Arusha kuna mambo jamaani, hizi bwebwe zote bila shaka anaye ratibu ni huyo mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini Paul Makonda.
Naendelea kunoti kitu huyu Makonda kuna jambo lake zito anazidi kulitengeneza kwenye uongozi soon litakuwa rasmi.
=================
Hamasa ya mapokezi ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan imezidi kushika kasi katika Jiji la Arusha huku Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Wilaya ya Arusha Mjini ukiongoza jitihada za kuwaalika wananchi kushiriki mkutano huo.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 2, 2025, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta.
Katika kuongeza mvuto wa kampeni hizo, baadhi ya wanachama wa UWT wameonekana wakizunguka mitaa mbalimbali ya jiji wakiwa juu ya farasi, hali iliyowavutia wakazi na kuongeza shauku ya wananchi kushiriki tukio hilo.
Akizungumza leo Jumanne, Septemba 30, 2025, kuhusu maandalizi hayo, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Arusha Mjini, Mary Kisaka amesema zaidi ya wanawake 25,000 tayari wamejiandaa kumpokea na kushiriki mkutano wa mgombea huyo wa CCM.