Uwajibikaji hauko ‘Twitter’ pelekeni hoja bungeni

Uwajibikaji hauko ‘Twitter’ pelekeni hoja bungeni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Tumewachagua wabunge au viongozi kidemokrasia, tukitarajia watakuwa wajibikaji na kutusemea huko kwenye vyombo stahiki kama Bunge.

Hali imekuwa tofauti kwa wabunge wengi ambao mara nyingi wamekuwa wakija kuandika kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kujibizana na wananchi au kujitetea kuhusu mambo tofauti tofauti.

Wengine huwa wanakubaliana na mambo bungeni na wakitumbuliwa huwa wanakuja ‘Twitter’ na kupost kuwa hakukubaliana na jambo fulani, wakati kipindi linapitishwa hakuonyesha kupinga bali alipiga makofi huko bungeni.

Uwajibikaji uwe kwa vitendo na sio maneno tupu kwenye mitandao ya kijamii. Kama mbunge hakubaliani na jambo husika huko bungeni ni vyema akasimama na kuonyesha msimamo wake na sio kuwa kigeugeu wa kukubali bungeni na kuja kukataa Twitter.

Amehitimisha kwa kusema mitandao ya kijamii sio bunge.
 
Back
Top Bottom