SoC02 Uwekezaji katika Vipaji

SoC02 Uwekezaji katika Vipaji

Stories of Change - 2022 Competition

doreenfrankmkinga

New Member
Joined
Jul 31, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Watu wengi katika nchi yetu wanaishi maisha ya kawaida sana na ya kujutia sana huku wengi wao hawafurahii shughuli na kazi wanazozifanya. Lakini katikati ya watu wote hao kuna wengine bado huzunguka sana na bahasha zao wakiwa na elimu za juu kabisa bila mafanikio yoyote, na hata wakipata nafasi huwa hawafanyi vizuri sana kama inavyotakiwa.. Je ni kwanini imekuwa hivi?. Jibu ni kuwa watu wengi wamewekeza katika uwezo wa watu wengine na sio uwezo wao.

Kila mtu ana uwezo wake na kila mtu anakipaji chake na uwezo wa kufanya kitu fulani, lakini imetokea wimbi kubwa kuwa malezi tunayolelewa na Wazazi wetu au walezi na mfumo wa elimu Vyote hivi vimedidimiza Sana uwezo na VIPAJI walivyonavyo watu wengi.

Kwenye upande wa malezi Wazazi wengi sana wamefanya wamefanya watoto wao watembee katika ndoto za Wazazi kuliko ndoto za watoto wenyewe.

Mfano mtoto Ana kipaji cha kucheza mpira lakini mzazi anataka mtoto awe daktari, mzazi atataka mtoto aishi kwenye ndoto za udaktari lakini akishamaliza ndipo aanze ndoto za mpira kitu ambacho sio sahihi.

Hivi je mtoto uyo anaweza kufanya kazi yake kwa ueledi kama inavyotakiwa?!. Tunasahau kua ili kipaji cha mtu kikue lazima kifanyiwe mazoezi na nguvu kila Mara kwahiyo mpaka akisoma amalize bila kupewa nguzu hupoteza makali kwa asilimia kubwa Sana.

Hivyo basi Wazazi inabidi wawekeze Sana katika uwezo wa watoto wao na VIPAJI walivyonavyo kulizo kuwekeza katika vitu wanavohotaji wao maana katika UWEKEZAJI unaongea thamani na kuimarisha makali ya kipaji hiko ndipo tutazaa wafanyakazi bora wenye kupenda kazi zao na na wenye ueledi mkubwa Sana na hapo ndipo mwanzo wa maendeleo maana kila mtu anafanya kazi kwa ufasaha mkubwa.

Katika mfumo wetu wa elimu, umeegemia Sana kujua uwezo wa mtoto katika nyanja mbili ambao ni kuandika na kusoma, kwahiyo mtoto aliye na uwezo wa kuongea au mwenye uwezo wa kucheza mpiraa anaonekana ni mjinga na hapendi shule. Kitu ambacho huua na huficha uwezo wa watoto wengi Sana.

Je, tufanye nini ili tuweze kuwekeza katika uwezo alionao mtoto?!

1. Serikali haswa Wizara ya Elimu inabdi kurekebisha mfumo wa elimu kwa kupanua wigo na kumpa nafasi hata yule ambaye uwezo wake haupo kwenye kuandika na kusoma awe huru kutoa kile alichonacho ili kikuzwe na kuwekeza humo.

2. Darasa la saikolojia litolewe mashuleni ili watoto wasijione wajinga pale ambapo wanashindwa kufanya vema, inabdi agundue kua Ana uwezo mkubwa wa kufanya makubwa Kwa kutumia kipaji chake.

3. Walimu wasipende kudidimiza ule uwezo alionao mtoto kwasababu anafeli katika kusoma na kuandika, Bali wawe nao karibu na kuwajua ili kuwatia moyo kuwaendeleza mbele zaidi.

4. Wazazi inabidi waishi na watoto katika ndoto za watoto walizozibeba sio walizobeba wao maana tuanwapa majukumu kutimiza kile alchokibeba mzazi moyoni na wala sio alchokibeba mtoto moyoni.

Tukifanya hivi kwa kizazi cha sasa basi tujiandae kutoa jamii bora kabisa Yenye kufanya kazi kwa ueledi wote na kuipeenda nchi kwa ujumla na uchumi unaendelea kujua siku hadi siku.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom