Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hapo ni mchanganyiko wa sababu nyingi
1. Ukosefu wa vitendea kazi muhimu hasa kwenye upimaji wa magonjwa ( maabara, molecular tests, xray, ultrasound, echocardiogram(TTE or TOE), CT scan, CTPA, CT angio, MRI, MRI angio, Bone scans, white cell scans, PET scan etc list ni ndefu)
2. Ukosefu wa wataalam kwenye vipimo ambavyo vinahitaji technologists na technicians wenye ujuzi mkubwa
3. Uendelezaji wa mfumo wa tiba kwa kizamani - hivi sasa watu wenye akili zao huduma zao za afya wanaziendesha kwa multidisciplinary approach kuna medical team (madaktari), diagnostic teams (maabara, xray, scans) nursing team, phsyiotherapist, dietician, social workers na occupational therapists wakati sisi bado umuhimu uko kwa madaktari peke yao, kila kitu ni daktari daktari daktari!!!.
4. Ukosefu wa miundo mbinu (umeme, maji nk) maana vifaa vingine ni mamashini makubwa yanayohitaji kuwepo kwa maji na umeme wa uhakika pamoja na technicians ambao wanaweza ku vi service. Kuna technilogical gap kati ya vifaa vya kisasa na uwezo wetu kuvitumia
5. Uhafifu wa mfumo mzima wa afya - wagonjwa hawapati huduma za chakula, malazi, dawa zenyewe ni feki, maji ya drip eti ndugu wakajinunulie, hata ambulance sytem hakuna, kila mgonjwa ajisafirishe mwenyewe kwenda na kutoka hospitalini
6. Udhaifu wa elimu wanayopata madaktari kwenye vyuo vyetu ni tatizo kubwa, hata kama wanasomeshwa vizuri ukweli kwamba hospitali hazina vifaa vya uhakika kwa kupimia wagonjwa basi ni dhahiri kuwa daktari wa muhimbili kuna nyanja za udaktari ambazo hataziona hadi anamaliza masomo yake, mimi huwa nawafananisha na wanafunzi wa shule za kata ambao wanasoma sayansi bila kuwepo maabara, madaktari wetu wa muhimbili siyo wakamilifu kwenye masomo yao.
7. Tabia ya kitanzania ya ubinafsi, kila mtu anajali maslahi yake mwenyewe inachangia sana kudumaza maendeleo ya sekta nyingi ikiwemo afya. Hata kama mzungu atatuonea huruma kwa ulofa tulionao na akatamani kusaidia kuweka vifaa na kusomesha madaktari kwa ufanishi wa juu hao wakuu watakokabidhiwa hilo jukumu bado wataangalia kwanza familia zao na za marafiki wao kama hawanufaiki basi mpango utajifia tu.
Hauhitaji Lab technologist wala CT Scan au MRI kudiagnose MALARIA na SINUSITIS. Wala hauhitaji professors kutibu hayo magonjwa mawili. Malaria na Sinusitis zinakuwa diagnosed na kutibiwa Clinical Officers huko kwenye dispensary vijijini huko, don't tell me somebody has to use thousands of our dollars to go to India for that!