Uwekezaji NSSF & PSSSF kwangu naona ni upigaji tu!

Uwekezaji NSSF & PSSSF kwangu naona ni upigaji tu!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nakumbuka huko nyuma viongozi wa haya mashirika walikuwa na pesa kama wafanyabiashara wakubwa kwasababu ya miradi ya deal.

Hebu Watanzania jiulizeni kitu kimoja

Bondi za serikali kwa miaka zaidi ya 20 sasa zinalipa 12%-16% kuna sababu gani sherika likachukuwa pesa na kwenda kuwekeza kwenye majengo au nyumba! kwasababu kwenye bond hawawezi kuiba.

Hivyo haya mashirika yangetakiwa pesa yote waweke kwenye bond na kuwa na management ndogo sana tu basi. Hivyo kila siku kulalamika tufanye nini ni ujinga pesa ziwekwe kwenye bond za serikali zote kwa 12%-16%.

Mtu mwenye Tsh 10M leo pesa wakiacha baada ya miaka 20 kwa 14% itakuwa Tsh 137,434,899. Hivyo tatizo sio mbinu za uwekezaji sababu kubwa ni wizi mtupu
 
Kuwekeza kwenye majengo kuna faida nyingi kuliko uwekezaji wa bondi za serikali.
1. Ajira kwa mafundi, vifaa vya ujenzi na management ya usimamizi wa majengo hayo.
2. Kuboresha miji
3. Kupunguza uhaba wa makazi.
4. Kodi ya pango na kodi ya ongezeko la thamani kwa huduma zote hizo.
Huwezi kuzuia faida hizi kwakuwa tu huwaamini watumishi wa mashirika hayo.
 
Back
Top Bottom