MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Tangu msimu huu wa Ligi uanze, Kwa kiasi kikubwa bodi ya Ligi na vilabu vimejitahidi kuboresha viwanja na kuvifanya walau kuwa na hadhi. Ila pamoja na yote kuna baadhi ya viwanja ni aibu TUPU kwa Ligi namba sita kwa ubora barani Afrika.
Huu uwanja wa Sokoine unaotumiwa na KenGold ni kama shamba la mpunga! Sijajua vigezo gani vilitumika kuupitisha, Ila kiuhalisia haufai hata kidogo! Ni mbovu! Mbovu! Mbovu! Mno! Pitch haina quality, hata jinai ulivyokaa kwakweli inasikitisha sana.
Baadhi ya viwanja vingine kama ule wa Arusha unaotumiwa na Coastal union nao ni mbovu sana, Sijui bodi ya Ligi wako wapi kutazama viwanja hivi. Pamoja na jitihada zilizofanyika kuboresha viwanja vyetu, Bodi ya Ligi mkalitazame na hili pia! Kwani inatia doa na ni AIBU kubwa kwa Ligi yetu inayotazamwa kila kona ya Afrika.