briophyta plantae
Senior Member
- Feb 18, 2017
- 117
- 132
Uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid ni uwanja wa michezo uliopo katika jiji la Arusha
Uwanja huu hutumika sana kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu (soka)na shughuli nyingine mbalimbali za kitaifa. mchezo wa kwanza wa Futboli ya Kimarekani nchini Tanzania ulionyeshwa katika uwanja huu, ni uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000.
Uwanja huu ulipewa jina hili ili kumuenzi Meya wa kwanza muafrika Kaluta Amri Abeid.
hivi majuzi kumefanyika mchezo kati ya costal unioni ya tanga na azam fc ya dar es salaam, maoni yangu kwa kulinganisha hadhi ya mkoa wa arusha na ikiwa kama kiwanja kilichopo katikati ya mji na wenye historia kubwa basi inaleta mtazamo wa kiwanja cha hovyo kabisa.
licha ya kiwanja kipya kujengwa ndani ya jiji ya arusha haina maana tusahau hichi tulichonacho kwa sasa. Unaangalia mpira kupitia televisheni unaona ni kama wanachezea kwenye shamba lililosahaulika tu. Hivi jukwaa kulipiga rangi mara kwa mara inasaidia nini, si bora wapige tarazo (mafundi wanaelewa) ya rangi mbali mbali zinazovutia..?
Mkandarasi anayejenga uwanja mpya kwanini asipewe sub contract akarabati huu uwanja? Hiyo pitch ya kuchezea nadhani ipo hivyo hivyo kwa miaka yote, haijawahi badilika.
Runway yenyewe ya kukimbia ni ya vumbi na wanariadha wetu wengi wanatoka Arusha na Manyara, aisee ni kituko.
Jiji la Arusha hamuoni hili kweli?
Tafadhali huu uwanja uangaliwe kwa jicho la tatu.

- Majukuwaa yafanyiwe ukarabati na kuongezewa ikiwezekana.
- Vyoo sidhani kama vinakidhi mahitaji.
- Frame zinazozunguka uwanja zikarabatiwe na ziwe uniform kuleta muonekano mzuri.
- Vyumba vya kubadili nguo na mabafu.
- Taa za kisasa kuwezesha mechi kuchezwa hata usiku.
- Runway itengenezwe vzr inavyostahili.