JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Uwazi, Uingiaji, Usimamizi na Upatikanaji wa Mikataba na Taarifa katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi umebaki kuwa ni changamoto.
Hali hii inazuia wananchi kupata taarifa sahihi, na kwa wakati, hili linapunguza hali ya kujiona kuwa ni wamiliki wa rasilimali zao na kupunguza shauku ya kushiriki kikamilifu katika majadiliano na maamuzi kuhusu usimamiaji wa rasilimali za umma.
Uwazi wa Mikataba ni uwekaji na upatikanaji rahisi wa mikataba inayohusu rasilimali za umma iliyoingiwa kati ya serikali na makampuni.
Mchakato wote wa utayarishaji wa mikataba unatakiwa kuwa wazi, wa haki, na wenye ufanisi tokea hatua za upangaji, utoaji wa zabuni, ugawaji, na utoaji wa mikataba hadi utekelezaji.
Upvote
1