SoC03 Uwekezaji katika Sekta ya Habari

SoC03 Uwekezaji katika Sekta ya Habari

Stories of Change - 2023 Competition

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA HABARI.

Tupo katika karne ya 21 ambapo tumeshuhudia ulimwengu ukipiga hatua kubwa katika upande wa teknolojia ambayo imefanya ulimwengu kuwa kama kijiji. Teknolojia imerahisisha upashanaji habari kwa haraka na kufikia idadi kubwa ya watu wa kila pembe duniani.

1C-768x536-1.jpg


Kupitia vyombo vya habari kama vile televisheni, radio, magazeti na mitandao ya kijamii imefanya tasnia ya Habari kuwa na nguvu ya ushawishi ulimwenguni kwa maana taarifa inaweza kujenga uwezo wa watu katika kufikiri na kufanya maamuzi sahihi na wakati huohuo inaweza kubomoa fikra na kusababisha maafa makubwa katika jamii.

56914032_605.jpg


Waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutoa taarifa kwa umma, kuelimisha, kuburudisha na kuibua hoja nzito zenye kuonyesha udhaifu kwenye baadhi ya maeneo nchini kwa kupeleka taarifa za kinachojiri kwa watunga sera ili kuweza kufanyiwa kazi na kuchukuliwa hatua stahiki katika maeneo husika kwa malengo mazuri ya kupunguza au kuondoa kero.

MIFANO HALISI NI..

Uchakavu wa miundombinu kama madarasa, barabara, na majengo ya vituo vya afya.

FsiiaNDWwAAh7wT.jpg


baada ya taarifa za uchakavu wa madarasa kuripotiwa katika vyombo vya habari na picha za madarasa hayo kusambaa katika mitandao ya kijamii tumeona serikali ikichukua hatua ya kujenga madarasa na kuyakarabati. Ni wazi kuwa taarifa hizi sizingeripotiwa popote ingechukua muda mrefu kwa serikali kufanya maamuzi ya kujenga madarasa mapya na kuyakarabati yale chakavu.


61aca545cbc22021199172.jpg


Matukio ya ubakaji, ulawiti na ukatili dhidi ya watoto na wanawake. tumeshuhudia hivi karibuni pamekuwepo ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wa jinsia zote wa kike na kiume pamoja na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwa maana ya mauaji na kujiua kwa baadhi ya watu na kubwa zaidi ni wanandoa kuuana kwa kile kinachosemwa ni wivu uliopitiliza wa mapenzi.

kiukweli tuwape pongezi waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele kuripoti haya matukio na kutoa mawazo yao ya jinsi gani tunaweza kukabiliana na matukio ya mfanano huo kazi imebaki kwetu wananchi na serikali kuhakikisha tunasahihisha pale tulipokosea na kuweka nia ya dhati yenye dhima ya kutokomeza matukio yote ya ukatili
IMG-20220606-WA0032-1024x767.jpg


waandishi wa habari kupitia sekta ya habari wamekuwa kiungo muhimu kati ya serikali yaani (ikulu, bunge, na mahakama) kwenda kwa wananchi kwani licha ya kutuhabarisha yanayoendelea nchini wamekuwa na jukumu la kutuunganisha na serikali kwa kupeleka kero zetu sehemu husika na kutupa mrejesho juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali.

Je tumewekeza ipasavyo katika sekta ya habari ili kuhakikisha tunajenga taifa imara?

kwa umuhimu wa sekta ya habari ni wazi kuwa ni miongoni mwa sekta nyeti sana zinazohitaji kuwa na uwekezaji mkubwa na ulio imara katika kila sehemu inayohusiana na sekta hiyo kama vile rasilimali pesa kwa maana ya mitaji, vifaa, usafiri na pia rasiliamali watu wenye elimu na uweledi kutoka vyuo vyenye ubora vinavyotoa stashahada na shahada ya uandishi wa habari.

DSJ.png


Ni vyema upatikanaji wa waandishi wa habari uwe na msingi ulio thabiti wenye kutengeneza waandishi wa habari wenye uelewa mpana wa jinsi ulimwengu unavyoenda wenye uwezo wa kufikiri kimantiki zaidi na uwezo wa kuibua hoja zenye maslahi mapana kwa taifa letu.

Kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuna vituo vya radio 183 na Televisheni 45 vilivyosajiliwa kutoa huduma Tanzania katika ngazi ya Taifa na kanda. Pia kuna magazeti, majarida, foramu, blogu na Televisheni za mitandaoni kimsingi katika idadi tupo vizuri.

5-34-scaled.jpg


Swali la msingi ni je wingi wa vyombo vya habari unaenda sambamba na ubora wa maudhui unaohitajika kwa umma wa Tanzania?

Vipi kuhusu utendaji na watendaji wa vyombo vya habari pamoja na wadau wake.? je kuna uweledi na vipi sheria na kanuni zinazosimama vyombo vya habari zinaendana na kasi ya ukuaji wa vyombo vya habari.?

Mimi kama kijana wa Tanzania mwenye matamanio ya kuona nchi yangu ikipiga hatua ya maendeleo napendekeza tuongeze nguvu ya uwekezaji katika sekta ya habari kupata taarifa na maudhui sahihi yenye malengo ya kujenga viongozi na wananchi.

Na hilo litawezekana kwa kufanya yafuatayo.

1. Kuwaandaa waandishi wa habari kulihudumia taifa na sio kutetea maslahi ya watu wachache au maslahi yao binafsi

2. Uboreshaji wa maslahi na mazingira ya kazi ya waandishi wa habari kwa kuwawezesha kufika kila kona Tanzania kutafuta habari na pia kuwakatia bima za afya wapatapo changamoto za kiafya wao na familia zao.

bima.jpeg


3. Utungaji wa sheria na kanuni zinazowalinda waandishi wa habari wanapotimiza majukumu yao kusiwepo vitisho dhidi yao vitakavyowafanya kushindwa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi

4. Taasisi za serikali na binafsi ziwajibike kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari. watumishi wa serikali wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari wanapohitajika kutolea ufafanuzi baadhi ya masuala katika maeneo yao ya kazi

5. Kuhakikisha kuna usawa wa habari zitolewazo kati ya mijini na vijijini. waandishi wengi wamejikita mijini na kusahau kuwa kuna matukio mengi ambayo yanajiri sehemu za vijijini ambayo yanastahili kuonekana katika vyombo vyetu vya habari

6. Kufadhili taarifa za kichunguzi na kitaalamu.

7. Kupunguza gharama za vifaa vya teknolojia kama vifaa vya studio, simu, televisheni pamoja na gharama za vifurushi ili kumtengenezea mwananchi mazingira rafiki na nafuu ya kupata habari.

8. Mamlaka ziendelee kupewa rasilimali watu na pesa ili kudhibiti taarifa za upotoshaji na wapotoshaji.

Sekta ya Habari ni sekta yenye nguvu ya kujenga au kubomoa. kama Taifa ni jukumu letu kuitumia sekta ya habari kwa maendeleo ya taifa letu.​


Picha kwa hisani ya mtandao.
 
Upvote 4
Mtu ujengwa kutokana na vitu anavyoona na kusikia mara kwa mara sekta yetu ya habari ina jukumu zito la kutujenga sisi WaTanzania.
 
Wakuu wa Jamiiforum bado mnakaribishwa kusoma, kuchangia na kupigia kura andiko langu lilojikita katika kuelezea umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya Habari
 
Back
Top Bottom