SoC04 Uwekaji Vyoo kando ya Barabara za Kitaifa na Wilaya kulinda Afya ya Wasafiri na Mazingira

SoC04 Uwekaji Vyoo kando ya Barabara za Kitaifa na Wilaya kulinda Afya ya Wasafiri na Mazingira

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
Barabara kama njia kuu ya usafiri
Tanzania ina jumla ya kilomita 181602.2 za mtandao wa barabara, chini ya mgawanyo wa Kilomita 37225.5 barabara za kitaifa (barabara kuu na za kimkoa) na kilomita 144376.5 barabara za kiwilaya (barabara za mtoza, za kulisha na za vijijini). Mtandao huu unatengeneza 80-90% ya safari zote nnchini, yaani njia ya barabara ndio njia kuu ya usafiri na usafirishaji nnchini, (Bodi ya mfuko wa Barabara, Aprili 6 2024). Pamoja na mtandao huu mkubwa wa barabara zingatio la uwekaji wa vyoo kando ya barabara halipo.
Maelezo ya kitabibu juu ya mwili na hitaji la utoaji taka mwili
Kwa mujibu wa ripoti za kitabibu binadamu ana uwezo wa kustahimili kukaa na haja kwa saa 4 mpaka 6, yaani kibofu cha mkojo cha binadamu kina uwezo wa kutunza takribani vikombe viwili vya mkojo yaani 400-700 mililita(www.vinmec.com). Ustahimilivu wa kibofu hiki unaathiriwa na; umri wa mtu( mtoto, mtu mzima,mzee),jinsi, hali ya hewa( baridi/joto) na utimamu wa afya.
Upande wa pili wa shilingi, binadamu anashauriwa kunywa kiasi cha kutosha cha maji kwa siku angalau vikombe 4 hadi 8( 1.5 Lita) kulingana na uzito/ urefu, shughuli zake za siku na mtindo wa maisha.
Picha ya kibonzo cha mtu anaejizuia haja.
IMG_20240503_150156.jpg

Chanzo: Matthew Solan​

Madhara ya kiafya yatokanayo na kuzuia haja kwa muda mrefu
Ukaaji na haja kwa muda mrefu una madhara makubwa katika mwili wa binadamu, baadhi ya madhara haya ni:
•Kutanuka kwa kibofu na ulegevu wa mishipa ya kibofu.
•Kuumiza figo, zoea la mara kwa mara la uzuiaji wa haja huweza kusababisha mawe katika kibofu.
•Maumivu ya mwili.
•Uzalishaji wa bakteria katika kibofu hivyo ugonjwa wa UTI, hii huwapata wale wenye historia ya ugonjwa.
•Kudhalilisha utu wa mtu kwa kushindwa kujizua zaidi.

Madhira hayo hapo juu huwapata watu wenye zoea la kuzuia haja. Kwa upande wa wasafiri na watumiaji wa barabara kundi la wazee, watoto, wagonjwa mfano wenye tatizo la tezi dume na kisukari, wajawazito na watu wengine wamekua wakikumbwa na adha wakiwa barabarani mpaka kufika mwisho wa safari zao. Baadhi ya abiria na watu wemejenga zoea baya la kujizuia unywaji wa vimiminika wawapo safarini mfano maji na sharubati! Hii ni hatari zaidi kwa afya, kwani zoea hili huweza kupelekea tatizo la upungufu wa maji mwilini na hatimaye kufunga choo ama choo kigumu.

Kukwepa haya, taifa halina budi kuja na mpango mkakati wa utoaji wa huduma ya vyoo kwa watumiaji wa barabara. Mfano kwa safari za masafa marefu huduma hii hupatikana maeneo ya stendi ama katika migahawa/hoteli kando ya barabara, hii haitoshi kutimiliza mahitaji ya mwili. Mfano abiria atokaye Dar es salaam-Mwanza atapata huduma ya choo stendi au katika hoteli ama akilazimisha sana atajisaidia maporini kando ya barabara! ikichagizwa na semi maarufu ya "kuchimba dawa", hali hii si sahihi ki afya na kimazingira.​
Zoea la "kuchimba dawa" yaani kujisaidia kando ya barabara ni hatari kwa afya na usalama wa mazingira, hivyo hitajiko la usimikaji na ujenzi wa vyoo kando ya barabara kuingia.
Muundo wa vyoo kando ya barabara
Vyoo kando ya barabara vinaweza kuwa katika mfumo wa:​
•Vyoo vya kudumu.
•Vyoo vya kuhamisha
Hivi ni vyoo vya kukokotwa na gari na kuweka sehemu kwa muda maalumu.
Picha ya choo cha kuhamisha​
IMG_20240503_150059.jpg

Chanzo: Picha toka mtandaoni(google)​

Utolewaji wa huduma ya choo kwa watumiaji wa barabara utakua chini ya usimamizi wa mawakala wa barabara, halmashauri na wadau wengine wa maendeleo.

 Barabara za Kitaifa( barabara kuu na za mkoa)
Wakala wa barabara nchini TANROADS- kwa kushirikiana na wadau wawe wahusika wakuu wa usimamizi na uendeshaji wa vyoo katika barabara hizi. Tenda zitolewe kwa wabia katika utoaji wa huduma kwa kusimamiwa na TANROADS.

Barabara za kiwilaya(za mjini na vijijini na za kulisha)
TARURA kwa kushirikiana na halmashauri kupitia idara za maji safi na usafi wa mazingira wapewe jukumu la utoaji wa huduma hii.
Hawa watahusika na:

•Ujenzi wa vyoo na miundombinu yake.
•Kuhudumia vyoo
•Kusimamia na kukarabati miundombinu yote ya vyoo katika maeneo yao.
Mambo ya kuzingatia wakati wa uwekaji wa vyoo kando ya barabara.
Uwekaji wa vyoo kando ya barabara uzingatie mambo yafuatayo;
•Umbali
Umbali kati ya choo toka kituo A hadi B, hesabu zipigwe na usanifu ufanywe kwa kuzingatia ushauri wa kitabibu yaani kwa muda XXY mtu anaweza kuzuia haja hivyo choo A kitaweka kilomita X na choo B baada ya kilomita Y kwa kuzingatia mwendo wa gari kwa saa.

•Makundi ya watumiaji wa barabara na mahitaji yao. Kitabibu wazee, watoto na watu wenye kesi za upasuaji wa vibofu ama historia ya magonjwa ya kisukari na UTI wanahitaji huduma ya mara kwa mara utoaji taka mwili.

•Miundombinu rafiki
Miundombinu rafiki kwa kundi la watu wenye mahitaji maalumu haina budi kuwepo.Pawepo vyoo vya kawaida na vyoo vyenye miundombinu rafiki kwa kundi la wahitaji. Miundombinu kama:
•Vyoo vya kukaa
•Vyoo vyenye ngazi /njia za baiskeli za walemevu.
•Jinsi
Vyoo vya wanaume na wanawake vitenganishwe kwa umbali maalumu utakaoamuliwa na wataalamu wa ujenzi. Pawe na wahudumu wa jinsi zote mbili katika maeneo ya vyoo kuhudumia watumiaji wa barabara.
•Mazingira
Tathmini ya athari za kimanzingira zifanyike kabla ya ujenzi wa choo. Maeneo vyoo vitakapo wekwa visisababishe madhara kwa mazingira kuvizunguka.
Changamoto zinazoweza kujitokeza na jinsi ya kukabiliana nazo.
•Gharama za uendeshaji na miundombinu.
-Bajeti zitengwe mahsusi na kuelekezwa katika huduma hizi. Fedha za miradi ya barabara zijumuishe gharama za ujenzi wa vyoo na miundombinu wezeshi.
-Kandarasi za ujenzi wa barabara ziwatake wajenzi kuzingatia uwekaji wa vyoo kwa kadri ya mahitaji.

•Ustaarabu na uharibifu wa miundombinu.
Zoea la "uchimbaji dawa"/kujisaidia kando ya barabara katikati ya safari linapaswa kukomeshwa kwa utoaji wa elimu kwa umma kwenye vituo vya mabasi na kwenye mabasi na kwa kutumia vyombo vya habari.
Wanajamii wafundishwe uzalendo na kupenda mazingira yao sambamba na kulinda miundombinu ya vyoo.
Zoea la kujisaidia kando ya barabara ni la aibu na hatari kwa afya na ni uchafuzi wa mazingira hivyo halina budi kukomeshwa.​
Faida za uwepo wa vyoo kando ya barabara
Uwepo wa vyoo kando ya barabara hizi (za kitaifa na kiwilaya) kutakuja na lukuki ikiwemo;
•Kuzuia magonjwa na kulinda afya ya wasafiri.​
•Kutunza mazingira
•Kufurahia safari kwa wasafiri Abiria katika safari hawatarazimika kujizuia kutumia vinywaji na kujibana kwa kuogopa adha, fedheha na aibu safarini.​
 Hitimisho
Ni rai yangu kwa serikali kuja na mfumo wa utoaji wa huduma hii muhimu ili kulinda afya ya watumiaji wa barabara na mazingira. Hii ni karne ya jamii iliyostaarabika kujisaidia vichakani( uchimbaji dawa) hakuna nafasi. Shime kwa kandarasi wa barabara kuzingatia ujenzi wa miundo mbinu ya vyoo kando ya barabara kulinda afya na mazingira yetu.​
 
Upvote 1
Tanzania ina jumla ya kilomita 181602.2 za mtandao wa barabara, chini ya mgawanyo wa Kilomita 37225.5 barabara za kitaifa (barabara kuu na za kimkoa) na kilomita 144376.5 barabara za kiwilaya (barabara za mtoza, za kulisha na za vijijini). Mtandao huu unatengeneza 80-90% ya safari zote nnchini, yaani njia ya barabara ndio njia kuu ya usafiri na usafirishaji nnchini, (Bodi ya mfuko wa Barabara, Aprili 6 2024).
Takwimu kama kawaida huhuuuh!

Madhira hayo hapo juu huwapata watu wenye zoea la kuzuia haja. Kwa upande wa wasafiri na watumiaji wa barabara kundi la wazee, watoto, wagonjwa (wenye kisukari) wajawazito na watu wengine wamekua wakikumbwa na adha wakiwa barabarani mpaka kufika mwisho wa safari zao. Baadhi ya abiria na watu wemejenga zoea baya la kujizuia unywaji wa vimiminika wawapo safarini mfano maji na sharubati! Hii ni hatari zaidi kwa afya, kwani zoea hili huweza kupelekea tatizo la upungufu wa maji mwilini na hatimaye kufunga choo ama choo kigumu.
Kisha sayansi
Kukwepa haya, taifa halina budi kuja na mpango mkakati wa utoaji wa huduma ya vyoo kwa watumiaji wa barabara.
Halafu suluhisho.

Tanzania tuitakayo. Hii hapa
 
Tanzania ina jumla ya kilomita 181602.2 za mtandao wa barabara, chini ya mgawanyo wa Kilomita 37225.5 barabara za kitaifa (barabara kuu na za kimkoa) na kilomita 144376.5 barabara za kiwilaya (barabara za mtoza, za kulisha na za vijijini). Mtandao huu unatengeneza 80-90% ya safari zote nnchini, yaani njia ya barabara ndio njia kuu ya usafiri na usafirishaji nnchini, (Bodi ya mfuko wa Barabara, Aprili 6 2024). Pamoja na mtandao huu mkubwa wa barabara zingatio la uwekaji wa vyoo kando ya barabara halipo.

Kwa mujibu wa ripoti za kitabibu binadamu ana uwezo wa kustahimili kukaa na haja kwa saa 4 mpaka 6, yaani kibofu cha mkojo cha binadamu kina uwezo wa kutunza takribani vikombe viwili vya mkojo ( 400-700 mililita ya mkojo). Ustahimilivu wa kibofu hiki inaathiriwa na umri wa mtu( mtoto, mtu mzima,mzee),jinsi, hali ya hewa( baridi/joto) na utimamu wa afya.Upande wa pili wa shilingi, binadamu anashauriwa kunywa kiasi cha kutosha cha maji kwa siku angalau vikombe 4 hadi 8( 1.5 Lita) kulingana na uzito/ urefu, shughuli zake za siku na mtindo wa maisha. Ukaaji na haja kwa muda mrefu una madhara makubwa katika mwili wa binadamu, baadhi ya madhara haya ni:

•Kutanuka kwa kibofu na ulegevu wa mishipa ya kibofu.
•Kuumiza figo, zoea la mara kwa mara la uzuiaji wa haja huweza kusababisha mawe katika kibofu.
•Maumivu ya mwili.
•Uzalishaji wa bakteria katika kibofu hivyo ugonjwa wa UTI, hii huwapata wale wenye historia ya ugonjwa.
•Kudhalilisha utu wa mtu kwa kushindwa kujizua zaidi.

Madhira hayo hapo juu huwapata watu wenye zoea la kuzuia haja. Kwa upande wa wasafiri na watumiaji wa barabara kundi la wazee, watoto, wagonjwa (wenye kisukari) wajawazito na watu wengine wamekua wakikumbwa na adha wakiwa barabarani mpaka kufika mwisho wa safari zao. Baadhi ya abiria na watu wemejenga zoea baya la kujizuia unywaji wa vimiminika wawapo safarini mfano maji na sharubati! Hii ni hatari zaidi kwa afya, kwani zoea hili huweza kupelekea tatizo la upungufu wa maji mwilini na hatimaye kufunga choo ama choo kigumu.

Kukwepa haya, taifa halina budi kuja na mpango mkakati wa utoaji wa huduma ya vyoo kwa watumiaji wa barabara. Mfano kwa safari za masafa marefu huduma hii hupatikana maeneo ya stendi ama katika migahawa/hoteli kando ya barabara, hii haitoshi kutimiliza mahitaji ya mwili. Mfano abiria atokaye Dar es salaam-Mwanza atapata huduma ya choo stendi au katika hoteli ama akilazimisha sana atajisaidia maporini kando ya barabara! ikichagizwa na semi maarufu ya "kuchimba dawa", hali hii si sahihi ki afya na kimazingira.​
Zoea la "kuchimba dawa" yaani kujisaidia kando ya barabara ni hatari kwa afya na usalama wa mazingira, hivyo hitajiko la usimikaji na ujenzi wa vyoo kando ya barabara kuingia.

Vyoo kando ya barabara vinaweza kuwa katika mfumo wa:
-Vyoo vya kudumu.
-Vyoo vya kuhamisha, hivi ni vyoo vya kukokotwa na gari na kuweka sehemu kwa muda maalumu.

Utolewaji wa huduma ya choo kwa watumiaji wa barabara utakua chini ya usimamizi wa mawakala wa barabara, halmashauri na wadau wengine wa maendeleo.

•Kwa barabara za Kitaifa( barabara kuu na za mkoa)
Wakala wa barabara nchini TANROADS- kwa kushirikiana na wadau wawe wahusika wakuu wa usimamizi na uendeshaji wa vyoo katika barabara hizi. Tenda zitolewe kwa wabia katika utoaji wa huduma kwa kusimamiwa na TANROADS.

•Barabara za kiwilaya(za mjini na vijijini na za kulisha)
TARURA kwa kushirikiana na halmashauri kupitia idara za maji safi na usafi wa mazingira wapewe jukumu la utoaji wa huduma hii.

Hawa watahusika na ujenzi wa vyoo na miundombinu yake, kuhudumia vyoo, kusimamia na kukarabati miundombinu yote ya vyoo katika maeneo yao. Vyoo kando ya barabara vizingatie makundi yote ya watumiaji wa barabara, vyoo vyenye miundombinu wezeshi kwa watu wenye mahitaji maalumu na wasio na mahitaji maalumu. Uwekaji wa vyoo kando ya barabara uzingatie mambo yafuatayo;

•Umbali kati ya choo toka kituo A hadi B, hesabu zipigwe na usanifu ufanywe kwa kuzingatia ushauri wa kitabibu yaani kwa muda XXY mtu anaweza kuzuia haja hivyo choo A kitaweka kilomita X na choo B baada ya kilomita Y kwa kuzingatia mwendo wa gari kwa saa.

•Makundi ya watumiaji wa barabara na mahitaji yao, kitabibu wazee, watoto na watu wenye kesi za upasuaji wa vibofu ama historia ya magonjwa ya kisukari na UTI wanahitaji huduma ya mara kwa mara utoaji taka mwili.

•Watu wenye mahitaji maalumu, miundombinu rafiki kwa kundi hili. Pawepo vyoo vya kawaida na vyoo vyenye miundombinu rafiki kwa kundi la wahitaji.

Changamoto zinazoweza kujitokeza na jinsi ya kukabiliana nazo.
•Gharama za uendeshaji na miundombinu.
-Bajeti zitengwe mahsusi na kuelekezwa katika huduma hizi. Fedha za miradi ya barabara zijumuishe gharama za ujenzi wa vyoo na miundombinu wezeshi.
-Kandarasi za ujenzi wa barabara ziwatake wajenzi kuzingatia uwekaji wa vyoo kwa kadri ya mahitaji.

•Ustaarabu na uharibifu wa miundombinu.
Zoea la "uchimbaji dawa"/kujisaidia kando ya barabara katikati ya safari linapaswa kukomeshwa kwa utoaji wa elimu kwa umma kwenye vituo vya mabasi na kwenye mabasi na kwa kutumia vyombo vya habari.​
Wanajamii wafundishwe uzalendo na kupenda mazingira yao sambamba na kulinda miundombinu ya vyoo.
Zoea la kujisaidia kando ya barabara ni la aibu na hatari kwa afya na ni uchafuzi wa mazingira hivyo halina budi kukomeshwa.

Uwepo wa vyoo kando ya barabara hizi (za kitaifa na kiwilaya) kutakuja na lukuki ikiwemo;
-Kuzuia magonjwa na kulinda afya ya wasafiri.
-kutunza mazingira
-Kufurahia safari kwa wasafiri, abiria katika safari hawatarazimika kujizuia kutumia vinywaji na kujibana kwa kuogopa adha, fedheha na aibu safarini.

Ni rai yangu kwa serikali kuja na mfumo wa utoaji wa huduma hii muhimu ili kulinda afya ya watumiaji wa barabara na mazingira. Hii ni karne ya jamii iliyostaarabika kujisaidia vichakani( uchimbaji dawa) hakuna nafasi. Shime kwa kandarasi wa barabara kuzingatia ujenzi wa miundo mbinu ya vyoo kando ya barabara kulinda afya na mazingira yetu.
The best way ni kuhakikisha kila kijiji along our roads kinakuwa na public wash rooms na zinakuwa managed na Bwana/Bibi afya wa eneo husika, na watumiaji tulipie huduma. Hiyo itakuwa rahisi kuhakikisha matumizi ya vichaka yanakuwa si lazima au yanafikia mwisho.
 
Naam! Vijiji pia vinaweza kushirikiahwa katika zoezi hili. Usafiri wa umma hauna budi kuboreshwa.
 
Back
Top Bottom