Uwekezaji si kitu kibaya ndugu!. Kama uwekezaji unafanywa na rate ni nzuri hakuna tatizo lolote kwani badala yake ni kuwafanya Tanesco wafanye hizo shughuli ambazo kila mtu anafahamu kuwa hawawezi na Tanesco yenyewe inawashinda. Wananchi hawawezi kuingia kwenye mipango ya kusaidiwa na goverment kila siku imefika wakati wa makampuni binafsi kusambaza umeme vijijini na mikoani na kuweka umeme wa uhakika kwa wawekezaji hasa wa viwanda. Wananchi sasa wanalipa zaidi kwani inabidi watu watumie majenereta, vibatari, biashara zinazotegemea umeme zimefungwa, gharama ya uendeshaji wa biashara umeongezeka, kuna biashara ambazo zimesimama mpaka swala la umeme lieleweke .n.k Kwani Tanzania tuna tofauti gani na nchi zingine kila siku tunalalamika umasikini lakini tumekuwa watu wa kupenda kila kitu kifanywe na serikali. Tatizo la umeme sio uwekezaji bali ni Tanesco na serikali!