Uwekezaji:zijue fursa mbalimbali za kiuchumi wilayani lushoto,tanga.

Bw.Daffa

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
420
Reaction score
116
Assalam Aleykum Wana Jf.

Nategemea kama wajasiliamali mlifuatilia KONGAMANO kubwa la uwekezaji kanda ya kaskazini lilofanyika pale jijini Tanga

Nadhani itakua busara kama ntaibua fursa mbalimbali za Kiuchumi ktk moja ya Wilaya za Mkoa wa Tanga,Lushoto.
Labda nianze kwa kukupa taarifa fupi kuhusu wilaya hii ambayo kwa upeo wangu bado kuna fursa nyingi hazija tumiwa ipasavyo(under utilized).
Lushoto ipo upande kaskazi mwa wilaya ya korogwe,upande wa Kaskazini mashariki inapakana Kenya,na maghalibi kuna Kilimanjaro,Ipo barabara kuu ya Rami kutoka mombo hivyo kuunga kwenye Barabara ya Dar to Arusha Road. Hali ya hewa na ubaridi kwa Imezungukwa na milima ya Usambara.
Naam,nisiwachoshe sana ni mention fursa hizi zifuatazo:
*Hali ya hewa inaruhusu kilimo cha matunda na mbogamboga lakini bado wakulima wanalima kwa scale ndogo na bila kutumia mbinu za kisasa,Soko sio zuri kwani hakuna Wasambazaji wa kutosha,Hivyo kama hufkirii kulima unaeza kununua mazao kutoka kwa wakulima.
*Ardhi ya kutosha ipo kwan wakulima hulima vijishamba vidogodogo.Mbali na Matunda na mboga pia Mahindi,mpunga,maharagwe,viaz mviringo pia vinamea hasa Lushoto Magharibi km Mlalo,lukoz,mkuz,mtae n.k
*Lushoto mjini hakuna Maabara nzuri ya kisasa ya binafsi.
*Pamoja na uwepo wa Vyuo kama SEKOMU,Ija na shule kubwa kama St.Mary's Mazinde juu,Kifungilo na Shambalai High School bado hakuna Maktaba nzuri ya Binafsi wala Tuition Center ya Kudumu.Hii ni Fursa kwa walimu ambao kimsingi Mshahara hautoshi.
*Kwa wenye kutaka Ufugaji wa Kuku ama mifugo mingine,bas Mazingira ni Rafiki sana kwani ni Eneo ambalo kuna nyasi za kutosha na Ukame sio sifa ya Lushoto.
*Ni wilaya yenye kuvutia watalii hasa hali ya hewa ya ubaridi baridi na Milima ya Usambara,hivyo Hotel za Kitalii pamoja na Migahawa ya Kitalii ni Biashara yenye soko la uhakika
*Uwepo wa Vyuo umeichangamsha sana hii wilaya,Ila bado hakuna maduka makubwa ya kisasa(kuna Mini-Supermarket moja tu) taasisi za fedha kama Benki ni NMB NA CRDB...Niishie hapo naamini wapo wanoijua hii wilaya zaidi wataongezea:
KARIBUNI LUSHOTO
 
Assalam Aleykum Wana Jf.

Nategemea kama wajasiliamali mnafuatilia Mkutano mkubwa wa uwekezaji kanda ya kaskazini unaofanyika pale mjini Tanga.

Kiongozi, lile lilikuwa ni Kongamano na sio Mkutano. Hapo kwenye red inatakiwa iwe uliofanyika maana tukio lilikuwa tarehe 26-27/09/2013. Kongamano lilitulia na nilikuwepo pale Mkonge Hotel.
 
Kiongozi, lile lilikuwa ni Kongamano na sio Mkutano. Hapo kwenye red intakiwa iwe uliofanyika maana tukio lilikuwa tarehe 26-27/10/2013. Kongamano lilitulia na nilikuwepo pale Mkonge Hotel.

Mkuu nashukuru,Nishaedit tayari
 
Je naweza kufungua barber shop ya kisasa hapo?

Kwanza ni kushujuru kwa kuibua hoja ya Barber shop,Unaweza mkuu kumbuka hii wilaya inakua kwa kasi ikichagizwa na vyuo pamoja na Uwepo wa wafanya biashara kutoka nje ya wilaya hasa wachaga
 
Nikihitaji kulima,
Bei za Mashamba zikoje?

Bei za mashamba hasa kwa maeneo ya Kilimo zaidi sio Gharama kubwa kwani Wakulima wengi wanauza na kubaki na Ardhi ndogo kwa ajiri ya Familia tu. Sina gharama halisi ila Ukifanya utafiti naamini bai itakuridhisha
 
Niko lushoto tangu 2010 naweza sema naijua lushoto kimazingira na kibiashara...ni kweli kilimo kinakubali sana hasa mazao ya maharage viazi,karote,kabichi,nyanya,vitunguu,matunda n.k tatizo kubwa linakuja kwenye upatikanaji wa ardhi ni mgumu kutokana idadi kubwa ya watu hasa wazawa kwani wazee wa kisambaa wana kawaida ya kuoa mke zaidi ya mmoja hivyo wakua na watoto wengi sana,halafu jiografia yenyewe ni ya milima mashamba mengi yapo milimani,mara nyingi kilimo chao hukifanyia kwenye "vitivo" (mabonde membamba) ambapo hawakubali kuuza kutokana na potentiality yake.

Pili kibiashara lushoto bado sanaa mzunguko wa hela ni mdogo sana kwa hapa center biashara ni wakati wa uwepo wa wanafunzi hasa wa Ija coz hiki ndio chuo ambacho kipo mjini mara nyingi wakiondoka mji unakua doro mnoo pia na wenyeji wa hapa bado hawajawa na muamko kama sio wa kabila lao wanaweza wasikupe ushirikiano kwenye biashara yako unless uwe unaweza kuongea kilugha chao kisambaa....tatu kuhusu tuition center hapo ni mtihani hata ufanye bure unaeza usipate mtoto hata mmoja Kwa ujumla lushoto bado sana haina muamko ni tofauti kabisa na mombo,korogwe au muheza na hii ni kutokana na muingiliano mdogo wa makabila tofauti tofauti na wasambaa wana wivu na roho za kwa nini hawapendi kuona mwenzao anaendelea yani hata wao kwa wao hawapendani.
 
Nina mashaka kuwa haya ni mawazo ya mtu ambaye hajafanya utafiti, pamoja na kuwa Lushoto toka wakati huo, bado haikupi kibali cha kuweza kushutumu bila utafiti. Kwanza nikujulishe kuwa Lushoto kama wilaya ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu kuliko wilaya nyingine mkoani Tanga. Ina uchumi mkubwa kuliko Korogwa, Muheza na Mombo unayosema. NI wilaya ya Kitalii, imetambuliwa hivyo kitaifa. Ni kweli kuna vitu kadhaa ambavyo ni vya kuangalia kwa kina, uwezo wa uwekezeji, nafasi ya kuweza kupanua uelewa wa watu kwa kutumia maeneo waliyonayo kibiashara zaidi. Mwingiliano kwa upande wa mjini ni mkubwa. Kwa upande wa vijijini ni kama ilivyo maeneo mengine mengi ya Tanzania. Tunaona ipo nafasi ya kuwekeza, japo maeneo ni shida kwa kuwa ukweli ni kuwa idadi ya watu ni kubwa (kumbuka ni wilaya ya kwanza kama sio kati ya zile za kwanza kutambuliwa rasmi kama wilaya). Ni kati ya wilaya ambazo umeme umekuwepo kwa mjini tokea miaka ya 1930. Nisiseme sana ila nipende kukumbusha kuwa ni vizuri kuzungumza kwa kufuata mambo ya kina ya kiutafiti na isiwe kiushabiki.
 
Kweli kabisa mkuu,Na kuhusu Mwamko wa elimu si wazazi na wanafunzi tu pia Hakuna walimu waliomua kwa kwa dhati kuanzisha kituo cha kuto elimu(Fursa)...Nimeshangaa sana kufananisha Lushoto na Mombo,Korogwe n.k Lol!
 
Niko lushoto tangu 2010 naweza sema naijua lushoto kimazingira na kibiashara...ni kweli kilimo kinakubali sana hasa mazao ya maharage viazi,karote,kabichi,nyanya,vitunguu,matunda n.k tatizo kubwa linakuja kwenye upatikanaji wa ardhi ni mgumu kutokana idadi kubwa ya watu hasa wazawa kwani wazee wa kisambaa wana kawaida ya kuoa mke zaidi ya mmoja hivyo wakua na watoto wengi sana,halafu jiografia yenyewe ni ya milima mashamba mengi yapo milimani,mara nyingi kilimo chao hukifanyia kwenye "vitivo" (mabonde membamba) ambapo hawakubali kuuza kutokana na potentiality yake.

Pili kibiashara lushoto bado sanaa mzunguko wa hela ni mdogo sana kwa hapa center biashara ni wakati wa uwepo wa wanafunzi hasa wa Ija coz hiki ndio chuo ambacho kipo mjini mara nyingi wakiondoka mji unakua doro mnoo pia na wenyeji wa hapa bado hawajawa na muamko kama sio wa kabila lao wanaweza wasikupe ushirikiano kwenye biashara yako unless uwe unaweza kuongea kilugha chao kisambaa....tatu kuhusu tuition center hapo ni mtihani hata ufanye bure unaeza usipate mtoto hata mmoja Kwa ujumla lushoto bado sana haina muamko ni tofauti kabisa na mombo,korogwe au muheza na hii ni kutokana na muingiliano mdogo wa makabila tofauti tofauti na wasambaa wana wivu na roho za kwa nini hawapendi kuona mwenzao anaendelea yani hata wao kwa wao hawapendani.

Ndugu yangu afadhali umetoa wasiwasi wako Kuusu wilaya hii kongwe hapa Nchini,
Nikianza na uzoefu wako wa tangu Mwaka 2010,Mimi ni mzawa wa huko hivyo mabadiliko mbalimbali nimeyashuhudia Ajabu kubwa ulikuwepo tangu 2010 lakini uzoefu wako Ni Wa lushoto ya mwanzoni mwa miaka ya 2000.Na sio Lushoto ya Leo hii
Ama kwa upande wa Ardhi,ni wazi kuwa ardhi nzuri ya kilimo ni ngumu sana kuipata na ukiipata bas ni gharama,hiyo si Lushoto tu ni popote..Nilchoshauri mimi ni kwamba wapo watu wanakodisha kama hujapata kununua naamin unaweza kukodi tena kwa bei nafuu.
Ni kweli wazee wa kisambaa walikua na Utamaduni wakuoa mke zaidi ya mmoja lakini siku hizi hili swala limepungua hasa kwa kuwa Fursa za elimu zimewafikia kwa kias flani Lushoto ina watu wengi kwa sasa hasa wageni wafanya biashara
Swala la Mzunguko wa hela kuwa mdogo au mkubwa kiuchumi lina Maelezo mengi Mf. Watu kutokua na uwezo wa kununua(Low purchasing capacity),Wafanya biashara kushindwa kutangaza bishara zao vzuri hivyo watu kutonunua kwa sababu hawana ufahamu wa kutosha,Uwepo wa taasisi chache za Kifedha n.k. Ni jinsi utakavyoiweka biashara yako mkuu,mbona wapo wafanyabiashra walofanikiwa palepale.
Suala la Ukabila,hapa ndo umepotosha mkuu. Wapo wafanya biashara,wachaga,wapare na mabila mengine wamefanikiwa lakini hawajui kisambaa, hapana mkuu kuwa mkweli hapa.
Swala la mwamko wa Elimu kwa miaka hii ya Shule za kata sio mdogo kivile..Mwaka huu nimepata bahati ya kufundisha baadhi ya shule Kama mwalimu wa kujitolea na Pia nikafundisha Tuition kwa wakati mmoja pale Hazina,Joyo na Kitopeni nilichogundu walimu hawajaamua kuanzisha vituo hivi kwa dhati kwani wengi huishia kukuimbia na hela za wanafunzi Hivyo wazazi kukosa imani,Roho za kwanini sio kivile nahizi zipo kila mahali kaka.
 
Kwa mimi ambaye sijafika lushoto i will pay a visit na nina uhakika fursa zipo.
 
Nakupongeza kiongozi kwa utafiti wako wa kisomi kwani umenifungua sana juu ya wilaya ya lushoto, mimi nimeipenda na MUNGU atusaidie kufanikisha ili suala. lakini pia nawakaribishe ktk wilaya ya Rungwe-Mbeya, ila nipeni muda nifanye utafiti wa kutosha(0769882278)
 
Tuko pamoja Mkuu,Binafsi naisubiri kwa hamu hiyo Post ya Mbeya....Utafiti mwema mkuu
 
Back
Top Bottom