Old Member (Retired)
JF-Expert Member
- Sep 29, 2012
- 3,401
- 1,610
UTT hawauzi hisa ila wanauza vipande (units). Muundo uko hivi: unanunua vipande vya mfuko mmojawapo wa UTT (Jikimu, Liquid, n.k.) kwa bei ambayo itakuwepo kwenye soko siku unanunua. UTT itachang'anya hiyo pesa yako pamoja na za wawekezaji wenzako na kutafuta fursa nzuri za kuziwekeza. Itaziwekeza kwenye hisa za makampuni (Company Shares), Amana za Serikali (Government Bonds/Treasury Bills), Amana za makampuni (Corporate Bonds) na fursa zingine zenye hatarisho (risk) ndogo. Kila UTT inapopata faida kutokana na uwekezaji huo na thamani ya kila kipande cha aliyewekeza kwenye mfuko inaongezeka. Kwa mfano, kama wakati unanunua bei ya kila kipande ilikuwa Sh. 200 baada ya muda ukitaka kuuza bei ya kipande inaweza kuwa Sh. 250, ikiwa na maana utapata faida ya Sh. 50 kwa kila kipande. Hivyo ukubwa wa faida utakayopata utategemea vile vile ulinunua vipande vingapi. Ununuzi na uuzaji wa vipande ni rahisi kwa sababu hautegemei kuwepo mteja wa kununua kutoka kwako bali ni UTT/Mfuko wenyewe ndiyo unauza na kununua hivyo vipande.