Uzalendo katika sera za uchumu

Bulesi

Platinum Member
Joined
May 14, 2008
Posts
14,275
Reaction score
13,929
Mheshimiwa Rais Dr. Pombe Magufuli katika salaam zake za mwaka mpya wa 2019 kwa wananchi, amesisitiza sana suala la amani na uzalendo kama nyenzo muhimu zitakazoliletea mafanikio makubwa taifa letu kama zitadumishwa katika mwaka huu tuliouanza. Mimi niavyoelewa ni kwamba wananchi wataonesha na kutekeleza uzalendo kwa nchi yao kwa kupenda na kulinda vile vilivyo mali ya nchi yao na ni jukumu la serikali pia kuonesha uzalendo wake kwa kutunga na kutekeleza sera ambazo wananchi zitawasaidia kulinda na kujivunia vile vilivyokuwa vyao kwa kifupi maendeleo yao!

Huko nyuma mara nyingi serikali ilipojaribu kuwasaidia wananchi wake katika masuala ya kiuchumi hasa ya kilimo kwa kutoa subsidies ,mashika ya kimataifa hususani benki ya Dunia na IMF yalipinga sana hatua hizo jambo ambalo lililazimisha serikali kuacha kutoa misaada hiyo na wananchi kupata taabu sana. Kitendo cha serikali kutowasaidia wananchi pale wanapopata shida za kweli kiuchumi sio kitendo cha kizalendo na ningeisihi serikali ya awamu ya tano isikubali shinikizo za mashirika ya kimataifa ya fedha wanapopinga utekelezaji wa sera za kuwasaidia wazalendo wa nchi yetu.

Mfano mmoja wa sera za kizalendo ambao serikali kwa kupitia benki kuu [BOT} kwa makusudi kabisa inaweza kuitekeleza ni hii ya kuzifainyia ukaguzi wa kina benki zetu zilizoanzishwa na wananchi na kuzijumuisha zipi katika hizo zinaweza kupatiwa mikopo hata ikibidi serikali kununua hisa ili kuongeza mitaji yao [ recapitalization] badala ya kuzifutia leseni zao za kujiendesha !. Uamuzi kama huo utawezesha benki hizo ziendelee kufanya kazi kwa kutoa ajira na pia kuwakopesha wananchi wa kipato cha chini ambao mabenki ya kutoka nje mara nyingi hayawahudumii; na ni wananchi hao hao wa kipato cha chini ambao Magufuli anasema anawatetea! Uamuzi kama huo wa serikali utaonesha kwa vitendo nini maana ya kupenda kilicho chetu yaani uzalendo wa Kweli na sio maneno tu!!
 
Naunga mkono hoja ya serikali kupitia BOT kufikiria jinsi ya kusaidia benki za wananchi kuweza kuongeza mitaji( recapitalize) ili zisiweze kufutiwa leseni zao. Serikali inaweza kuchukua moja ya hatua zifuatazo:- Inaweza baada ya kufanya uchambuzi ukazipa mikopo benki zitakazostahili au serikali inaweza kununua hisa katika hizi benki ambazo wanaweza baadae kuziuza na kurudisha fedha walizowakopesha.

Nchi nyingi zikiwemo za kiafrika ( Ghana ) zimechukua hatua kama hizi na kusaidia uchumi wa nchi zao badala ya kukimbilia kuzifutia benki leseni zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…