Kubbra Hooda
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 208
- 297
Habarini wakuu? Bila kupoteza muda ningependa tujuzane je kuna ukweli wowote juu ya uwepo wa nchi iitwayo giningi, Kwa wale waliobahatika kusoma kitabu kinachoitwa KIVULI KINAISHI cha mwandishi MoHAMED SAID ambacho kinaeleza juu ya uwepo wa nchi hiyo iliyogubikwa na mambo ya GIZA..(japo ameeleza kifashi zaidi) pia nilibahatika kutazama filamu ya kitanzania inayoitwa SIRI YA GININGI iliyochezwa na GABO ambayo imeonyesha uwepo wa eneo hilo lenye mauza uza.
Kuna tetesi eneo hilo linapatikana Zanzibar eneo ambalo kuna limegubikwa na mambo ya GIZA na yakutisha, Je kuna yeyote aliyewahi kufika eneo hilo?au habari hizi ni za kusadikika tu? na kama eneo hilo lipo je habari za kichawi zinazohusishwa na eneo hilo ni za kweli ? Na kama linapatikana Zanzibar ni ktk kisiwa gan je ni UNGUJA AU PEMBA?
Wakuu kuishi ni kujifunza kwa anaejua chochote anaweza kuchangia na kutujuza juu ya uwepo wa eneo hilo.