Ni biashara ngumu sana ambayo inahitaji wewe mwenyewe uwe na uzoefu nayo otherwise uwe na mtu mwaminifu sana aisimamie. Unataka kuvua wapi? kama baharini je ni uvuvi wa maeneo ya pwani au mbali na bahari? na pia unataka kuvua uvuvi wa aina gani yaani samaki gani.. kuna uvuvi wa dagaa (utahitaji boti kubwa kidogo yenye injini ya ndani na nyavu za purse seine), uvuvi wa nguru na papa kwa kutumia mishipi au kwa kutumia nyavu za jarife n.k.
Kama nilivyosea sio tu kununua boti na injini bali pia kujua unaenda kuvua nini na wapi ndio itakusaidia kujua aina gani ya nyavu, boti na injini ya kufunga. Kama ni mgeni kabisa unahitaji watu wazoefu mno na waaminifu wakuelekeze vinginevyo unaweza ingizwa mjini.