Uwekezaji wa Mo Dewji Simba na Udhamini wa Azam kwa Yanga

Jr king

Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
50
Reaction score
55
Heshima kwenu wakuu...

Moja kwa moja niingie kwenye mada husika. Kumekuwa na mkanganyiko kati ya uwekezaji uliofanywa na Mo pale Simba na udhamini uliofanywa na Azam kwa wanandinga wa Jangwani.

Sisi wa Buhigwe kitu kinachotuchanganya ni kuwa ina maana Mo ataimiliki simba maisha kwa hiyo 21B? Na yanga amejidhaminisha 41B kwa miaka 10 tu?

Sasa kama ni hivyo mbona kama Simba tumepigwa?

Tafadhali wajuzi wa Mambo tuelimisheni hicho kitu.
 
Tafuta maana ya uwekezaji na udhamini. Kwa mfano MO kwa miaka minne sasa anaipa support Simba ya karibia billion tatu kila mwaka. Maana yake mpaka sasa ameisha toa 12 B. Lkn ile 20 B iko pale pale.
 
Ngoja waje uone watakavyo kuparua na ile mikucha yao! 👹
Kikubwa kinachotusumbua sie wa nyarubanja huku...Ni kushindwa kutofautisha Kati ya uwekezaji na udhamini, Tupigeni msasa hapo
.
 
Ngoja waje uone watakavyo kuparua na ile mikucha yao! 👹
Mm nina watu mzee wangu, siogopi hiyo mikucha yao....Simba tumeipambania Sana hatuwezi kukubali iangukie mikononi mwa mabwenyenye kirahisi namna hiyo......Narudia Nina watu.
 
Ninyi wajuvi wa Mambo ndio mnapaswa kututofautisha Kati ya uwekezaji na udhamini, sie huku nyarubanja Kigoma ni giza tororo......

Tafuta maana ya uwekezaji na udhamini. Kwa mfano MO kwa miaka minne sasa anaipa support Simba ya karibia billion tatu kila mwaka. Maana yake mpaka sasa ameisha toa 12 B. Lkn ile 20 B iko pale pale.
 
Tafuta maana ya uwekezaji na udhamini. Kwa mfano MO kwa miaka minne sasa anaipa support Simba ya karibia billion tatu kila mwaka. Maana yake mpaka sasa ameisha toa 12 B. Lkn ile 20 B iko pale pale.
Wewe wasema!
 
Bilion 20 ipo pale pale wapi ambapo hapana jina?
 
Jambo liko wazi, udhamini wa Simba ni mkubwa kuliko uwekezaji kwenye timu.
 
Udhamini anaofanya AZAM sasa unakuwa kielelezo na kuwaonyesha wawekezaji uchwara kwenye michezo nchini. Mimi ni mpenzi wa Simba ila nia ya Mo Dewji kuwekeza Simba imekuwa kujijenga yeye zaidi kuliko timu.

Azam ametuonyesha kuwa hisa 49 za Simba sio Bilioni 21 anazotaka kuweka Mo.
 
Tafuta maana ya uwekezaji na udhamini. Kwa mfano MO kwa miaka minne sasa anaipa support Simba ya karibia billion tatu kila mwaka. Maana yake mpaka sasa ameisha toa 12 B. Lkn ile 20 B iko pale pale.
Simba imekuwa sehemu yake ya kutengeneza faida, angalia jezi ya Simba imejaa matangazo yake tayari. Kwa hiyo hizo anazotoa hatoi kama charity.
 
Kwani nani kasema charity mi nimeongelea udhamini na uwekazaji, ningetaka kuongelea charity ningeongelea MO foundation. Uwe unasoma na kuelewa
 
Udhamini anaofanya AZAM sasa unakuwa kielelezo na kuwaonyesha wawekezaji uchwara kwenye michezo nchini. Mimi ni mpenzi wa Simba ila nia ya Mo Dewji kuwekeza Simba imekuwa kujijenga yeye zaidi kuliko timu.

Azam ametunyesha kuwa hisa 49 za Simba sio Bilioni 21 anazotaka kuweka Mo.
Ukifanya breakdown ya udhamini wa Azam ni kwamba Yanga atakua anapata karibia billion tatu kwa mwaka, kitu ambacho MO ameanza kutoa miaka minne nyuma, utasemaje uwekezaji sio udhamini wa MO wa billion 20 kwa mkupuo ni ubabaishaji. Naona wewe ndio mbabaishaji.
 
Back
Top Bottom