Uwanja wa Ndege wa Bukoba bado umefungwa. Huduma zaweza kurejea Ijumaa

Uwanja wa Ndege wa Bukoba bado umefungwa. Huduma zaweza kurejea Ijumaa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Uwanja wa ndege wa Bukoba bado umefungwna na hakuna ndege ya abiria inayotua.

Pamoja na Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa jana kueleza umma kwamba ndege zinaweza kutua, lakini kampuni mbili za ndege; ATCL na Precision hazijapeleka ndege zao Bukoba.

Ndege ya ATCL iliyokuwa itue leo uwanja wa Bukoba saa 5.40 asubuhi na kuondoka kuelekea Dar es Salaam saa 6.10 mchana haikufika.

Abiria waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wamepandishwa kwenye basi dogo na kupelekwa Mwanza.

Jamii Forums iliyokuwepo uwanjani hapo ilisikia matangazo yakiwataka abiria hao kupanda basi lililoandaliwa na kuelekea Mwanza na kwamba watapanda ndege usiku wa leo kuelekea Dar es Salaam.

"Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, abiria wa Air Tanzania watalazimika kusafiri kutoa Mwanza, hivyo kuna magari yameandaliwa ili kuwafikisha Mwanza na ndipo safari ya Dar es Salaam itaendelea, poleni sana kwa usumbufu," ulisikika ujumbe kutoka kwa mhudumu ndani ya uwanja wa Bukoba.

Jamii Forums ina taarifa kuwa ndege za abiria huenda zikaanza kutua na kupaa katika uwanja wa Bukoba kuanzia Ijumaa ambapo ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyotua na kuzama ndani ya Ziwa Victoria, Jumapili - Novemba 6, itakapovutwa na kutolewa eneo na jirani barabara ya kutua ndege (runway).

Jitihada za kuiondoa kabisa eneo jirani na barabara ya kutua zinaendelea.
 
Back
Top Bottom