Uwekezaji kwenye AI “ the new bitcoin”

Uwekezaji kwenye AI “ the new bitcoin”

kinshwi

Member
Joined
Aug 22, 2016
Posts
22
Reaction score
39
Mwaka 2009 wakati bitcoin inaanzishwa ilikuwa na thamani ya usd 0.4 ambayo ilikuwa ni kama tsh. 520 tu kwa wakati huo, ilipanda thamani taratibu na hivi sasa miaka 16 baadae thamani ya bitcoin moja ni Karibia Milioni 236 za kitanzania. Aliyewekeza Tsh. 520 mwaka 2009 au Tsh. 22,000 mwaka 2012 leo angekuwa anamiliki M 236. Lakini ni wachache sana waliojua au hata kudhubutu kufanya hivyo, hata wataalamu wabobevu wa mambo ya IT, uchumi na uwekezaji hii fursa iliwapita, hawakuijua.
ni mtazamo wangu kwamba Artificial intelligence ni bitcoin mpya itakayopanda thamani sana kwa hii miaka inayokuja. Kila sekta kuanzia afya, banking, IT, engineering , usafirishaji etc itategemea sana akili mnemba katika utendaji kazi, naamini ni fursa nzuri kuwekeza kwenye makampuni na startups zinazojishughulisha na Artificial intelligence. Naamini pia wapo watanzania wenzetu wenye elimu na uzoefu wa kutosha wa namna ya kufanya uwekezaji huu , kwasasa sijafanikiwa kuona makampuni local yanayojihusisha na AI .Kwa wale wenye ujuzi karibuni mtufunze ili hii generational opportunity isitupite tena kama tulivyopitwa na bitcoin .
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom