Uboreshaji Afya ya msingi ni kuhakikisha kunakuwepo na mikakati endelevu wa kuhakikisha huduma za afya hususa ni kuzuia maambukizi mapya (Prevention)
Afya ya msingi inayoanzia katika jamii ni muhimu sana na hasa ndio msingi ambao unawagusa wananchi moja kwa moja hususa ni walioko maeneo ya vijijini na wale wasio na uelewa mkubwa juu ya maswala ya afya ambao ndio wengi zaidi.
Uwepo wa ugonjwa wa Covid 19 umedhihirisha na kuonyesha wazi ni jinsi gani nchi ilikua nyuma katika mikakati ya kuboresha afya ya msingi inayoanzia katika jamii, kama taifa tulipuuza kuwekeza zaidi katika afya ya msingi kitu ambacho ni hatari na kitafanya mapambano dhidi ya COVID 19 yawe magumu hadi kesho kutwa,
UDHAIFU WETU ULIKUA WAPI?
Wakati virusi vya covid 19, vikilipuka kwa mara ya kwanza mji wa Wuhan China, Baadhi ya Nchi zilianza kuchukua tahadhari kwa kuelimisha wananchi moja kwa moja kwa kutumia wahudumu wa Afya msingi, vyombo vya habari, serikali nk, wakati huo Tanzania ikiwa inatoa elimu kupitia Luninga na mitandao ya kijamii kitu ambacho kilifanya elimu hiyo isiwafikie wananchi ipasavyo na kwa uelewa mpana na hata wengine walioko vijijini hawakujua chochote kuhusu gonjwa hili, sababu huduma za Afya kwao si rafiki hawana waelimishaji wala hawana teknolojia,
Wakati tukisikia C0VID 19 imefika nchi za jirani, kwetu mapambano dhidi ya COVID hayakuchukuliwa kwa uzito mkubwa sababu elimu haikuwa ikiwafikia wananchi ipasavyo,
Jambo jema la kumshukuru Mungu ni kwamba kwa upande wetu species za kiafrica ugonjwa huu haukuwa na athari sana kama wenzetu wa ughaibuni bali umeonyesha effect sana kwa watu wa makundi maalumu wazee sana na wenye magonjwa sugu pengine ni kwasababu ya hali ya hewa na nature ya immunity ya muafrica,
Lakini tukiwaza vipi kama covid ingekuja kwa wembe uleule uliowapitia watu weupe? Tusifanye mizaha na magonjwa ya milipuko dunia haitaisha leo wala kesho je tumejiandaaje kukabiliana na majanga kama hayo yanapotokea?
Vipi kama ukiibuka ugonjwa mwingine mbaya zaidi kuliko covid? tutaendeleza mizaha? Je wananchi watafikiwa na elimu ipasavyo? Wahudumu wa afya msingi jamii wapo? kama taifa kuna mahali hatuko sawa.
Ukosefu wa wahudumu wa afya msingi
na utiliaji wa mkazo juu ya elimu ya kujikinga na kuzuia maambukizi umepelekea,
(i) watu kushindwa kujikinga dhidi ya maambukizi mapya
(ii) Kufanya mapuuza na mizaha
(ii) kuvaa barakoa zisizo sahihi/zisizosaidia chochote
(iiii)Kufuata matamko ya kisiasa yasiyo ya kitaaluma.
(iv) Taifa kukosa tamko la pamoja dhidi ya mapambano ya Covid
NINI KIFANYIKE?
Sasa basi, Serikali kupitia taasisi zake na wizara zake, ni wakati sahihi wa kuwekeza vilivyo na ipasavyo katika huduma ya Afya za msingi kwanzia kwenye shina ambako ndio kwenye jamii mpaka kufikia ngazi ya juu kabisa, taifa bila Afya hakuna maendeleo, hakuna furaha hakuna lolote la msingi, nguvu kazi zinapotea watu mashuhuri waliotegemewa wanapotea,
serikali izuie wanasiasa kuingilia tafiti na mikakati ya kitaalamu,
tujiandae kwa lolote, tuwe na utimamu kila wakati vipi kama covid ikienda mpaka wimbi la kumi? je, wimbi linalokuja tunajua linauzito na ukali kiasi gani? ni nini hasa tumeshafanya mpaka sasa, Tutaongeza mitungi ya oksijen ili tupokee wagonjwa wengi lakini vipi kwanini tusiwekeze katika elimu ya kuzuia maambukizi ili hiyo mitungi ya oksijen ikose wateja iwe mingi?
kwanini tusipunguze mizigo hospitali zetu kwa kuwaelimisha wananchi na wanavijiji ili wasizidi kisambaza maambukizi?
Corona imekua na effect ndogo kwa waafrica ukilinganisha na mabara mengine, je tumejifunza kulingana na makosa? vipi ukija ugonjwa mwingine ambao ni hatari zaidi nani atabaki?
Rai yangu kwa serikali fanyeni hima muwekeze katika afya ya msingi ya kuzuia maambukizi ikibidi muhakikishe hata kila zahanati au kila kijiji au kila kata, kunakuwa na dawati la elimu kwa jamii yaani ambalo linahusika na elimu ya afya kwa jamii, kufuatilia mienendo ya afya ndani ya jamii, kutoa elimu kwa jamii, na kuhakikisha kila mwananchi wa kata/kijiji/ eneo husika taarifa zake za kiafya zipo kwnye dawati hilo,
Dawati la elimu ya afya likiwepo kila kata litasaidia,
i) Wananchi kupata elimu kwa kina juu ya magonjwa mlipuko kwani watakua wakipewa elimu kwanzia majumbani kwao mpaka kwenye mikutano ya hadhara
ii) Taarifa za wagonjwa wenye magonjwa sugu kujulikana na kujua ni namna gani ya kuwakinga dhidi ya magonjwa mlipuko
iii) Ufuatiliaji wa karibu wa hali ya utekelezaji miongozo ya upunguzaji wa maambukizi mapya
iv) Utayari wa kukabili magonjwa mapya yanayoibuka kila siku
v) Upatikanaji sahihi wa takwimu za wagonjwa na hali zao nchini kote,,
Kwa kuzingatia hayo itapelekea kila mwananchi wa nchi hii awe na taarifa za afya na elimu juu ya magonjwa na kujikinga, hizi promosheni za kwenye TV na social network hazisaidii, ndio maana mpaka leo kuna watu hawajui ni vipi korona inaambukizwa unaweza ukastaajabu mtu anatoka kwake amevaa barakoa halafu akifika kwenye mkusanyiko wa watu anavua ili apige vizuri story, tujifunze bila mikakati madhubuti tutaendelea kukusanya wagonjwa na hospitali zetu zitalemewa.
Mwisho kabisa nawakumbusha watanzania wenzangu hususa ni vijana, tuendelee kuelimisha watu tujikinge na tuwakinge wazee wetu, tusiingie kwenye mikusanyiko bira barakoa, tumieni vitakaza mikono mnapogusana na watu wengi,
Tuondoe hofu na tufuate miongozo ya wizara ya afya na sio wanasiasa
Wasalaaam

Upvote
1