Uwanja wa Taifa kufungwa matangazo ya kidigitali kama uwanja wa Azam wa Chamazi

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuingia ubia na kampuni Mama ya kitanzania ya Formula360 Ltd katika uwekaji wa matangazo ya kidigitali katika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kwa lengo la kuongeza mapato kwa Serikali.

Formula360 Ltd ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikifanya shughuli za utangazaji wa kidigitali na usio wa kidigitali pamoja na kununua matangazo kutoka vyombo vingine vya habari.

Kupitia ushirikiano huo Formula360 itawekeza shilingi Bilioni moja katika ufungwaji wa TV (screen,) kuzunguka uwanja wa Taifa na kutoa nafasi kwa Wadau kutangaza matangazo mengi katika uwanja huo unaobeba mashabiki wapatao 60,000.

Kabla ya makubaliano haya uwanja wa Taifa ulikuwa ukitumia matangazo tuli yenye kiwango na ubora hafifu na ujio wa Formular360 utafanya matangazo hayo kuwa ya kisasa pamoja na kupendezesha uwanja.

Kampuni ya Formula360 Ltd inamilikiwa na kuendeshwa na Watanzania na inaendelea kufungua njia kwa kampuni za ndani kushiriki katika juhudi za kuleta Maendeleo ya Taifa.
#MillardAyoUPDATES
 
Jambo jema sana hili. Ndani ya miaka 2 soka letu limepiga hatua kubwa kwenye uboreshwaji wa miundo mbinu.
 
Sawa lakini wangeanza na pitch, vyoo, na viti vyote vimechoka hii ni sawa na kujipilizia perfume bila kuoga
 
Nilikuwa na shangaa sana kwanini uwanja wa taifa haufungwi screen za pembezoni..

Utafanya uwanja upendeze..
 
Nilikuwa na shangaa sana kwanini uwanja wa taifa haufungwi screen za pembezoni..

Utafanya uwanja upendeze..
Mm bado nashangaa kwa nini screen kubwa za uwanjani hazioneshi matukio ya uwanjani. Yaani ukiwa pale taifa usipoona goli likifungwa ndio basi tena mpaka ukitoka uchungulie you tube.
 
Hongera nyingi kwa hiyo Kampuni.

I wish na Wananchi na sisi siku moja tutakuwa na uwanja wetu wa kuingiza watu elfu 40 hivi kule Kigamboni, halafu ndani yake kuna hayo matangazo ya kidigital yakipendezesha uwanja.

Na siyo porojo tu za viongozi wetu miaka nenda kujivunia mafanikio uchwara kama yale ya unbeaten, kusajili wachezaji wastaafu wa EPL, kuifunga simba, nk.
 
Umeongea vema
 
Sawa lakini wangeanza na pitch, vyoo, na viti vyote vimechoka hii ni sawa na kujipilizia perfume bila kuoga
Vyooni
Watanzania si wastaarabu hata kidogo

Pale Mlimani City vyoo vinakuwa safi sababu watu wanachungwa, kuna watu hukojoa kwenye water sinks
 
Mm bado nashangaa kwa nini screen kubwa za uwanjani hazioneshi matukio ya uwanjani. Yaani ukiwa pale taifa usipoona goli likifungwa ndio basi tena mpaka ukitoka uchungulie you tube.
Zilikuwepo ila hamisi tambwe ndo aliyesababisha zitolewe baada ya kuwafunga simba bao la mkono refa akaita kati wakati kwenye screen kubwa inaonekana jamaa mpira umedunda kwenye mkono.
 
Hiyo bi 1 wangenunua nyasi bandia angala viwanja 2 viwekwe pitches zetu bado ni mbovu sana na hazina mvuto wa kucheza mpira.
 
Hilo haliwezekani kulwa na dotto ni mali ya sirikali haiwezi ruhusu iwe na viwanja wakati inapata pesa kila week zikicheza
 
Watengeneze kwanza ile screen ya uwanjani
Ile ni nzima ila wanaogopa vurugu marefa hawaeleweki,ukitaka kuamini zikipigwa game kubwakubwa za kimataifa wanaiwasha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…