Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kuvurumishwa leo November 21, 2020 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, ambapo Wagosi wa Kaya, Coastal Union, wanapambana na Mnyama Mkali, Simba SC.
Ni mechi kali na ya kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 za mchezo huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu VPL.
Kocha wa Coastal Union Juma Mgunda amesema wao wapo tayari kabisa kwenye mchezo huu, huku akisisitiza kwa wachezaji wake kuwa makini wawapo uwanjani.
Na upande wake Kocha wa Simba SC Sven Vanderbroeck amesema wanatarajia kukutana na ushindani kwani mechi haitakuwa rahisi, lakini tupo tayari kwa mapambano.
Kumbuka mtanange huu wa VPL ni kuanzia saa 10: 00 jioni.. Usikose Ukaambiwa.
Kulipewa Mwana.. Kulitaka Mwana
Update,
Timu ya Simba SC wakiwa ugenini wameitandika bila huruma Coastal Union mabao 7-0 kwenye Ligi Kuu Tanzania VPL' mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco amefunga mabao 3 Hat-Tick, Cloutius Chama mabao 2 huku Dilunga na Morrison wakifunga bao 2 kwa mmoja.