Uwepo wa kina Mdee Bungeni kikwazo cha Rais kuonana na CHADEMA?

Uwepo wa kina Mdee Bungeni kikwazo cha Rais kuonana na CHADEMA?

malang0

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
440
Reaction score
523
Huenda uwepo wa wanachama waliofukuzwa chadema almaarufu covid-19 ni mojawapo wa sababu za Rais Samia Suluhu Hassan, kuchelewa kutimiza ahadi yake ya kukutana na chadema. Kwa utambulisho wa Nusrat Hanje jana jijini Mwanza kama mbunge wa chadema hii inaashiria mama anawatambua hao covid-19 waliofukuzwa uanachama chadema.

Kwa muktadha huo, mkutano wake na chadema huwenda ukawa wenye hoja ngumu kwani chadema wataendeleza hoja zao kwa kiongozi huyo wa nchi kutetea katiba wanaodai inavunjwa na Spika wa Bunge.

Pia uwepo wa tetesi za kiongozi mmoja wa upinzani kupewa ubunge ili aungane na hao covid kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni vinazidi kuchelewesha mkutano huo?
 
Pia uwepo wa tetesi za kiongozi mmoja wa upinzani kupewa ubunge ili aungane na hao covid kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni vinazidi kuchelewesha mkutano huo?
Mwizi mstaarabu huwa anakuibia ila anahakikisha unabakia na nauli ya kukufikisha nyumbani kwako !! sasa hawa wenzetu wamekomba kila kitu baadaye wanaanza kuhangaika kuokoteza okoteza wabunge wa upinzani ili kanuni za kudumu za Bunge ziweze kufikiwa.
 
Back
Top Bottom