SoC04 Uwezo wa teknolojia katika kukuza sekta ya kilimo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 25, 2024
Posts
6
Reaction score
6
Kilimo kimekuwa uti wa mgongo wa taifa la Tanzania kwani kwa asilimia kubwa nchi yetu inategemea kilimo ili kuzalisha malghafi mbalimbali kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa pamoja na kulisha taifa zima. Tangu tupate uhuru kilimo kimekuwa kikichangia katika pato la taifa na ukuaji wa kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 60 kwani ni mazao yanayotokana na kilimo ndiyo yamekuwa yakitumika katika kulisha viwanda ili kuwezesha uzalishaji wa bidhaa nyingine nyingi ambazo zinatumika na kusaidia watanzania katika maisha ya kila siku.

Mazao mengi hupotea wakati wa uvunaji kutokana na aina ya uvunaji wa kizamani ambao hutumika Kwa mfano, mazao ya mikunde (kama vile maharagwe, choroko, na dengu) yanaweza kupotea kwa asilimia 40 kila baada ya kuvunwa, Kwa mazao ya mizizi (kama vile viazi, ndizi, na karoti), hali ya ubichi inaweza kusababisha kuharibika haraka, na matumizi ya mbinu duni wakati wa kuvuna na kuhifadhi husababisha upotevu wa hadi asilimia 452. Vilevile, mazao ya mbegu za mafuta yanaweza kupotea kutokana na matumizi ya maghala duni na kutokutumia viuwadudu wakati wa kuhifadhi.

Zipo baadhi ya teknolojia ambazo endapo kama zitatumika zinaweza kuifanya sekta ya Kilimo ipige hatua kubwa na hata kutupeleka katika Tanzania tuitakayo teknolojia hizo ni kama hizi zifuatazo;

Matumizi ya mashine maalumu za Kilimo.
Mashine hizo ni pamoja na matrekta ya kujiendesha yenyewe ambayo hutumika zaidi kwenye mashamba makubwa. Matrekta hayo hufanya shughuli mbalimbali kama kupanda, kuvuna, kupalilia na kuandaa shamba kwaajili ya kilimo. Mkulima anachotakiwa kufanya ni kutuma maelekezo kielektroniki ya kazi anayohitaji kufanyika na matrekta hayo. kwani mashine yenyewe inafanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi kuliko binadamu na hivyo kurahisisha kazi.

Matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji data.
Teknolojia hii hukusanya data kwa maeneo yenye rutuba na maendeleo ya mazao mashambani huongeza ufaninisi mkubwa katika ufanyaji wa maamuzi kwani mkulima atakuwa na taarifa kamili ya mazao ya aina gani yanastawi sehemu gani na kwa wakati gani kwa mfano mfumo wa habari wa kijiografia (GIS) unatumika kuchanganua taarifa katika aina mbalimbali za ramani.

Kupitia taarifa zinazokusanywa katika mfumo huu mkulima anaweza kutabiri madhara ya hali ya hewa katika shamba lake na kujipanga nayo. Pia kupitia mfumo huu mkulima anaweza kufahamu ni kipindi kipi anaweza kulima au kuvuna shambani kwake.

Matumizi ya ndege isiyo na rubani (drone).
Wakulima wenye mashamba makubwa ni vema kutumia ndege zisizo na rubani kukagua mashamba yao, kupulizia dawa katika mazao pamoja na kumwagilia mazao. Ndege hizi zinaweza kuwa msaada sana kwa wakulima na kusaidia kuongeza ufanisi katika upuliziaji wa dawa kwenye mashamba makubwa na hata kukagua na kutambua ni eneo lenye shida shambani ili mkulima aweze kulishughulikia mapema.

Kufanya sensa za udongo.
Kuna vifaa mbalimbali vya kielektroniki ambavyo mkulima anaweza kutumia kupima hali ya udongo ya shamba lake. Vifaa hivi vya kielektroniki vinavyotumika huwa na sensa ambazo zinaweza kutambua hali ya unyevu iliyopo kwenye udongo, rutuba ya udongo pamoja na joto lililopo kwenye udongo. Kupitia taarifa zitakazo kusanywa na vifaa hivi vya kielektroniki mkulima anaweza kufahamu jinsi ya kuboresha uzalishaji wa mazao katika shamba lake na hata kufanikiwa katika kuongeza.

kufanya programu mbalimbali za kilimo.
Hizi ni programu maalumu kwaajili ya kusimamia shughuli za kilimo. Programu hizi zinaweza kutumika kupitia kompyuta au hata simu janja ambapo zitakuwa na uwezo wa kuwasiliana na sensa ulizoweka kwenye udongo na kukusanya pamoja na kuzihifadhi hizo taarifa pia zinamuwezesha mkulima kupanga ratiba ya shughuli mbalimbali za kufanyika shambani kila siku.

Kuanzisha miradi ya kilimo cha umwagiliaji.
Miradi hii itakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuhakikisha ardhi inakuwa nyevu kwa muda mwingi ili mazao yaweze kustawi vizuri, ambapo visima vitachimbwa katika maeneo ya mashambani ili kurahisisha upatikanaji wa maji karibu na mashamba na hii itawezesha ufanyikaji wa kilimo hata kipindi cha kiangazi ambapo sehemu kubwa ya nchi inakuwa haina mvua. Moja ya mbinu bora ya umwagiliaji ni kutumia njia ya matone ambayo hupunguza kabisa umagaji wa maji mengi.

Teknolojia ina umuhimu mkubwa sana kwenye kilimo kwani inasaidia katika upatikanaji wa masoko kwa haraka.
Teknolojia inaboresha upatikanaji wa masoko kwa wakulima kuuza mazao yao na kwenye masoko ya pembejeo kama mbegu bora na mbolea. Lakini pia kupitia vifaa vya kidijitali kama simu janja mkulima anaweza kupiga picha na kutangaza mazao yake moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii na kupata wateja kwa urahisi badala ya kubeba mazao yake na kwenda nayo tu sokoni pasipo kujua atamuuzia nani kwa na kwa wakati gani.
Teknolojia inasaidia Kuongeza ufanisi na Uzalishaji.

Teknolojia zinasaidia kuongeza ufanisi wa kilimo na kuongeza mavuno ya mazao kwa mfano kupitia hii mkulima anaweza kupata taarifa na kujua jinsi ya kukabiliana na baadhi ya wadudu wanaoshambulia mazao, aina ya mbolea bora pamoja na mbinu nyingine nyingi zinazorahisisha shughuli zake shambani.

Mataifa mengi sana yamenufaika kiuchumi kupitia kilimo kwa mfano taifa la Israel lenye idadi ya watu milioni 9.5 tu ambayo ni mara 7 ya wakazi wa Tanzania ni moja ya mataifa yanayoongoza katika uzalishaji wa matunda na mbogamboga licha ya sehemu kubwa ya taifa hilo kuwa na jangwa huku chanzo kikubwa cha maji wanachokitegemea ikiwa ni mto Jordan.
Licha ya hayo yote taifa la Israel ni moja ya mataifa ambayo teknolojia ina nafasi kubwa katika kilimo kwani katika watu hulima hadi katika kuta za majengo kutokana na uchache maeneo yenye rutuba, wanatumia mbinu mbalimbali za kiteknolojia kama umwagiliaji wa njia ya kawaida na njia ya matone ambao unasaidia kupunguza umwagaji wa maji mengi katika mazao lakini pia wanatumia teknolojia za kisasa ili kuyafanya maeneo kuwa na rutuba.

Hivyo Tanzania inaweza kujifunza na kuiga katika mataifa haya yaliyoendelea katika sekta hii ya kilimo ili kujiendeleza yenyewe na hata ikiwezekana kumfanya mama na bibi kijijini wasahau habari ya kilimo cha jembe na badala yake wakatumia mashine za kilimo kama trekta na mashine za uvunaji pamoja na mbinu bora za kilimo ambazo zitawarahisishia kazi pamoja na kuzalisha mazao mengi zaidi ambayo yataleta faida kubwa kwa taifa.
 
Upvote 9

Kilimo ndiyo kama baba wa sekta nyingne nyingi za kiuchumi maana kupitia kilimo tunapata msosi unaotupa nguvu ya kufanya shughuli nyingne na pia unawezesha upatikanaji wa malghafi za kutengenezea bidhaa kwahiyo kilimo is everything.. big up Mwandishi kwa andiko zuri🔥🔥
 
🙏🙏🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom