Daniel Levert
Member
- Aug 29, 2022
- 16
- 7
UTANGULIZI
Kilimo ni dhana pana inayojumuisha uzalishaji wa mazao, ufugaji na uvuvi. Katika andiko hili nitaangazia kilimo kwa upande wa uzalishaji mazao.
Sekta ya kilimo ni sekta mama ya uchumi wa Tanzania. Huchochea maendeleo ya sekta zingine kama usafiri, viwanda na masoko. Mfumuko wa bei nchini unasababishwa na kuongezeka kwa uhitaji zaidi ya kiwango cha uzalishaji pamoja na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji mashambani. Tanzania ina idadi kubwa ya wakulima wadogo wadogo ambapo wengi wanashindwa kumudu ongezeko la gharama za mbolea, viwatilifu na usafiri. Ongezeko la gharama za uzalishaji, umbali wa masoko na ubovu wa miundombinu imepelekea wakulima kupunguza uzalishaji, wengi wanazalisha mazao kwa mahitaji ya chakula cha familia tu. Kiwango kidogo kinachopatikana huleta ushindani mkubwa katika masoko na kupelekea mfumuko wa bei.
Sekta ya kilimo huathiri sekta zingine hivyo mfumuko wa bei katika uzalishaji wa mazao hupelekea mfumuko wa bei katika sekta zingine na kupanda kwa gharama za maisha kwa ujumla.
UHALISIA MTAANI
Nilitembelea masoko mawili ya Singida mjini maarufu kwa uuzaji wa mazao ya nafaka ikiwemo mahindi, mchele, mihogo, mtama na viazi vitamu. Soko moja linaitwa soko mjinga na jingine soko la mahembe, nilifuatilia zao la mahindi kama mfano. Maelezo ya wafanyabiashara wanaonunua mazao toka kwa wakulima yalifanana. Mei 2021 wafanyabiashara hawa walinunua debe la mahindi kwa wakulima kwa 8,000/= Tshs ,septemba 2021 debe lilipanda hadi Tshs 10000. Mei 2022, wafanyabiashara hawa walinunua debe moja la mahindi kwa 10,000/= Tshs , hadi 1 Septemba 2022 walinunua debe kwa 16000-17000/=Tshs kutoka kwa wakulima kukiwa na makadirio ya ongezeko la bei kwa asilimia 40 ikifananishwa na mfumuko wa bei ya mwaka 2021. Bei hutegemewa kupanda zaidi kipindi cha masika ikikadiriwa kufika 150,000/=Tshs kwa gunia moja la mahindi 2022.
picha halisi sokoni
Hadi April 2022 serikali kupitia wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) ilifanikiwa kuhifadhi takribani tani 198,496.165 za chakula katika ghala za taifa (Nukuu kutoka bajeti ya kilimo mwaka wa fedha 2022/2023).
Bajeti inaonesha utoshelevu na usalama wa chakula na lishe nchini ilihali watanzania wengi wanashindwa kumudu kupata lishe bora kutokana na gharama za vyakula kupanda sana, mavuno duni na hali zao zinazidi kua duni.
MAPENDEKEZO
Serikali kupitia wizara ya kilimo izingatie na iimarishe uhusiano mzuri na kampuni binafsi ambazo zimepiga hatua kubwa katika kilimo binafsi mfano MeTL. Pia kuzingatia mchango wa asasi za kiraia zisizo za kiserikali zinazofikiwa na watanzania wengi mfano Jamii Forums na Twaweza katika kusambaza taarifa za dira na sayansi ya maendeleo ya kilimo . Hii itasaidia kuongeza njia za kutatua changamoto zinazokumba kilimo cha Tanzania na uchumi kwa ujumla.
Iundwe tume huru nje ya jukwaa la siasa. Tume huru nje ya mifumo ya siasa itasaidia katika kutekeleza majukumu ya nchi kwa ajili ya watanzania wote bila kujali msimamo wa kiongozi fulani wala itikadi ya chama fulani. Tume ipewe uhuru wa kuratibu majukwaa mbalimbali na majadiliano ya matumizi ya fedha ili kutoa mapendekezo serikalini kabla ya fedha kuelekezwa katika miradi mbalimbali. Tume iwe na wataalamu wa uchumi ili kusimamia bei elekezi ya mazao na bidhaa zake maana thamani halisi ya ukuaji wa fedha yetu katika soko la dunia haiendani na thamani halisi ya mfumuko wa bei
Serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknolojia iyape kipaumbele masomo ya kutumia utashi wa binadamu kuanzia taaluma ya elimu msingi. Somo la kilimo lingewekwa katika mtaala ili kuongeza ushindani na ujuzi katika kilimo.
Kutoa elimu kwa wakulima katika njia rafiki zaidi kuhusu kilimo cha kisasa na mazingira kitakachowawezesha kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa inayoathiri ikolojia za asili na uzalishaji wa mazao. Serikali, makampuni na wadau mbalimbali wa kilimo wawatembelee wakulima mashambani na si katika majarida tu. Pia katika kukabiliana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, serikali iongeze ruzuku kwa wakulima mashambani wenye uwezo mdogo wa kumudu gharama za viwatilifu, mbolea na mahitaji mengineyo.
Ni ngumu kufikia nchi ya maendeleo ya viwanda na masoko bila kufikia nchi ya maendeleo ya kilimo kwanza, mfano halisi ni mataifa mengi yanayoongoza kwa maendeleo ya viwanda duniani ndio yanaongoza kwa kilimo pia na uuzaji wa chakula duniani mfano China na Marekani. Miundombinu ya mashambani nchini Tanzania ni ya kiwango cha chini swala linaloendeleza ugumu wa uzalishaji na mfumuko wa gharama za uzalishaji. Miundombinu bora ingesogezwa karibu na maeneo ya uzalishaji malighafi.
Kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za kilimo. Seikali iwaamini vijana na kuwapa nafasi kuwasilisha programu zao za maendeleo na kuchangia maamuzi. Ikumbukwe vijana ni kundi linaloathiriwa na mabadiliko ya sasa lakini litaendelea kuathiriwa maana vijana ndio viongozi wa kesho hivyo wapewe nafasi.
Tanzania ina takribani hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo, kati ya hekta zote ni takribani hekta milioni 10.8 tu sawa na asilimia 24 ndizo zinazolimwa kwa mwaka(wizara ya kilimo,2017).
Serikali ingeongeza hekta zingine kwa ajili ya kuwapa vijana fursa maana imekua ni kilio kikubwa kwa vijana kukosa ajira huku wakiitwa wavivu kua mali ipo shambani hivyo wakajiajiri, mashamba ambayo wengi hawajui wanaanzia wapi kuyapata. Serikali ingefungua milango kwa kuwekeza katika kufungua mashamba mapya ili kuongeza wigo wa soko la ajira na uzalishaji kwa vijana. VIJANA TUKIWEZESHWA TUNAWEZA, TUFUNGULIENI MASHAMBA TUCHAPE KAZI.
picha kutoka mtandaoni
HITIMISHO
Kutokana na takwimu za shirika la chakula na kilimo duaniani(FAO) mwaka 2018 inaonyesha kufikia mwaka 2030 biashara ya chakula itakua juu zaidi kufikia dola za kimarekani trilioni 1. Kwa upande mmoja ni taarifa nzuri sana , kwa upande mwingine ni onyo, taarifa hii inaweza kua nzuri ama onyo kwa taifa husika kutokana na hatua itakazoamua kuchukua katika uzalishaji na usimamizi wa mazao kuelekea 2030.
Kilimo pekee hakiwezi kutokomeza umaskini na kukabiliana na mfumuko wa bei ila kinaweza kutumika kama nyenzo kuu ya kuunganisha sekta zingine ili kuleta uchumi thabiti. Natoa wito kwa wataalamu na wadau wote kutoka idara za sera na mipango, wizara ya kilimo, viongozi wa serikali kuu na watunga sheria wa nchi kufumbua macho kutizama mbali zaidi ili kufanya uaamuzi bora leo na kutoa mwongozo mzuri kwa ajili ya kesho ili ifikapo 2030 tuwe na utoshelevu unaoonekana wa mazao kwa chakula pamoja na biashara.

Upvote
10