Uwamuzi wa kumfukuza Miguel Gamondi ulikuwa wa kukurupuka!

Uwamuzi wa kumfukuza Miguel Gamondi ulikuwa wa kukurupuka!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
Watanzania ni watu ajabu ajabu sana!

Hatuna uvumilivu ,ni watu wa papara, majungu na fitina sana! Kufungwa mechi mbili tu unamfukuza Kocha!
Manara naye mtu wa fitina na Unafiki sana!

Kisa Gamondi asalimiani naye , wamefanya fitina Hadi wakamfukuza.

Mnamfukuza Kocha aliyekwisha Jenga kikosi imara kwa ajili ya mashindano ya ndani na Kimataifa!

Soma Pia: FT: Young Africans SC 0 - 2 Al Hilal | CAF CL | Benjamin Mkapa Stadium | 26.11.2024 |

Kocha mmemleta Said Mnyamwezi! Kuna Mjerumani anaitwa Said?! Ona sasa aibu tuliyopata Wana Yanga kwa kupigwa 2 kwa mtungi Tena nyumbani!

Gamondi angeshinda mechi hii asubuhi sana!

Aibu ziwaendee viongozi wote wa Yanga kwa ubabaishaji huu!
 
Back
Top Bottom