Sidhani kama serikali inatambua umuhimu wa michezo katika kutengeneza ajira na muendelezo wa soka kwa kuwa na viwanja bora. Kwa mfano mpira sasa hivi umeajiri vijana wengi achilia zile ajira ambazo si za moja kwa moja.
Fikiria kwa mfano Simba wametia nanga jijini Mwanza kucheza mechi yao hapo. Biashara nyingi za mahoteli, migahawa, mama ntilie, mabasi, boda boda, bajaji, wauza jezi n.k. wote hawa hufaidika na ujio wa timu kama Simba. Mzunguuko wa pesa unakuwa mkubwa ghafla achilia mbali ukweli kwamba hii ndio ligi pendwa katika ukanda huu. Sasa kama Zambia, Kenya, Uganda, Burundi, mitandaoni n.k. wanafuatilia ligi hii kwa ukaribu, iweje tuwe na viwanja vibovu? Sababu mojawapo iliyomkimbiza Calinho ni hivi viwanja vibovu na inasemekana alikuwa anapata shida sana kucheza katika viwanja hivyo.
Kama tunataka soka letu liendelee ni lazima turekebishe viwanja hivi.
Hongera Azam kwa kututoa kimaso maso katika suala la kurusha matangazo mubashara lakini viwanja ndio bado changamoto.