Nahonyo
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 5,550
- 5,379
Uwanja wa uhuru, milango yake ya kuingilia na kutokea watu wa kawaida imewekwa upande wa barabara itokayo Buguruni, kwenda Kurasini. Pembeni mwa barabara hii kuna mfereji mkubwa sana uliejengwa na watengeneza barabara hii, wao sina shida nao kwa kuwa walijenga kabla ya ukarabati wa uwanja huu.
Ila kwa wajenzi wa uwanja wa Uhuru kwa kuwa wameamua kuelekeza mageti ya kuingillia na kutokea upande ule, walitakiwa wazibe baadhi ya maeneo ya mfeji huu, ili wateja wa uwaja huu wapite kwa amani. Wakati wa kuingia kwa kuwa watu wanaingia mmoja mmoja sio shida sana, ila inapofika tukio limeisha hususani mpira, ni kero kubwa sana, watu wanaminyana pale, watu wanaibiana pale, watu wadumbukia kwenye ule mtalo mpaka wanajutia kwenda mpirani. Wakati wa kutoka mtalo ule huwalazimisha watu waminyane sehemu moja, nadhani serikali italiona hili na kulifanyia kazi mapema haraka iwezekanavyo. Kwa ajilli ya kujali afya ya wananchi wake, ambao pia ni wateja wao kwenye uwanja huu.