martialmtata
New Member
- Jul 22, 2023
- 3
- 2
Jibu kwangu ni hapana, kwangu naona Tanzania haihitaji katiba mpya sio kwasababu katiba ya sasa hivi ni nzuri hapana. Kuna kitu nahisi Bado hakipo sawa kwanza tujikumbushe kuwa katiba na sheria za nchi zinalindwa na wananchi pamoja na watawala kwa mtazamo wangu ukiacha muhimili wa bunge mahakama na utawala kunatakiwa kuwe na muhimili wa wananchi (bunge Bado halijatosha kuwa wawikilishi wa wananchi) hawa wote wanatakiwa kuhakikisha kwamba hakuna anaevunja hizo sheria na katiba, lakini kwa Tanzania mambo hayajawa hivo bado Kuna kitu kikubwa kabla ya katiba kinatakiwa kifundishwe kwa wananchi kwa mfano
Sheria bila power hakuna sheri, hata kama utakua na sheria nzuri vipi bila wananchi kuwa na power hakuna kitu utakachokifanya. Fikria mara ngapi kwa hii katiba na hizi hizi sheria mara ngapi watawala wamezisigina, Mara kibao fikiria kuhusu polisi na watendaji wengine wa Serikali walivozisigina hizi sheria, je Kuna Chochote kimetokea hapana, na Kuna wakati watawala wamekua wakijinasibu kwa kukutimizi haki za kikatiba kama hisani, si unakumbuka kuhusu mikutano ya vyama vya kisiasa ni kitu kilichukuliwa na kurudishwa kama hisani na ikahitajika na pongezi
Je nini kimefanyika juu Yao? hakuna kitu. Mara ngapi askari wamefanyia watu manyanyaso na nini kimefanyika dhidi yao, jibu litakua ni mara kibao na hakuna Chochote kilichofanyika. Na vipi kuhus hizo mahakama amabazo nazo tumekua tukizitegemea? Ni mara ngapi zinalalalamikiwa kutokutoa haki na maamuzi Yao kuingiliwa na serikali, jibu pia ni mara kibao Je tatizo ni ukosefu wa elimu? hapana, mara ngapi hao wasomi (elites) wametapeliwa haki zao? si walikaa miaka saba bila kupandishwa madaraja na walikua kimya, sina takwimu sahihi za watu wenye elimu msingi lakini nina hakika ni wengi kama elimu angekuwa mkombozi basi tungekua tushaanza kuona ukombozi lakini Bado hakuna hata dalili ambazo zinaonesha kwamba Kuna sehemu tunaenda. Au pia ni tatizo la mfumo wa elimu, zaidi yakuwa na vijana wenye sifa za kusifia na kulamba watawala na watu walifanikiwa ili waweze kwa pengine kujinufaisha wao binafsi( personal interest) Kwa kifupi taifa linavijana wengi ambao binafsi hawawezi kujitegemea
Report ya CAG si hio imetoka, watu wamepiga pesa za kutosha. unaona bunge wamechukua hatua zozote za haraka dhidi ya ubadhilifu uliofanyika. hapana ni zaidi ya kuambiwa wananchi tusubiri mwezi wa kumi na moja. Watu wamekwapua pesa za serikali na wametulia. wanajua watu watapiga kelele na usiku watalala hakutakua na jipya jingine zaidi ya kelele za mtandaoni na maisha kuendelea kama kawaida( keyboard warriors). Hata kama wewe ni kiongozi amabae upo kwasababu ya manufaa binafsi unaachaje kufanya ubadhilifu Ile hali unajua hakuna wakukuwajibisha.
Tozo zilkuja mfumuko wa bei ukaja uliona chochote kilichotokea. watu walipiga kelele nyuma ya batani na maisha yakaendelea. viongozi washajua hao ndo watu wanaowaongoza na hakuna kitu kinaweza kuwawajibisha Kuna kero nyingi za kijamii zinatokea mtaani lakini wananchi pamoja na viongozi wote wako busy na mambo Yao, je unahisi katiba tu bila usimamizi wa nguvu ya wananchi vitaweza kujibi hayo maswali? kwa mfano Kenya wanakatiba nzuri kuliko sisi lakini wananchi kila siku wanajitaidi kuiwajibisha serikali kama wangeamua kukaa na kupiga kelele mtandaoni sizani kama katiba yao nzuri pia ingewasaidia
Sizani kama katiba itakuja kujibu haya matatizo.kwa mfano hiyo katiba mpya ikaletwa na ikakanyagwa kama hii. je nini kitafanyika? nani atawawajibisha watawala kama wao kwa wao hawataamua kuwajibishana, nani atawawajibisha? kwasababu tunajua mwananchi wa kawaida akivunja sheria atawajibishwa na utawala je mtawala akikosea na watawala wakamua kulindana wao kwa wao bila kuwajibishana nini kitatokea? Haya katiba iyo mpya nayo imevunjwa nini kitafanyika.
Hakuna nguvu ya wananchi nchini ni kama nchi ya kifalme lakini sio. kwenye nchi ambayo wananchi ndio wako na power kwa katiba hii hii ilitosha kabisa kuwawajibisha watawala dhidi ya ubadhilifu wa mali za umma pia hata utawala usiofuata sheria lakini bado tunaendelea kuona futuhi kama hizi ambazo hakuna asiyejua kama ni tatizo, nguvu pekee tuliyobaki nayo sasa wananchi pamoja na vyama vya upinzani ni maridhiano, ambayo nayo yanategemea huruma ya mtawala kama mtawala hatakua tayali kwa maridhiano inamaanisha hakutakua na Chochote ambacho kitaweza kufanyika kutatua matatizo yanayoikumba jamii
Power ya wananchi inaoneshwa kwa maandamano pamoja na migomo ya amani. Na ni kitu ambacho katiba ya nchi yetu inatambua kama maandamo ni haki ya kikatiba lakini huwezi kuona wananchi wakitimiza takwa hili la kisheria na haki Yao kila mmoja Karadhika na kile kinachoendlea. Tumebaki kutegemea huruma kutoka vyombo vya kimataifa kuiwajibisha nchi kwa kutokutoa misaada. Nashindwa kujua moja kwa moja tatizo ni nini wananchi hawana elimu ya kutosha au tatizo la kiutamaduni, uwoga au haya matatizo hayawagusi wananchi wakawaida ni watu wachache ndio wanaoona
Umeona wananchi wa kawaida wamefanya maandamo. umeona madereva, waalimu, wastaafu (working class) wowote wamefanya migomo, au sio haki Yao kufanya migomo kwa hii katiba? licha yakua haki zao zinakanyagwa. jibu ni hapana, kwaio je watawala watajiuzulu vipi. mamlka zitkua kwenye mgandamizo vipi kuwachukulia watu hatua? au kwa kelele za mitandaoni, sizani.
Vyama vya siasa, asasi za kirai pamoja wadau mbalimbali Bado wanakazi kubwa ya kuona na kutatua tatizo hili kubwa, ilipaswa lianze kutibiwa chanzo Cha tatizo na badae tatizo kwasababu Bado mwisho wa siku hata kama tutatibu hili tatizo la katiba mpya naona Kuna tatizo jingine ndani ya katiba mpya litaibuka na litashindwa kutatuliwa

Upvote
1