Uwekezaji wa majengo haulipi

Kwa nini hoteli nyingi zinachakaa wakati zinaingiza fedha?
Kwa sababu hata hizo biashara unazosema zinachakaa wakati zinaingiza fedha.

Nikiwa Manispaa fulani jijini Dar alikuja brother kutoka Dodoma akajenga kwenye kiwanja alinunua kwa 46M mwaka 2018. Akajenga rentals 10 units chumba self na jiko uchwara kwa kutumia milioni 80 na chenji. Mwenyewe yuko kwenye mid 40s.
Jumla hapo katumia 126M+.

Hizo nyumba anapangisha 130k kama mbili hivi na 150k nyingine.
130k×2=260,000
150k×8=1,200,000
Total 1,460,000 kwa mwezi.

Nyumba za kupangisha inategemea na quality ila nina family relative namjua tangu nahitimu sekondari nilimkuta amejenga nyumba mpaka naandika hapa hajawahi zirekebisha lolote wala kubadili mifumo ya umeme wala maji, kwanza hayupo hata nchini. Miaka 10+.

Sasa huyo brother 1,460,000 wa kwa mwezi kwa mwaka ni 17.52M. Kwa miaka 10 ni 175.2M. Sasa cha ajabu ni kwamba eneo lilelile aliponunua ardhi, pembeni kiwanja kingine (exactly nusu ya kama alichojenga) kimeuzwa last year July kwa 45M nikiwepo. Maana yake yeye kiwanja pekee chenye units 10 hata ukizibomoa zote kinabaki na thamani ya 70M kwa bei ya July 2025, kimepanda thamani mara mbili ndani ya miaka 7.

Miaka 10 ijayo kiwanja chake kitakuwa na about 150M valuation. Kodi atakayokusanya ndani ya miaka 10 atakuwa na 175.2M. Total 325.2M.

Sasa hapo ukitoa miezi michache bila wapangaji, yuko mjini sehemu hot. Na miezi michache ya kusamehe kodi wapangaji wasumbufu. Bado anabaki na faida.

Alafu sasa anaweza kopea hicho kiwanja mkopo akafanya hizo biashara zako unazosema haziziki hela. Alafu baada ya miaka 10 umkute hajakarabati nyumba useme hela haikurudi ndio maana kaziacha. Kumbe ameishajifia watoto wake ni vilaza wanalewea pombe, sasa assume hao walevi angewaachia duka la vipuri au bar. Mwaka mwingi duka limepukutika.
 
Biashara za miaka 10 zilishapitwa na wakati, mfano; leo hii jf wakiweka ada ya kwa mwezi shilingi 1000, kuna uwezekano wakawa wanapiga milioni 500 kila mwezi.
 
Mahesabu yako nimeyapitia, ila ebu jiulize swali, mfano leo hii jf wakaamua kututoza ada ndogo tu kwa mwezi sh. 1000 unahisi wanaweza kutengeneza kitu gani? Ni zaidi ya milioni 500/mwezi, Hii ndio maana halisi ya 80/20 rule
 
Biashara za miaka 10 zilishapitwa na wakati, mfano; leo hii jf wakiweka ada ya kwa mwezi shilingi 1000, kuna uwezekano wakawa wanapiga milioni 500 kila mwezi.
JF ilianza mwaka 2006 isingekuwa na malengo ya muda mrefu ungekuwa Facebook na wenzako mnasoma story za Idi Makengo. Mimi ningekuwa Quora na Reddit.
 
JF ilianza mwaka 2006 isingekuwa na malengo ya muda mrefu ungekuwa Facebook na wenzako mnasoma story za Idi Makengo. Mimi ningekuwa Quora na Reddit.
80/20 rule unaifahamu inavyofanya kazi?
 
80/20 rule unaifahamu inavyofanya kazi?
Na ukasome debt financing, pia usome diversification. Maana unaamini aliyejenga nyumba za biashara aliokota hela tu hivyo hana kitu cha kufanya kilichompa hiyo hela.

Unajua kuwa mtoto wa Bakhressa amejenga mji kabisa, achana na nyumba? Umeisikia ile Fumba town? Sasa huyo ni mtoto wa rich family ambaye ana access na mabilioni ya mitaji, ameishafanya mitambo, logistics, production, supply, importation, food packaging na mambo chungu nzima ila kawekeza kwenye nyumba. Wewe ukute ukoo wa wakulima wa viazi unapinga vikali real easte. Kijana badilika.
 
Kujenga majengo hakuna shida, je hizo hela ulizowekeza zitarudi baada ya miaka mingapi?
 
Sasa unadhani ni biashara gani ambayo ukiwekeza ina guarantee ya faida 100% na unaanza kula faida muda huo huo?
 
Risk free.
Mtu hata awe mwizi kiasi gani hawezi kuiba nyumba na kukimbia nayo ila biashara zingine msaidizi wako akiamua tu siku moja anabeba mzigo wote na kupotea nao kisha unakuwa maskini tena.
 
kila biashara ina changamoto zake. namfahamu mtu ame inject 1+ bil tzs kwenye hiyo biashara pale Kariakoo na Upanga, mtaji haujarudi bado ila baada ya miaka chini ya kumi utakuwa umerudi. ni commitment tu.
 
Hawa watu sasa hivi tunawaacha na hizi thread zao maana hata ukiwapa mifano hai wanaumia watabaki kusema unajimwambafai. ASIEJUA MAANA HAAMBIWI MAANA.
 
Mkuu umeongea vema.
 
Recoup katika real estate ni miaka 8-15. Hivyo unapofanya uwekezaji katika eneo hili unapaswa kulijua hili.
Kuhusu kulipa au kutokulipa kwa uwekezaji kwenye majengo siri yake ipo kwenye location. Ndio maana majengo yenye zaidi ya miaka 100 yaliyopo msasani beach, upanga yana return kubwa kuliko mahekalu ya bweni beach au bunju beach. mfano; Apartment ya vyumba 3 yenye sqm 200 pale Palm Village inauzwa mil 650-750 wakati hekalu la ghorofa vyumba 5 lenye sqm 2500 Mbweni mil 200-400
Ukweli mchungu ni kuwa ni ghali sana kuwekeza majengo katika prime areas. initial investment cost ni super expensive jambo ambalo linawafanya baadhi ya watu wawekeze apartments goms, chanika au kongowe. Ukifanya miscalculation yakujenga gharofa ya kifahali katika eneo lisilo sahihi ni vigumu kupata faida hata ikipita miaka 30, na hata ukiamua kuuza utauza kwa hasara. Hii ndio sababu mchina yupo tayari kutoa 1Bil kukununua sqm 450 msasani kuliko kutoa mil 200 kununua sqm 2000 mweni. Tuongoze umakini katika maamuzi ya ununuzi wa plot kuliko katika kuendeleza kwani ukikosea kununua hautaweza kurekebisha kasoro hata ujenge jengo zuri vipi ila ukikosea kujenga unaweza kurekebisha au hata kuuza kwa faida
 
Chai
 
Mfano nina milioni 200, itanichukua miaka mingapi kuipata hiyo milioni 200 niliyoiwekeza?
Inategemea uwezo binafsi wa mtu katika kuratibu au kupanga mikakati, Binafsi yangu ndani ya mwaka hadi miaka miwili naweza kurudisha hiyo pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…