flan.



10 Serious Effects of Cigarette Smoking on Environment and Human Health - Conserve Energy Future
 
Nangoja muje alafu siti ya mbele nimeichukua mwenyewe...
 
mbona kiini cha mahindi kinaliwa na panya wakati huo huo na sisi tunataka dona.?
kwahiyo sisi tumekuwa panya ama.!
mambo mengine ni maamuzi tuu hata kama utaumia baadae.
 
This is a capitalist world mkuu. Unakuwa served kile unataka hata kama kina madhara utaambiwa tu kina madhara ila kama unakitaka na unatoa hela hakuna namna tutakupa tu utajua mwenyewe mbele kwa mbele sisi tumeshakunja kimango tumetia mfukoni.

"Uvutaji wa Sigara ni Hatari kwa Afya Yako".

Na bado utakutana na matangazo mengi mazuri ya kuisifia sigara ili ivutie watumiaji.

Kuna wakulima wanaendesha maisha yao kwa kulima tumbaku, wanasomesha watoto wao na kupiga pesa. We vuta tu uchangie wengine.
 
Kwani sigara, pombe,soda kipi kinamadhara zaidi??
 
Madhara anatakiwa kuyaona mtumiaji kabla ya muuzaji mkuu, tukisema watu wasiuze Sigara kisa ina madhara mwisho wa siku watu watakua hawafanyi biashara maana kila kitu kina madhara yake
 
This is a capitalist world mkuu. Unakuwa served kile unataka hata kama kina madhara utaambiwa tu kina madhara ila kama unakitaka na unatoa hela hakuna namna tutakupa tu utajua mwenyewe mbele kwa mbele sisi tumeshakunja kimango tumetia mfukoni.

"Uvutaji wa Sigara ni Hatari kwa Afya Yako".

Na bado utakutana na matangazo mengi mazuri ya kuisifia sigara ili ivutie watumiaji.

Kuna wakulima wanaendesha maisha yao kwa kulima tumbaku, wanasomesha watoto wao na kupiga pesa. We vuta tu uchangie wengine.
Sio ivyo siku zote,madhara yanangaliwa sema hili mmelipuuzia.
Mfano Fiesta haijafanyika leaders kwa sababu ni karibu na hispitali na watu wanaweza kufa sababu ya kelele...sasa huoni apo wamezingatia afya za watu au unataka kusema pale kuna maslahi binafsi.

Same capitalism you are talking about..
 
Kuna jamaa bodaboda kitaani ...alikuwa kaandika nyuma ya pikipiki yake.. "niacheni kama nilivyo"....sasa siku moja kakimbiza pikipiki akaanguka vibaya mno... sasa watu wote wanapita wanamuacha!...
Kumbe walisoma Yale maandishi nyuma ya pikipiki!... na wakamuacha kama alivoandika
 
Back
Top Bottom