SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Katika karne za sasa sayansi na teknolojia zimeweza kutawala, vitu vingi vimeweza kurahisishwa kupitia sayansi na teknolojia tunaona katika nchi mbalimbali jinsi gani wanavyoweza kutumia na kunufaika na sayansi na teknolojia kupitia bunifu mbalimbali wanazoweza kuunda na kuleta manufaa kwao kwenye matumizi tofautitofauti, tunaona nchi kama Marekani hawa ni wanufaikaji wazuri katika sayansi na teknolojia wameweza kutengeneza mifumo ya utetezi na mawasiliano ya simu, pia nchi hiyo imeweza kuzalisha makampuni makubwa mbalimbali kama google, facebook, Apple, IBM, microsoft, na Intel katika makampuni hayo watu wengi wameweza pata ajira kutakana na ujuzi walionao kwa kupitia mataofa mbalimbali.
Nchi nyingine ni China imekuwa ni nchi tajwa sana kwenye masuala ya kiteknolojia imeweza kutumia vijana wa nchini mwake katika kufanya shughuli mbalimbali zinazotumia teknolojia katika viwanda vyao.
Katika nchi yetu tukiweza kuwekeza kuwekeza zaidi katika masuala ya teknolojia mfano teknolojia ya habari na mawasiliano, sayansi ya komputa au teknolojia ya vyombo vya anga na kivita katika vyuo vyetu tunaweza kumuandaa kijana kwa kumpatia mafunzo ya kutosha ambayo yatayoweza kumsaidia kupata ujuzi wa kufanya bunifu zitakazoleta manufaa katika jamii mfano; utengenezaji wa bidhaa za kielektoniki, bidhaa nyingi sana tumeweza kuagiza au kununua katika nchi zingine na sio ndani ya nchi yetu, tukiweza kutengeneza bidhaa viwanda vyetu binafsi vitakavyoweza kutengeneza bidhaa mbalimbali za kidijitali au kisasa zaidi hatutaweza kutegemea nchi nyingine sababu na sisi pia tunazalisha na tunao vijana wenye ujuzi wa kutosha ambao wanaoweza kuzalisha bidhaa hizo , katika nchi yetu kukiwa na uwekezaji katika teknolojia kutakuwa na makampuni ya utengenezaji simu, utengenezaji wa ndege magari, treni, pikipiki, vifaa mbalimbali vya kielektroniki, mapambo na urembo.
Hivyo serikali au kuweza kuanzisha shule na vyuo vya kipekee ambavyo vitavyoweza kufundisha masuala ya sayansi na teknolojia pekee ili kuweza kupata wataalamu waliobobea katika katika sekta hiyo ya sayansi nateknolojia na wakimaliza mafunzo waweze kuingia moja kwa moja kwenye viwanda husika na kufanya taaluma yao hivyo tutaweza kukuza pato la nchi na kutoka katika uchumi wa kati, uwekezaji katika sayansi na teknolojia hii inaweza kusaidia ajira kwa watu wengi nchini katika sekta mbalimbali na kuweza kujipatia kipato vilevile kuinua kiuchumi.
Duniani kuna teknolojia nyingi sana ambazo zinaweza kupelekea ukuaji wa kiuchumi, kisiasa au kilimo, katika kilimo hapa nchini kwetu kukiwa na wanasayansi na wataalamu bora watakao weza kufanya utafiti katika uparikanaji wa mbegu bora zitakazoweza kuleta kilimo chenye tija, mazao mengi na mbolea bora itayoweza kukuza mazao kwa haraka.
Pia katika vyuo na shule kuwe na utaratibu wakuibua vipaji kwa wanafunzi kwa kugawa tuzo kwa wabunifu mbalimbali wa masuala ya sayansi na teknolojia ili kuweza kuwapa motisha ya kuwaendeleza katika taaluma au vipaji vyao.
Hapa Tanzania kuna wataalamu wengi wa kisayansi nateknolojia ila hawana watu wa kuwashika mkono ili kuweza kuwaendeleza kuwaendeleza katika masuala ya bunifu zao za sayansi na teknolojia, pindi tutakapo weza kuwekeza katika masuala ya sayansi na teknolojia tutaweza kujitegemea katika vitu vingi na uchumi pia utaweza kukua, sayansi nateknolojia ni vitu vikubwa sana kwani tunaliweza kujitengenezea vifaa vyetu wenyewe vya kivita mfano mabomu ya nyukria, makombora, risasi, bunduki au vifaru.
Katika nchi za wenzetu kama ujerumani wao wameweza kuwekeza katika kutengeneza vifaru na silaha nzito za maangamizi zitumikazo karika vita, hii imewapelekea kuwa na uchumi mkubwa katika nchi yao, mataifa mengi ya kimagharibi yameweza kuwa na uwekezaji mkubwa katika nchi zao kupitia sayansi na teknolojia mfano kama marekani kuna makampuni mengi yanayohusisha teknolojia mbalimbali zikiwemo za kibiashara, mitandao ya kijamii,
Uundaji wa vifaa vya kielektroniki na uundaji wa vifaa vya kimatibabu, tukiweza kuwa na kampuni angalau inayohusiana na teknolojia ya utengenezaji vitu au bidhaa mbalimbali kwa kuwatumia wataalamu wa ndani ya nchi pamija na nje ya nchi tutaweza kuendelea sana kiuchumi katika taifa hili, na kitu kikubwa kinachopaswa ni elimu, ujuzi na uwekezaji ili kuweza kufanikisha lengo hili, ila kwa hapa nchini kwetu kuna klabu mbalimbali zilizoundwa na watu binafsi zinazohusisha maswala ya sayansi na teknolojia mfano wake ni Apps and girls hii ni klabu iliyoundwa ili kumsaidia mtoto wa kike kujitambua, kupata ujuzi wa teknolojia ya tehama, ujasiliamali, uongozi na kutimiza ndoto zake, nyingine ni Tanzania data lab maarufu kama dlab hii inahusiana na uhamasishaji kwa wanawake na wasichana katika teknolojia na kufanya tafiti mbalimbali zitakazoweza kuwasaidia wataalamu katika masuala ya teknolojia.
Teknolojia iliyopo sasa nchini kwetu haitoshelezi katika sekta mbalimbali kama ajira, kilimo, siasa na uchumi inahitajika uwekezaji mkubwa ili sayansi na teknolojia iweze kukua mfano hapa Tanzania kumetokea na wabunifu kama Masoud Ally Kipanya maarufu kama (Kp) ambaye kaweza kubuni gari lake linaloweza kutumia umeme, ilihali angeweza kupata sapoti kutoka kwa serikali, kampuni au watu binafsi tungeliweza kusonga mbali katika teknolojia hiyo, pua katika vyuo vyetu kuna kuna baadhi ya wanafunzi wameliweza kubuni vitu mbalimbali ambavyo vinamanufaa katika jamii.
Tukiweza kuthamini vipaji vyetu basi tutaweza kufanikiwa pia kiuchumi, Watanzania wengi wanadhani vitu vinavyotengenezwa ndani ya Tanzania basi vitu hivyo havidumu na wanaamini vitu vinavyotoka katika nchi zenye uchumi mkubwa ndio bora sana, ingali vyetu pia vina ubora pia vikiweza kuthaminiwa na kupewa kipaumbele kama wanavyoweza kuvipa hivyo vingine, na katika sayansi pia tunatakiwa tuwekeze wanasayansi kutokea nchini kwetu, kwani huleta mwitikio mkubwa kwa vijana kuitafuta elimu na kuweza kuzifikia ndoto zao kwani tunao madaktari, wanakemia, na watafiti mbalimbali wanaohusiana na mambo kadha wa kadha ya kisayansi .
Hivyo ningependa kiomba serikali na watu wote wa nchi hii tuweze kupenda vya kwetu na tuwekeze katika sayansi na teknolojia kwani ukuza uchumi wa nchi na huleta ajira kwa watu tofautitofauti hususani kwa vijana.

Upvote
1