Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Baada ya kuona tunaitwa kuwekeza kwa UBIA kwenye VIVUKO; nikaingia kwenye TOVUTI yao kuona hawa jamaa wanafanya nini katika Huduma ya VIVUKO Home | TEMESA
Kwa haraka haraka naona kama kazi za hawa watu nyingi ni za administration / Usimamizi (Hivyo wanaweza wakasimamia kwa uchache au wajifute na hao so called wabia wafanye hizo shughuli ambazo naona kama ni duplication....
USHAURI WANGU
Sehemu ya Uendeshaji na Usalama wa Vivuko
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuandaa mpango kazi wa muda mrefu na muda mfupi kwa ajili ya programu za uendeshaji na usalama wa vivuko.
(ii) Kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa viwango na taratibu za usalama wa kivuko.
(iii) Kusimamia na kushirikiana kwa pamoja na mameneja wa mikoa juu ya njia bora zaidi za kuboresha utendaji kazi wa vivuko na usalama wa vivuko.
(iv) Kufuatilia na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya kila siku katika vituo vyote vya vivuko nchini.
(v) Kutathmini hali ya vifaa vya uokozi na usalama watumishi wa vivuko wanapokuwa ndani ya kivuko ili kuhakikisha kuwa wote wanatimiza mahitaji ya usalama wakati wote.
(vi) Kutathmini ufanisi wa huduma za vivuko na taratibu za usalama na kuushauri Wakala kupitia mkurugenzi.
(vii) Kupanga na kuratibu mafunzo kwa watumishi wa vivuko kuhusu masuala yanayohusu usalama wa vivuko.
(viii) Kuhakikisha taarifa zote zinazohusiana na masuala ya uendeshaji na usalama wa vivuko zinakusanywa kwa wakati.
Sehemu ya Umeme na Elektroniki
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuratibu na kuunda programu za muda mfupi na za muda mrefu za umeme na elektroniki.
(ii) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa kazi za umeme na elektroniki.
(iii) Kuanzisha na kukuza sera, mipango na programu ambazo zitaongeza na kuchochea ubora wa bidhaa za umeme na elektroniki na kazi za matengenezo.
(iv) Kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kazi za umeme na elektroniki katika vituo vya uzalishaji.
(v) Kuendeleza na kuhuisha kazi za matengenezo na huduma za ufundi, miongozo na viwango juu ya maswala ya umeme na elektroniki.
(vi) kuunda na kuanzisha utekelezaji wa viwango vya ubora wa matengenezo ya kazi za umeme na elektroniki.
(vii) Kuratibu na kuunganisha ripoti za shughuli za umeme na elektroniki.
Sehemu ya Huduma za Ushauri
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuendesha huduma za ushauri wa kiufundi.
(ii) Kumsaidia mkurugenzi wa matengenezo na huduma za kiufundi juu ya kazi za ushauri wa umeme, mitambo, elektroniki, TEHAMA na huduma za ushauri.
(iii) Kusimamia watumishi wote wa sehemu ya huduma ya ushauri wa kiufundi.
(iv) Kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa mipango kazi ya ushauri wa muda mfupi na muda mrefu kwa kazi za umeme, mitambo, elektroniki, mawasiliano ya simu na kazi za TEHAMA.
(v) Kuanzisha na kukuza sera, mipango na programu zitakazochochea ubora wa bidhaa za umeme na TEHAMA.
(vi) Kuangalia utekelezaji wa kazi za ushauri wa umeme, mitambo, elektroniki na TEHAMA.
(vii) Kuratibu na kujumuisha ripoti za kazi za ushauri wa umeme, mitambo, elektroniki na TEHAMA na kuwasilisha kwa mkurugenzi wa matengenezo na huduma za kiufundi.
Sehemu ya Ufundi na Ukodishaji Mitambo
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuratibu uundaji wa mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya kazi za ufundi.
(ii) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa kazi na mipango kuhusu ufundi.
(iii) Kuanzisha na kukuza sera, na mipango itakayochochea huduma bora za ufundi na matengenezo.
(iv)Kuangalia utekelezaji wa huduma za ufundi na shughuli za matengenezo katika vituo vya uzalishaji .
(v) Kumsaidia mkurugenzi juu ya kukuza na kuhuisha vifaa vya uzalishaji na matengenezo, miongozo na viwango juu ya masuala ya ufundi.
(vi) Kuunda na kuanzisha utekelezaji wa viwango vya ubora wa matengenezo kwa kazi za ufundi.
(vii) Kuratibu na kunganisha ripoti za kazi za ufundi na kuziwasilisha kwa mkurugenzi wa uzalishaji, matengenezo na ukodishaji mitambo kwa ujumuishaji.
(viii) Kuratibu uundaji wa mipango ya huduma ya ukodishaji mitambo ya muda mfupi na muda mrefu.
(ix) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipango ya huduma ya ukodishaji mitambo.
(x) Kuanzisha na kukuza sera, programu na mipango itakayochochea huduma bora za ukodishaji mitambo.
(xi) Kuunda na kuanzisha mipango madhubuti ya utekelezaji wa viwango vya matengenezo vya ubora wa ukodishaji mitambo.
(xi) Kuratibu na kujumuisha ripoti za ukodishaji mitambo mara kwa mara.
Kwa haraka haraka naona kama kazi za hawa watu nyingi ni za administration / Usimamizi (Hivyo wanaweza wakasimamia kwa uchache au wajifute na hao so called wabia wafanye hizo shughuli ambazo naona kama ni duplication....
USHAURI WANGU
- Kwahio ni kwamba kama TEMESA inahusiana na Usalama na sio necessarily Upatikanaji wa Faida je kuwekeza jambo kama hili kwa watu binafsi ni busara. ? Hivyo kwa ushauri kama usalama ni lazima basi kitengo hiki kipunguzwe ukubwa na wabakie na kazi ya kusimamia tu ubora...
- Na kama ni issue ya mapato kwanini tuingie UBIA na tusiwaachie watu binafsi wafanye moja kwa moja...