SoC04 Uwekezaji wa vijana

SoC04 Uwekezaji wa vijana

Tanzania Tuitakayo competition threads

procee

New Member
Joined
Mar 15, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Napenda kushiriki katika story of change kwa kutoa mawazo, mapendekezo na maoni yangu juu ya Tanzania tuitakayo. Yapo mengi ambayo ningependa kuyazungumzia katika mada hii lakini ushiriki wangu utaangazia zaidi juu ya suala la Uwekezaji kwa Vijana.

Nini maana ya uwekezaji kwa vijana?
Uwekezaji kwa vijana ni pamoja na kuwawezesha vijana katika nyanja mbali mbalimbali nchini kwani uwezeshwaji wa vijana unapelekea kukuwa kwa sekta mbalimbali nchini kwakuwa shughuli nyingi za vijana zimejikita na zinagusa nyanja mbali mbali ikiwemo uchumi, kilimo, teknolojia, michezo na Sanaa, pamoja na uongozi.

Kwanini vijana wawezeshwe Zaidi?
Idadi kubwa ya watu Tanzania ni vijana wenye umri kati ya miaka 20 mpaka 45 ikiwa ni kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Idadi hii inaonesha ni jinsi gani vijana ni nyenzo muhimu ambayo kama ikisimamiwa na kufanyiwa uwekezaji mzuri inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika taifa hili. Matokeo ya sensa pia yanaonesha kuwa idadi kubwa ya vijana hawana ajira zilizo rasmi ambao wengi ni wahitumi wa elimu kwanzia ngazi ya sekondari mpaka vyuo vikuu.

Ukosefu wa ajira za uhakika kwa vijana imekuwa ni changamoto kubwa kwa vijana na taifa kiujumla. Licha ya kuwa na changamoto ya ajira nchini, wapo baadhi ya vijana waliobuni na kuibua mawazo mbali mbali ya kibunifu kama vile machinga, wakulima wadodo wadogo na waendesha boda boda, hizi zote zikiwa ni juhudi zao binafsi katika kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini. Kama vijana hawa wakiwezeshwa inaweza kuwa njia bora zaidi yenye kulenga kuwapa kujiamini na kuwajengea uwezo wa kujipambania zaidi ili kuchochea maendeleo yao binafsi na maendeleo ya taifa kiujumla ambapo katika kipuindi cha miaka 5 mpaka 10 ijayo tunaweza kuwa na vijana wenye maendeleo kwa kiasi fulani.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la visa vya kujiua, matumizi holela ya madawa ya kulevya, ulevi, ukatili na uhalifu nchini ambapo inaripotiwa kuwa vijana ndio wanaohusishwa zaidi na matukio haya. Hii inaonesha ni jisi gani vijana wa kitanzania wanakubwa na changamoto mbali mbali ambazo kama zisipo patiwa ufumbuzi itakuwa vigumu sana kama taifa kuifikia ndoto ya Tanzania tuitakayo hususani katika miaka 10 mpaka 50 ijayo.

Ili kuwa na mabadiliko ya kimaendeleo katika taifa letu laTanzania ni muhimu serekali, taasisi binafsi na wadau wa maendeleo kuwekeza kwa vijana kwa kuwajengea uwezo wa kujiamini na kujitambua kuwa wao ndio nguvu kazi au nyenzo muhimu ya maendeleo ya taifa hili kama ilivyo katika lolote apa duniani. Nikiwa kama kijana wa kitanzania mwenye nia ya dhati ya kuifikia “Tanzania tuitakayo” naona ni vyema serekali kuwatazama zaidi vijana kwani baadhi ya vijana wana mawazo chanya, ubunifu, ujuzi na maarifa lakini wanakosa uthubutu na kushindwa kujiamini kwa kukosa msaada (support) hali inayopelekea kuwa na uwezo mdogo (low productivity) katika nyanja mbali mbali hususani katika uchumi.

Uwekezaji kwa vijana unaweza kuwaongezea vijana kujiamini na kujitumza zaidi kwani njia hii inaweza kuwasaidia vijana wengi kuondokana na na msongo wa mawazo unaosababishwa na ugumu wa maisha unaopelekea wengi wao kujiua na kuingia kwenye matumizi holela ya dawa za kulevya, kubeti na ulevi. Kabla hatujaendelea ebu jiulize Je! mtaani kwako ni vijana wangapi wamekata tamaa na kujiingiza katika matumizi holela ya dawa za kulevya pamoja na matukio mengine ya kihaliffu ambao pengine kama wangepatiwa misaada na kujengewa uwezo wangekuwa tofauti na walivyo sasa?

Uwekezaji kwa vijana unahusisha nini na unaweza kutekelezwa vipi?
Uwekezaji kwa vijana unahusisha kuwajengea vijana uwezo wa kujiamini na kuwa na mawazo ya kibunifu katika biashara, kilimo, teknolojia pamoja na kuibua vipaji mbali mbali katika sanaa na michezo. Hii inaweza kuwa njia moja wapo ya kutatua changamoto zinazo wakumba Vijana wengi wa kitanzania kwani wengi wao wanakosa support katika kuanza, kujiendeleza na kujiimashisha zaidi katika kuwa wabunifu na shughui mbali mbali za kiuchumi, jambo linalopelekea vijana wengi kushindwa kuendana na kasi ya ukuwaji wa uchumi duniani kwani mabadiliko ya kiuchumi yameathiri kwa kiasi kikubwa uchumi kwa kiasi kikubwa kwani gharama za maisha zimeongezeka zaidi jambo ambalo linathiri baadhi ya shughuli za vijana wengi wa kitanzania na kupelekea kukata tamaa na kushindwa kuzifikia ndoto zao. Ili kuifikia Tanzania tuitakayo, ni muhimu sana Serekali kushiriki katika kuwainua vijana na kujikita zaidi katika kuwajengea uwezo na kukuza ujuzi zaidi kwa vijana katika sekta mbali mbali ikiwemo teknolojia, kilimo biashara pamoja na ubunifu katika sanaa na michezo ili kuruhusu vijana wengi kushiriki katika shuhuli za maendeleo yanayoweza kutuletea Tanzania tuitakayo kama ifuatavyo;

Serekali pamoja nataasisi za maendeleo zinaweza kuwawezesha vijana wa kitanzania kupitia utoaji wa mitaji na mikopo nafuu ili kuwawezesha wale walio jiajiri na wenye ujuzi katika fani mbalimbali kujiendeleza zaidi, pamoja na wale wenye mawazo yenye kuleta matokeo chanya katika jamii. Hata hivyo Kumekuwa na jitihada mbali mbali zilizofanywa na serekali pamoja na taasisi binafsi katika kuwawezesha vijana, mfano kampeni iliyofanywa na benki ya CRDB iliyojulikana kama ‘IMBEJU’ ya mwaka 2022 ambayo ililenga uwezeshwaji wa vijana na wanawake wajasiriamali ambapo takribani bilioni 5 zilitengwa kwa mujibu wa bank ya CRDB. Niwakati sasa wadau wa maendeleo, taasisi binafsi na Serekali kiujumla kuhamasika na kuwafikia vijana wengi zaidi na kuwajengea mazingira wezeshi katika shughuli mbali mbali za kiuchumi kama vile biashara ndogo ndogo mfano machinga kwa kuwapa mikopo nafuu, wakulima wadogo wadogo kupitia kampeni ya kilimo biashara, pamoja na kuwekeza zaidi katika kukuza na kuibua vipaji na ubunifu wa vijana katika Sanaa na michezo, kwakufanya hivyo katika kipindi cha miaka 5 mpaka 10 ijayo vijana wengi watakuwa na uwezo na maendeleo kwa kiasi kikubwa.

Vilevile taasisi binafsi na serekali wanaweza kuwainua vijana kupitia kuwapa mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali yenye kulenga kutatua changamoto mbali mbali zinazoikumba jamii kwani vijana wengi hawana uelewa juu ya namna ya kubuni na kuibua fursa za kiuchumi ilihali kuna fursa nyingi za kiuchumi katika jamii mfano kilimo biashara, ufugaji, uwekezaji katika hisa na nyingine nyingi ambazo zinaweza kuwawezesha vijana kwendana na kasi ya ukuwaji wa uchumi duniani ambapo katika kipindi cha miaka 5, 10 hadi 25 ijayo vijana wengi watakuwa wajasiriamali na wabunifu zaidi endapo wakiwezeshwa zaidi.

Serekali na taasisi binafsi pia zinaweza kuwawezesha vijana kwa kuwajengea ujuzi na maarifa kwa vijana hususani matumizi ya tknolojia, kwamfano; serekali inaweza kutenga bajeti kwaajili ya kuendeleza vijana katika tecnolojia kama inavyofanywa katika nchi nyingi ikiwemo Rwanda na Kenya. Uwekezaji katika Teknolojia na Tehama unaibua fursa mbali mbali kama vile uchumi wa kidigitali “digital economy” ambayo ndio sera ya uchumi wa dunia kwa sasa. Vijana wengi hawana uelewa juu ya matumizi ta teknolojia hususani akili bandia “AI” katika kuibua fursa mbali mbali za kiuchumi kitu ambacho kinaweza kusababusha kupungua kwa kasi ya ukuwaji wa uchumi nchini. Nchi nyingi zilizo endelea mfano Korea, China na Marekani zimewekeza zaidi katika maendeleo ya teknolojia kwa kuwawezesha vijana wabunifu kuendeleza na kukuza bunifu zao jambo ambalo liapelekea kukuwa kwa uchumi.

Kwa kuhitimisha; Binafsi napenda kuwashauri vijana wenzangu kujijengea uwezo wa kujiamini na kuwa na uthubutu kwani kwa kupitia kujiamini wanaweza kushiriki katika fursa mbali mbali ikiwemo, biashara, ubunifu katika tehama, ubunifu katika kilimo biashara, ushiriki katika siasa na uongozi kwa kufuata maadili ya haki na utu kwani kwa kufanya hivyo tunaweza kuwa katika nafasi nzuri ya maendeleo ili kusudi katika kipindi cha miaka 5, 10 mpaka 25 ijayo tuwe na vijana wenye uwezo mkubwa katika taifa letu na tuweze kuifikia “Tanzania tuitakayo”. Asante kwa kusoma stori hii.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom