Pre GE2025 UWT yatoa onyo kwa wana CCM walioanza kufanya kampeni za chini kwa chini kuelekea Uchaguzi Mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu

Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilayani Rufiji Pwani imewaonya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM walioanza kutangaza nia na kufanya kampeni za chini kwa chini kama ishara kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliowakutanisha wajumbe wa jumuiya hiyo Katibu wa UWT wilaya ya Rufiji Mariam Mugasha amesema tabia ya baadhi ya wanachama wasio na nia njema kuanza kufanya kampeni kabla ya muda haikubaliki kwani ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu zilziowekwa na chama.


Your browser is not able to display this video.
 
Hana ubavu wa kuzuia. CCM kuna miamba imekaa kimya na haijulikani lakini siku ikifika watatangaza nia ya urais na huenda kuwa na raisi mwenye sura mpya kabisa mwenye umri usiozidi miaka kati ya 47-55
 
Mkaza mwana WA mama,mnamsifia!
Tulieni ifike 2030 patarudi kama palivyokuwa awali.
Miaka 60 ya uhuru Rufiji mlikuwa hamna maji ya bomba Wala barabara,?
Kulikuwa na Champa Cha upinzani huko miaka yote?
 
ni muhimu sana wale wabunge wanaitwa covi19 ambao wana nia ya kujiunga na CCM kwa wakati muafaka, waache kujipenyeza kwa siri majimboni na kurubuniwa na wajanja ati wanafaa kuanza kampeni za mapema kwa kujitambulisha kwa wananchi,

tafadhali waache vimbelembele, wafuate utaratibu, vinginevyo hawatapokelewa
 
Wabunge wote walishamaliza kampeni za 2025,ila hawakubaliki
 
Asilimia 70% ya wabunge hatarudi bungeni hata kama wakiwatoa kafara ya kuua ndugu, rafiki, wenye nyota njema nk
 
Asilimia 70% ya wabunge hatarudi bungeni hata kama wakiwatoa kafara ya kuua ndugu, rafiki, wenye nyota njema nk
inaweza kua kweli gentleman,

hata hivyo watakua replaced na wabunge wengine kutoka CCM na si vinginevyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…