Uwanja mkuu wa Taifa ni wa Simba na Yanga

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kinadhalia uwanja mkuu wa mpira ni mali ya Serikali, hivyo ni mali ya watanzania wote, lakini kiuhalisia aliyebuni wazo la kujenga uwanja ule kichwani mwake alikuwa ana picha ya kujenga uwanja wenye hadhi, ukubwa na miundombinu inayotosheleza mahitaji ya Simba na Yanga na mashabiki wao wa dar es salaam. Hivyo kiuhalisia uwanja ule ni mali ya Vilabu vya Simba na Yanga nchini ambavyo vina mashabiki wengi wa aina na ngazi zote za kijamii nchini, na ndiyo maana vilabu vingine vinaruhusiwa kuchezea viwanja vingine kama vya Azam, Karume, n.k isipokuwa Simba na Yanga.

Kama mashabiki wa Simba na Yanga wakiuharibu uwanja wao ni kosa kubwa sana lakini adhabu yao haiwezi kuwa kuzifungia Simba na Yanga kuutumia uwanja wao. Hii ni sawa na kesi ya mbuzi wa Bwana Heri waliokula mazao kwenye la shamba la Bwana Heri, yaani mbuzi wa Bwana Heri na shamba la Bwana Heri, utaiamuaje hiyo kesi?

Badala ya kusema Simba na Yanga wasikanyange tena uwanja wa Taifa kitu ambacho hakiwezekani, ingekuwa vizuri wasimamisi wa mpira na uwanja wakafanya yafuatayo:

1. Kutoa elimu ya mara kwa mara kwa watanzania kuhusu umuhimu wa uwanja ule kwao na madhara na adhabu za kuuharibu uwanja (information is power)
2. Kuondoa na kudhibiti viashiria vyote vinavyoweza kusababisha mashabiki kuuharibu uwanja ule kama vile vileo ndani na nje ya uwanja, marefa wabovu au wasio waadilifu kuchezesha mechi kwenye uwanja ule. Zile baa pale karibu na uwanja ziondolewe kabisa, maana zinasababisha mashabiki waingie uwanjani wakiwa tayari wameshalewa.
3. Uwanja kuwa na kamera za kumulika mashabiki na wachezaji wote uwanjani na vyooni.
4. Uwanja kuwa na askari wake wenyewe wanaojitegemea kulinda uwanja ambao kazi yao itakuwa ni kulinda uwanja wakati wa mechi badala ya wao kuwa watazamaji pia.
5. Kutoa adhabu kali sana kwa refa, mchezaji, mashabiki na club ambao watakuwa chanzo cha ghasia na kuharibu mali za uwanja.
6. Kutoa adhabu kwa club kucheza mechi kadhaa bila kuwa na mashabiki wao

Haitoshi kusema Simba na yanga wasicheze pale, wakachezee wapi na uwanja ule umejengwa kwa sababu yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…