Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) KUMUENZI BI TITI MOHAMED (1926 - 2000)
Leo nimetembelewa na Waandishi Maalum waliokuja nyumbani kwangu tufanye kipindi kuhusu maisha ya Bi. Titi Mohamed ambae taifa limeamua kumuenzi kama tangazo linavyoonyesha hapo chini.
Nimejitahidi kumueleza Bi. Titi kadri nilivyoweza.
Katika moja lililowashangaza wageni wangu ni pale nilipowaambia kuwa Bi. Titi Mohamed alihutubia mikutano ya TANU miwili akihanikisha wananchi wajiunge na TANU kudai uhuru mwaka wa 1955 hata haijui sura ya Julius Kambarage Nyerere inafananaje.
Naamini wengi wetu hatujui kuwa Bi. Titi Mohamed aliingizwa TANU na Schneider Abdillah Plantan, ili aunde Idara ya Wanawake katika chama ushauri aliopewa na John Hatch wa Labour Party ya Uingereza.
Hatch alikuja kumtembelea Tanganyika akiwa mgeni wa TANU.
Naamini wengi wetu hatujui kuwa Bi. Titi Mohamed aliingizwa TANU na Schneider Abdillah Plantan, ili aunde Idara ya Wanawake katika chama.
Bi. Titi alifanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa sana.
Bi. Titi alisimama na Julius Nyerere bega kwa bega ndani ya TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika akihutubia mikutano katika viwanja vikubwa vya mapambano vya Tanganyika kama Mnazi Mmoja na Jangwani Dar es Salaam, Tangamano, Tanga na Uwanja wa Majengo Moshi kwa kuvitaja vichache.
Bi. Titi alivuka bahari na kuingia Zanzibar alikotoa msaada mkubwa kwa Afro Shirazi Party (ASP).
Bi. Titi hakuishia visiwani, aliingia Kenya kuisaidia KANU ili Jomo Kenyatta atolewe kifungoni akihutubia mikutano iliyofurika watu Mombasa na Nairobi.
Si hili peke yake Bi. Titi aliwahamasisha wanawake wa Kenya kutoka jikoni waingie uwanjani katika mapambano ya kuipigania nchi yao.
Wakati huo Bi. Titi akifanya haya yote alikuwa msichana mdogo hajafika miaka 30.
Waandishi hawa maalum katika mazungumzo yetu baada ya kufahamu kuwa nimeandika vitabu kadhaa katika historia ya Tanganyika walitaka kujua kwa nini hadi leo sijaandika maisha ya Bi. Titi.
Jibu langu kwao lilikuwa ninao mswada wa maisha ya Bi. Titi kwa miaka mingi lakini sijathubutu kuuchapa kuwa kitabu.
Sijaweza kuwa na ujasiri huo.
Niliwaeleza kuwa mimi si wa kuandika maisha ya Bi. Titi kwani Bi. Titi ameacha ''mwanae,'' shoga yake na mzungumzaji wake katika waandishi wanawake mahiri Tanzania.
Mwanamama huyu alikuwa karibu na Bi. Titi kwa miaka mingi hadi umauti ulipomfikia.
Huyu kasomeshwa na Bi. Titi alif kwa kijiti historia ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika na askari mwenyewe aliyekuwa mstari wa mbele katika vita vile.
Bi. Titi kamweleza na kamsomesha shogs yake somo la ustahamilivu katika dhahma na fitna za siasa, utumishi wa jamii, kusamehe na kusonga mbele na mwenyewe Bi. Titi Mohamed.
Mwanamama huyu Bi. Titi alimfungulia kitabu cha maisha yake akamsomesha kuanzia ukurasa wa kwanza wa dibaji hadi ukurasa wa mwisho wa kufunga kitabu na kuweka kalamu chini.
Mwanafunzi huyu yeye kwa mapenzi hadi leo anamwita Bi. Titi ''bibi'' na haishi kumrehemu.
Huyu niliwaeleza Waandishi Maalum kapokea mengi katika historia ya maisha ya Bi. Titi kwani katembea na Bi. Titi mwenyewe katika safari yote ya maisha yake toka akiwa msichana mdogo.
Bi. Titi kwa mapenzi makubwa akimfungulia bint huyu masanduku yake ya nguo akimvisha shoga yake huyu kijana wa kileo muhitimu wa fani ya uandishi kutoka Uingereza khanga zake za miaka ya 1950 alizokuwa akivaa wakati wa TANU avae ajipambe achezee ngoma kila taasisi yao ilipokuwa na shughuli.
Huyu bint ndiye aliyemshika mkono bibi yake huyu akamfungulia mlango Bi. Titi atoke nje aliangalie jua upya.
Bi. Titi alitoka na akakubali kuwa Mlezi wa watoto hawa wa kike.
Bi. Titi katika shughuli hizi na vijana hawa kila walipomwalika shughuli yao na akiwa miongoni mwao walikuwa wakimkumbusha safari yake ya maisha na wenzake aliopigania nao uhuru wa Tanganyika wengi wao wakiwa wametangulia mbele ya haki.
Watoto hawa wa kike wasomi walikuwa matunda ya uhuru.
Kila alipowatazama walimkumbusha Bi. Titi, marehemu wanaharakati wenzake - Chiku bint Said Kisusa, Hawa bint Maftah, Tatu bint Mzee, Nyange bint Chande, Halima Selengia, Amina Kinabo, Mwema bint Sultan, Sharifa bint Mzee, Lucy Lameck, Fatma Matola kwa kuwataja wachache.
Nani leo anawakumbuka mashujaa hawa?
Ukurasa mmoja tu niliosoma aloniandikia mwandani huyu wa Bi. Titi umeniliza.
Nimelia kwa kuwa sikuwa nayajua niliyoandikiwa na nina hakika wachache sana wanayajua.
Nimelia kwa kuwa nilikuwa namuomboleza Bi. Titi baada ya kifo chake kupita miaka 21.
Wenzangu walikuwa wamelia na kufuta machozi.
Mwanafunzi huyu wa Bi. Titi ndiye wa kunyanyua kalamu kumwandika Bi. Titi si mimi mchezea pembeni.
Kama maandishi ya khanga yalivyozungumza, ''Tutamuenzi Bi. Titi Daima.''