Uwekezaji mkubwa kwenye kilimo ndio njia pekee ya kuwezesha Shillingi kuwa stable na Utalii pia

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Kama mnavyojua nchi zetu masikini vitu vingi tunaagiza nje, ukiangalia pesa tunazowapa Dubai, China, Japan etc kwa ajili ya kununua bidhaa zao ni nyingi sana kuanzia magari, electronics na kadhalika.

Njia pekee ya kuwezesha shillingi yetu kuwa stable ni kuwekeza sana kwenye kilimo ili tuweze kuuza nje. Kamwe kwa viwanda vyetu vya juice, mandazi na ice cream hatuwezi kuuza nje ya Afrika.

Tunahitaji mapinduzi ya kilimo ili tuuze nje, kuna soko kubwa la bidhaa za kilimo sema sisi hatujui sababu ya kukosa elimu ya masoko na serikali kutotoa mchango mkubwa.

Shilling inaporomoka sana kwa sababu tunatumia pesa nyingi ya kigeni kuagiza lakin sisi hatuuzi.

Pia kutangaza sana utalii utasaidia wageni kuja ila cha kusikitisha ni kuwa kampuni nyingi za utalii zinamilikiwa na wageni pamoja na hivyo tukileta watalii wengi watakuja na pesa watabadilisha hivyo tutapata pesa za kigeni.

Mwisho mlioficha pesa huko Uswisi na sehemu nyingine mje basi mziweke kwenye bank za Tanzania itasaidia.

Ni hayo tu. (money stunna )
 
Swadakta kabisa Mkuu,shida ni kwamba viongozi wetu hawalioni hilo
 
Upo sahihi. lakini ujue pia Kufanya Kilimo unahitaji uwe na Roho Ngumu kama Paka. Kilimo chetu kwa asilimia kubwa ni cha kutegemea Mvua, fikiria mwaka jana 2014 Mvua zilikuwa za kutosha watu walilima na walivuna sana tu, sasa tizama mwaka huu Wakulima wamehamasika kama mwaka jana wamelima na wamepanda wakitegemea Mvua lkn hadi sasa bado Mvua zinasuasua, matokeo yake yale mazao yameanza kukauka. So tuhamasishe Wakulima Kilimo cha Umwagiliaji
 
Kilimo ni sehemu pekee ambako nchi za dunia ya tatu zinaweza kukimbilia kwenye hii transition period.Ulaya hakuna chakula na viwanda vyao vimehamishiwa China. Ila kulima tu hakuwezi kusaidia bila msaada wa serekali wa kufundisha vizuri ma afisa kilimo,na kuwekeza kwenye nyenzo za kilimo na pia kufanya trade negotiations ya mazao na nchi zinazohitaji chakula.Nina imani mtu akila kwanza akashiba ataweza kufikiria vizuri na kufikiria kufanya mambo mengine ya maana zaidi.Mtu mwenye njaa hawezi kufikiria kitu kingine tofauti na kupata chakula ,huwezi kumwambia aanzishe kiwanda au afanye biashara wakati ana njaa
 
Pia tukifungua viwanda vingi nchi kwetu ina maana hatutatumia sana dollar.
Sisi hadi maziwa twaimport, mafuta ya kupikia etc
 
adui mkubwa wa kilimo chetu ni serikali. inawanyonya sana wakulima.
1. mkulima wa chai wa kenya anapata mara tatu zaidi ya wa tanzania. hizo zingine serikali inaiba.
2. bodi za mazao kama kahawa, korosho, pamba nk, badala ya kusaidia mkulima zimegeuka mzigo na kudumaza kilimo.

3. serikali inakataza watu kuuza mazao nje. nani atakubali awekeze pesa zake na kulima halafu lije limtu na kitambi chake limchagulie pa kuuza.

4.mabenki yanakoposha wakina komba ambao wanaenda kunywa na vidosho, mkulima kupata mkopo mpaka uwe mzungu.
inabidi sera na sheria zinazosimamia kilimo zibadilishwe tena kwa kuhusisha wadau ndiyo mambo yatabadilika. kuongeza uwekezaji tu haitatosha.
 
Pia tukifungua viwanda vingi nchi kwetu ina maana hatutatumia sana dollar.
Sisi hadi maziwa twaimport, mafuta ya kupikia etc

kuna vitu ambavyo hatutakiwu kuimport kwa mfano mafuta ya kura au ya kupikia, tunalima ufuta na alizeti hivyo tunaweza kuzalisha wenyewe mafuta na kuinua uchumi wa wakulima wa alizeti na ufuta na uchumi wa nchi pia, tukiwa na nia tunaweza hata kuexport nje ya nchi.. sema ndo ivo sijui tatizo nini jamani my Tanzania..
 

yaani hili liserikali letu sijui ni lini litaamka, viongozi wamekalia ufisadi tu badala ya kuwaza masilahi ya wananchi wao
 
Njia nyengine ni kukataza matumizi ya dola ya sio ya msingi ncxhini maana mpaka ada zinalipwa kwa dola..
 
Yani inasiktisha sana sana, hapa hapa Afrika ya mashariki unaenda dukani hukuti bidhaa ya TZ !! something has to be done jamani
 
Ujumbe mzuri, ila umenipa hasira.!
 
Asante red giant kwa pointi yako namba 3.umenikumbusha machungu niliyopata.prof.jumanne maghembe alipokuwa waziri wa kilimo alifunga mipaka kuwazuia wakenya kununua mahindi.nilipata hasara kubwa na kufilisika.
 
Kilimo bira serikali kutia nia nothing will change nchi nyingine zinatengeneza ma bilionea wake .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…