SoC04 Uwekezaji katika tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

DANIEL W LAIZER

New Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
1
Reaction score
2
UTANGULIZI
Miaka 15 iliyopita tulikumbana na wimbi kubwa la kushuka kwa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza hapa nchini Tanzania,sababu kubwa hasa ilikuwa Ni mabadiliko ya kiteknolojia ya namna ya uwasilishaji wa filamu na michezo ya kuigiza kwa jamii na hivyo kunifanya kupoteza mwelekeona hasa kushuka kwa soko la filamu na michezo ya kuigiza (2009).Lakini mbali na changamoto hiyo ambayo ilijitokeza wasanii mbalimbali pamoja na serikali yetu ya Tanzania ilipambana kuhakikisha ina leta uu tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza kama ilivyo hitajika na ndio ivyooo hadi leo hii.

Kwa asilimia 61.3 au pungufu,Kama wasemavyo wataalamu wa utafiti juu ya tansia ya filamu nchini Tanzania tangu 2009 hadi 2021 tansia ya filamu na michezo ya kuigiza bado ipo nyuma Sana,ni Kama serikali yetu imeipa mgongo kidogo na kugeukia michezo wa mpira ambao hauitaji Sana teknolojia .Baraza la filamu na michezo ya kuigiza nchini Tanzania(1984) inapambana katika uwekezaji na kila nyenzo paka pale walipoleta Tango TV kwa kusaidia kusambaza filamu na michezo ya kuigiza na,lakini bado pamoja na jitihada hizo kufanyika na nyingine zikiendea kufanyika kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza ipo nyuma Sana ukilinganisha na nchi kama Nigeria na South Africa ambazo kwa upande mwingine wapo vizuri hata kwa swala la kimichezo yaani michezo wa mpira na sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza ukilinganisha na Tanzania.

Swali zuri la kujiuliza na kujijibu wenyewe sisi,Kama WATANZANIA ni kwanini SIO sisi Tanzania tukawa tunaongoza vizuri katika AFRIKA au kimataifa katika tasnia mzima ya filamu na michezo ya kuigiza kwasababu tumejaliwa rasilimali nyingi,watu wabunifu na vitu vingi tunavyo lakini kwanini SIO sisi Tanzania?


Majibu ya hilo SWALI kuyajibu kwa kukuuliza Tena maswali haya MAKUU MATANO,Kama ifuatavyo;
(a).Je! ni Kweli nchi zinazoendelea vizuri AFRIKA katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza zinasukumwa kimaendeleo na teknolojia kubwa ya nchi hiyo?
(b).Je! Tanzania tuna ukosefu wawatu mahiri katika utayarishaji na uundaji wa filamu na michezo ya kuigiza?
(c).Je!ni kweli nchini Tanzania tuna ukosefu wa Soko la kunadi na Kuuza filamu na michezo ya kuigiza?
(d).Swali lingine ni kwanini filamu na michezo ya kuigiza nyingi nchini Tanzania zimetawaliwa na utamaduni wa lugha ya kiswahili (Swahilihood)?.Je ! ni kwel HAKUNA lugha nyingine tunahifahamu ya kutushindanisha katika Soko la kimataifa? Na mwisho ni!
(e). Serikali ya TANZANIA inakwama wapi Katika kuhakikisha hili CHUNGU la tansia ya filamu na michezo ya kuigiza inashika matawi kimataifa?

CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA TASNIA YA FILAMU NCHINI.
Upungufu mkubwa wa teknolojia katika tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza.Tanzania inachukuliwa Kama nchi ya tatu katika "DIGITAL OPERATION"lakini bado tupo nyuma katika teknolojia ukilinganisha na nchi Kama South Africa ambayo wamepiga hatua kubwa zaidi kwenye teknolojia hasa katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza ambayo inashawishi wait kutumia mazingira na rasilimali walizonazo kuitendea haki swala la filamu na michezo ya kuigiza

Miaka 5-25 ijayo.
Ni lazima Sasa Tanzania ijifunze kwamba teknolojia Ni ya muhimu Sana Katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza ,Ni lazima TANZANIA yetu iwekeze nguvu kubwa katika kuivuta teknolojia kwenye tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza kwa kufanya zaidi kitu KINACHO itwa "TRANFER OF TECHNOLOGY"kutoka kwa nchini zile ambazo wapo mbele zaidi kimaendeleo katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza, na sio kushinikiza teknolojia katika ofisi za serikali tu au vyanzo vya ukusanyaji mapato,huku ikisahau kuwa pia tuna uhaba wa teknolojia katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza . Hivyo natarajia na kuamini kwasababu inawezekana miaka 5 au 25 ijayo serikali itasaidia zaidi kuleta teknolojia katika tasnia ya filamu ambayo itasaidia hichi chungu Cha sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza kushika matawi kimataifa, huku tukiendelea kujifunza kwa nchi zinazoendelea kwenye sanaa ya filamu kwa kutumia teknolojia inayotumika.

Uhaba wa watu mahiri Katika utayarishaji na undaji wa filamu na michezo ya kuigiza. Tuna upungufu wa Wataalamu mahiri Katika utayarishaji na undaji wa filamu na michezo ya kuigiza, hasa katika ubunifu,lugha tunayotumia (Swahili au Kingereza),Katika matumizi ya vifaa vya kiteknolojia vya sanaa ya filamu, Katika uteuzi wa mazingira au uundaji wa mazingira,na hata pia swala la mavazi ya wasanii kipindi Cha utayarishaji wa tansia nzima ya filamu na michezo ya kuigiza.Hii ni changamoto ya upungufu wa wataalamu hasa katika lugha naona ndio inayoturudisha nyuma zaidi katika tasnia ya filamu nchini kwasababu watu wengi iwe ndani au kimataifa utazama zaidi lugha ili kupata ujumbe ambao aliutarajia kupokea,pia swala la mazingira filamu na michezo ya kuigiza nyingi za hapa nchini zinaegemea sana zaidimanyumbani,mahotelini,vijijini na kupelekea mazoea kwa watazamaji na hivyo kupoteza ile hulka ya watu kufatilia nini hasa kinaendea ndani ya tansia ya filamu na michezo ya kuigiza.


Miaka 5-25 ijayo.
Nchini Tanzania takribani 10,000 na zaidi kila mwaka wanapatikana wahitimu hasa waliosemea tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza!Je huwa wanaenda wapi baada ya kumaliza masomo hayo ya tansia ya filamu?au nini huwa wanafanya ili kuhakikisha sanaa waliosomea inawapa faidi wao wenyewe na kwa taifa kunufaika?hii ni kazi ya serikali na wasimamizi lengwa katika tasnia hii, kwamba ni lazima wakaanda na kutengeneza shirika litakalo simamia hawa vijana wenye ujuzi na ubunifu katika Lugha hasa (Kingereza na kiswahili), katika utumizi wa vifaa vya kiteknolojia ya filamu na michezo ya kuigiza pia na wenye ubunifu wa kuunda mazingira halisi na yasio halisi ili kufungua chungu hichi cha sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza kimataifa zaidi kwa miaka 5 au 25 ijayo na sio kutegemea mtu mmoja katika kuimarisha tansia ya filamu na michezo ya kuigiza. Hivyo basi, serikali uchukue hatua mapema kufungua Vyuo cha taaluma ya sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza tena za kisasa ambazo zitashawishi hata mataifa mengine kuingia katika tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza hapa nchini Tanzania.

Changamoto ya Lugha (Swahilihood).Hii tatizo kubwa inayoikumba nchi ya Tanzania Katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza,kwa Sasa umekuwa ni kama utamaduni kila kazi ya kisanaa nchini lazima iwe Katika lugha ya kiswahili wakati hakuna sheria yoyote nchini ya ulazima filamu zote na michezo ya kuigiza kutumia kwa lugha ya kiswahili au je! ni kweli Tanzania lugha inayojulikana zaidi ni kiswahili tu? hii inatupa mtazamo kwamba sisi wenyewe hatuhitaji kujulikana kimataifa kupitia tansia ya filamu na michezo ya kuigiza, kwani nchini nyingi zinazo zinazoendelea kushika matawi kimataifa katika tasnia ya filamu hutumia zaidi lugha ya kibiashara yaani lagha ya "KINGEREZA" hili nalo ni la kujifunza kwa nchi Kama Tanzania.

Miaka 5-25 ijayo.
Wataalamu wa sanaa ya filamu nchini Tanzania wanasema "Tanzania Ni muda Sasa wa kufungua hichi chungu Cha Sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza kimataifa" Ni lazima tupunguze utamaduni wa lugha yetu kutumika katika kila tansia ya filamu Kama wanavyofanya nchini zingine za AFRIKA ,Kama Kenya na Nigeria ambapo kwenye tansia zao za filamu na michezo ya kuigiza upenda Sana kutumia Kingereza kikiwa kimechanganywa na kiswahili kidogo na kunifanya tansia hizo kupata soko kimataifa ,pia mfano mzuri wa nchi ya India ambayo kwa Sasa Tanzania inaingia katika uwekezaji wa filamu na michezo ya kuigiza hapa nchini,nchin India kuna zaidi ya Lugha 20, lakini pia nawao utumia Kingereza Kama lugha ya biashara kimataifa Katika tansia ya filamu.Hivyo basi, ni shauri taasisi na wasimamizi wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini Tanzania, kwamba ili miaka 5 au 25 ijayo tuwe tumepiga hatua katika tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza ni lazima kuangalia upande wa matumizi ya Lugha ,sina maana ya kuhikosoa lugha yetu adhimu na tamu ya kiswahili hapana, naamini filamu ambazo zitajikita kwenye hii lugha ya biashara yaani KINGEREZA haiwezi kuharibu maana ya sisi ni taifa gani! au nini maudhui na ujumbe wa filamu hizo!,bali ndio kipaombele na mwanzo wa kufungua hichi chungu ambacho kilifikikwa kwa muda mrefu,kwa mafanikio katika soko la filamu nchini na kimataifa ,hasa kwenye tansia ya filamu na michezo ya kuigiza.
Uhaba wa uwekezaji Katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza. Soko la filamu na michezo ya kuigiza nchini Tanzania linakosa wawekezaji ,na wawekezaji wengi wamekimbilia katika michezo wa mpira ,pia nayo serikali inashindwa kuwavuta wawekizaji watakao badilisha tansia ya filamu nchini na michezo ya kuigiza ili kushika matawi kimataifa ,sababu kubwa ya kukosa wawekezaji wakubwa ni kutokana na mienendo mbovu na wawekezaji kupoteza imani Kama tansia hii ya filamu inaweza kuwalipa ,sio ivyo tu pia changamoto ya kiteknolojia na kukosekana kwa ubora wa filamu zenyewe za hapa nchini zinachangia katika kukosekana kwa wawekezaji wakubwa nchini Tanzania na kupelekea tansia ya filamu na michezo ya kuigiza kutegemea zaidi mtandao wa YOUTUBE ili kusambaza na kutengeneza nafasi mbalimbali kwa nchi za jirani, vyote Ivyooo upelekea sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza kukosa wawekezaji wa kudumu na kupoteza soko kimataifa.

Miaka 5 au 25 ijayo.
Ili Tanzania kuwavutia wawekezaji wakubwa hasa Katika tansia ya filamu na michezo ya kuigiza ni lazima kwanza, serikali kufanikisha swala zima la kiteknolojia hapa nchini ambayo itawashawishi wawekezaji wakubwa kuwekeza katika tansia hii ya filamu na michezo ya kuigiza,pia ni lazima Tanzania kutengeneza makampuni makubwa ambayo yanapatika hapa nchini, Kama ya wenzetu wamarekani wanakampuni kubwa kama NETFLIX,na SONY PICTURES na nyingine nyingi ambazo zinawasaidia Sana katika kutayarisha na kusambaza filamu zao kimataifa.Hivyo basi, miaka 5 au 25 ijayo tunatarajia na tunaamini kwasababu inawezekana kabisa, kuona mabadiliko makubwa , hasa muhimu zaidi ni uwepo wa makampuni ya kisasa zaidi ndani ya nchi na uwepo wa kiteknolojia katika sanaa ya filamu, ambayo kwa namna moja au nyingine itasaidia Sana katika kupunguza tatizo la ajira na kusaidia kusambaza filamu,hata kutuwezesha kukuza soko la mauzo ya filamu na michezo ya kuigiza kimataifa na sio kutegemea tu mitandao ya watu binafsi tena wa kutoka nje ya nchi ili kusambaza tansia ya filamu na michezo ya kuigiza.

MAPENDEKEZO YA ZAIDI
(a).Ni jambo la muhimu Sana serikali yetu ya Tanzania pamoja na jeshi lake la Tanzania likaangalia ni namna gani wanaweza kuitambulisha zaidi nchi yetu, kwa kutumia tansia ya filamu na michezo ya kuigiza kwa kuanda historia yetu ya Tanzania kwanzia enzi ya ukoloni paka tulivyo pata uhuru na hadi sasa na sio kubaki tukizisoma kwenye vitabu au kusikiliza hadithi,hii itasaidia nayo tansia ya filamu na michezo ya kuigiza kufikia matawi mbalimbali ya kimataifa huku watu wengi wakizidi kujifunza kuhusu nchi yetu pendwa ya Tanzania. Pia wasanii mbalimbali wapate vibali vya kuonesha tansia ya filamu na michezo ya kuigiza ndani ya jeshi letu la Tanzania ili nako kimataifa tukizidi kuitambulisha nchi yetu.
(b). Hivyo basi ni muhimu zaidi Tanzania kuweka jitihada kwenye kujifunza nini cha kufanya kwenye tansia ya filamu na michezo ya kuigiza kutoka kwenye nchi zilizo endelea kwenye tansia hii ya filamu na kuvitendea kazi kiukamilifu.

TWENDENI TUKATIMIZE NIA SISI KAMA WATANZANIA KATIKA TASNIA YA FILAMU NCHINI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Upvote 3
Asante Kwa ujumbe wako mzuri. Filamu nzuri sio lazima utumie kingereza ili uiuze kimataifa ndio maana Mkorea, mhindi na mchina kafanikiwa kuuza kimataifa tena Kwa lugha yake. Mfano wa ziada Nigeria wanatumia lugha za asili na movie ziko Netflix itazame "Snikulapo" na nyingine. Tanzania tunao waongozaji mahiri wanao uza kimataifa kama Amir Shivaji, Tom Johnson, John Kolo, Idris Sultan na wengine wengi lugha kwenye movie zao ni kiswahili na lugha za kubuni tu kama ilivyo kwenye"Wandongwa". Filamu yenyewe ni lugha kupitia matendo kabla watu hawajaongea mazingira, vitendo na mijongeo ya kamera inaongea unaangalia kitu gani, mfano Avatar ya Cameroon Ina lugha ambayo ilitungwa tu na part two kaweka mpaka lugha ya alama bado filamu inaeleweka. Muhimu kujua Filamu inahitaji uwekezaji na waandaaji wengi wa Filamu Tanzania hawana Hela mbaya zaidi hawajui namna ya kuomba Hela kwenye makampuni kama Netflix nk . Mwisho niseme Shida sio lugha, shida ni utaalamu na mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…