SoC04 Uwekezaji thabiti kuendana na hali halisi

SoC04 Uwekezaji thabiti kuendana na hali halisi

Tanzania Tuitakayo competition threads

king kibimbika

New Member
Joined
Apr 29, 2024
Posts
3
Reaction score
3
Dunia inakua kwa kasi na mabdiliko mengi yanatokea katika nyanja mbali mbali, nasi kama Tanzania tunahitaji UWEKEZAJI katika baadhi ya sekta ili tuweze kuendana na kas ya mabdiliko, kwa upande wangu, naona UWEKEZAJI ufanyike kama ifuatavyo:-

Cryptocurrency and bonding

Hii biashara mpya na watu na mataifa mbali mbali yanajihusisha na uuzaj na ununuaji wa hizi digital coins, sambamba na hilo inafanya kuwepo na matapel wengi wanajinufaisha wao na kutapel watu, hivyo serikali iwekeze kwa kutafuta kampuni inayo aminika, Kisha itoe mafunzo yaliyo kamilika ili mtu ajue faida na hasara za digital coins, hii itasaidia kwakuwa watu wengi hususan vijana tunapoteza pesa nyingi katika mitandao ya kijamii, unaweza kuta kijana anatumia Hadi elfu 30 kwa mwezi lakini haingizi hata mia kupitia hiyo mitandao, hivyo elimu na UWEKEZAJI katika sekta hii itasaidia kuinua vipato vya watu na hata kupunguza tatzo la ajira, kwakuwa sasa watu wengi wanamiliki smart phones hivyo itakuwa rahisi watu kujiajiri kupitia njia hiyo

Elimu
Ni wakati sasa kuangalia masomo tunayosoma yanatusaidia Nini, asilimia kubwa ya masomo tunayosoma yanatuandaa kwenda kuajiliwa, zaman ilikuwa ukisoma ukimaliza tu uhakika wa kuajiliwa ni mkubwa nyakati zimebadilika lakin mifumo yetu ya elimu haijabdilika, hivyo Kuna umuhim kutoka kwenye hiyo namna ya ufundishwaji(maarifa) na kuhamia kwenye ujuzi ndio ujuzi, sasa watu wanaotengeneza pesa nyingi ni watu wenye ujuzi na sio maprofesa.

Hata ukiangalia orodha ya watu matajiri duniani wengi Wana ujuz wa kutengeneza au kuzalisha kitu. hivyo ni muhim kuachana na elimu ya kukariri zaid tuwekeze kwenye elimu ya ujuzi,watu waweze tumia ukuaji huu wa sayansi na teknolojia kujipatia kipato kwa kuwezeshwa, na kuwekeza katika ujuzi wao, innovation zinafanyija chuo ikiwezekana hata wanafunzi wa sekondari pia wafanye, na wagunduzi waliobun kitu Bora, wapewe wataalam wa kuwasadia,kuwaongezea maarifa na kuwaendeleza, sio kuwacha na ubunifu wao kuuweka tu stoo

Kilimo

Watu wanasema kilimo ni uti wa mgongo, ni kwel sabab asilimia kubwa ya maisha tunayoish yanaendeshwa na kilimo mfano nguo tunazo vaa zinatokana na kilimo, vyakula tunavyokula ni kilimo,kwa kias tumepiga hatua kwenye kilimo lakin wakulima wadogo wengi bado hawafaidika, hivyo Kuna umuhim wa kuwekeza wkwenye kilimo, hasa kupunguza Kodi kwenye pembejeo za kilimo, ili wakulima waweze kuwekeza kwa wingi, kama tukiwa na mzao mengi Hadi kuweza kuuza nje ya nchi itasaidia kupata fedha za kigen, kwahyo serikali ikipunguza Kodi, itakuja kufaidika baadae kwenye uuzwaji, kilimo kinaweza kutuokoa sana kutokana na Tanzania kubarikiwa ardhi nzur inayofaa kwa kilimo hivyo, tukiboresha hii sekta na UWEKEZAJI ukafanyika kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia, kilimo kitatuinua sana na vijana wasio na ajira watapungua maana vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo kutokana na gharama kuwa kubwa sana.

Tiba asili

Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watumiaji na wauzaji wa madawa asili,mengi Yana wasaidia watu, huku wengine wakiwa matapeli. So serikali ijarib kukaa nao hao watu wa tiba asili na kujalib kuwawezesha kuanzia uzalishaji kwa kuwapatia vifaa vya kisaa Hadi utunzwzji wa bidhaa zao. pia kuweka sera itakayo Linda bidhaa ya mtengenezaji dhidi ya wezi .wengi tunatumia supplement kutoka mataifa mbali mbali, lakin ukichunguza kwa ndan baadhi ya supplement ni vitu asilia kabisa labda ni miziz, au majan ambayo yametengenezwa vizur na kupewa package nzur, japo chache Zina chemichals.

Hivyo serikali ikiwekeza huku kwanza itapata Kodi kutokana na uuzwaji wa hizo dawa pia itasaidia watu wengi kujiajili lakin pia afya za watu Zita imarika maana dawa zenye chemicals lazima ziwe na side effects kwenye mwili wa binadamu hivyo kuaribu afya ya mtumiaji taratibu, lakin dawa asili hasara yake ni ndogo sana. tukiwekeza hapa vilivyo hakika tunaweza uza hata nchi zengine

Sanaa na michezo

Hii sekta imekuwa ikitoa matajiri wengi akina Ronaldo, Messi, lebron James, Jay-Z hata mbwana sammata, alikiba kwa Tanzania na wengineo wengi wameweza kukusanya pesa mingi kupitia Sanaa na michezo.

Serikali iwekeze kwenye miundombinu ya michezo na swala la michezo liwe linatiliwa mkazo tangia mashulen, maana wachezaj wengi Tanzania wanacheza mpira au kufanya Sanaa baada ya kufel shule au wengine Wana degree na ni wasomi kabisa wanaamua kuingia kwenye sekta hii kujarib kama plan B, hivyo ukifanyika UWEKEZAJI wenye maana Sanaa na michezo itakuwa ndoto kama ilivyokuwaga kwa engineer,daktar ama kazi yoyote ya kitaaluma.

Tukiwekeza kwenye Sanaa na michezo tutaokoa Namba kubwa ya vijana wasio na ajira.
Sanaa ya uchoraji, uchongaji, muziki na kadhalika imetoa matajiri wengi hata wengine kumiliki galely ambayo watu hutembelea na kuona kaz za Sanaa Kisha wahusika kujipatia kipato, tukiwekeza kwenye Sanaa na watu wenye vipaji wakathaminiwa kama wanavyothaminiwa w maprofesa au wanasiasa, utafanya Sanaa na michezo kuwa ndoto ya Kila mtu kama ilivyokuwaga kwa engineer, doktor na kazi zengine za kitaaluma

Mwisho

Mtu akijua kusoma ,kuandika na kuhesabu,pia aijue nchi yake ili aweze kuwa mzalendo ,Kisha akaijua sayansi ili imsaidie kukabiliana na mazingira.akaujua utamadun wake ili akaulinda nankuuish maana ndio u
tambulisho wake, vitu vingine tukapunguza tukaweka vitakavyo msaidia Moja kwa moja kwenye ukuaji wa maisha yake, ila professional zibaki kuwa professional, walimu waendelee kusoma vitu vinavyowahusu, madktar na professional zote, hivyo ndio naona Tanzania inaweza kukua kwa miaka 25 ujayo,
Ahsanteni..🙏
 
Upvote 4
Back
Top Bottom