Uwanja wa gwambina unamilikiwa na nani?

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Kupitia mpira wadau wa mpira wilaya ya Misungwi mkoani mwanza wameamua kujenga uwanja mpya wa kisasa zaidi ambao uko nje kidogo na jijini la Mwanza wenye uwezo wa kubeba zaidi ya watazamaji elfu kumi na moja.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo ambao uko katika hatua ya mwisho meneja wa ujenzi Bw.Nyanda Mnyeti amesema kuwa walianza ujenzi kwa na mkandarasi mwingine ambaye alizungushia tofali na baadae wakapata mkandarasi mwingine ambaye alichimba na kuweka udongo ambayo unaofaa kwa ujenzi kama tofauti na awali.

Ameongeza kuwa uwanja huuo ni wa kisasa kwani ujenzi wa uwanja huo wamejifunza kupitia viwanja vya nje ya nchi ambapo maegesho ya magari yatakuwa nje wakati wa mechi huku makazi ya kocha,Viongozi na wachezaji watakuwa wanaishi karibu na uwanja ambapo kuna nyumba (Hostel) zao tayari za kuishi.
(Hii ni kwa mujibu wa tarifa za awali zizonikuliwa toka kwenye magazeti ya michezo)

Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000.

Akifafanua chanzo cha fedha killipopatikana kwaajili ya ujenzi huo, Mnyeti amesema alikopa Benki ya CRDB shilingi 300,000,000 kwaajili ya kujenga pitch na kiasi kingine aliuza magari yake binafsi 4, akapata shilingi 300,000,000, pia alisema alimuomba mke wake wauze gari yao ya kutembelea ndipo wakapata kiasi kilicho baki cha kumalizia uwanja huo.



 
Kazi nzuri sana Mnyeti! Mo na pesa zake anashindwa kumalizia Bunju!!
 
Juzi tu kwenye kikao chake nilimsikia akieleza juu ya jambo hili akiwashawishi wenzake wafanye kwenye maeneo yao. Kazi nzuri so far
 
Uwanja mzuri ila una mapungufu madogo..kwa mfano..uzio ni muhimu kuzunguka pitch..lakini pia naona hata lango la kuingilia uwanjani ni moja...
 
Hongera sana Mnyeti lakini usitufanue wajinga.

Huko kukopa CRDB ni geresha tu na wanasiasa karibu wote huwa mnafanya hicho kiini macho.

Pili unauza magari manne unapata milion 300,000,000 hayo ni magari ya aina gani uliyokuwa ukimili Mnyeti mpaka used magar manne upate hiyo pesa?

Mnyeti biashara ya madiwani kule Arumeru ilikulipa sana lakini tunashukuru umewekeze kwenye jamii.
 
Siyo hiyo tu na dhahabu ya wambulu huko Basotu nasikia anaitafuna kishenzi akishirikiana na wasukuma wenzangu
 
Mnakurupuka sana ku-quote minyuzi! Wewe mleta kaandika Bw. Nyanda Mnyeti wewe unamjadili Alexander Mnyeti!

Kuweni makini na maandishi!
 
Amejitahidi sana RC kwa kuhakikisha misungwi wanakuwa na uwanja muhimu ni kuweka uzio ili mashabiki wasiingie kwenye pitch
 
Juzi tu kwenye kikao chake nilimsikia akieleza juu ya jambo hili akiwashawishi wenzake wafanye kwenye maeneo yao. Kazi nzuri so far
Kwa nn hakuujenga Babati huko Manyara ambako ni mkuu wa mkoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…