Uzalendo kwa Mtanzania ni mtoto wa nje ya ndoa

Uzalendo kwa Mtanzania ni mtoto wa nje ya ndoa

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Nikiwa naendelea subiri mzigo wangu Kariakoo, ngoja niwape nondo moja.

Je, upo tayari kupigania nchi yako kwa jasho na damu endapo kuna adui kaingia?
Je, unahani una sababu yeyote ya kupigania nchi hii?

Kama unasoma nakala hii na kujibu "ndio," naona kabisa akili inasaliti moyo. Moyo unasema hapana, akili hapana, ila mkono ndio. Ukichunguza kwa umakini, unahofia huenda ukisema hapana utafukuzwa kazi na ukoo mzima unakutegemea. Huenda utapoteza marafiki waliokubali kukana mioyo yao.
Lakini jibu halisi ni "hapana."

Kabla ya kuandika uzi huu, nilifanya utafiti. Nilichukua wanafunzi kumi wa darasa la saba na kuwaambia waniandikie wimbo wa taifa. Alipata mmoja tu, na si kuwa alipatia sana.

Tukumbuke darasa la saba ndio darasa la mwisho katika elimu yetu ya msingi.

Ni Watanzania wachache sana wanaojua historia ya nchi yao. Yaani, zaidi ya 95% watakwambia mwasisi wa TANU ni Nyerere.

Waasisi wengi na wapigania uhuru wengi, majina yao yamefichwa kwa makusudi maalum, na sio nyingine ila uchu wa madaraka.

Nisiandike mengi sana ila kiuhalisia ni kwamba hauwezi kuwa mzalendo kwa kitu usichokijua. Pia huwezi jua pasi na kujulishwa.

Ningeshauri wizara iangalie upya historia ya nchi yetu, wakombozi wapewe heshima yao, ijenge hamasa ya mtu kuwa tayari kwa ajili ya nchi yao.

Mfano mzuri, sikiliza wimbo wa taifa la Marekani. Huinua hisia ya kulipambania (hata kama ulizama kiaina).
Tanzania, somo la uraia litenezwe kiasi kwamba mwanafunzi tangu mtoto anajua na kuthamini ardhi yao, rangi yao, mila zao, na kila kitu chao.

Nikiwa nimesimama hapa juani, acha niwaache na hili.

Nikireport kutoka hapa karibu na madereva bodaboda, mimi ni Astrum27 wa JF.
 
Wakati mnapambana watoto wenu wajue waasisi wa Tanu wakiwa Darasa la 7 upande mwengine wa dunia kuna watoto wa kichina wakiwa wanaunda simple machines kwa ajili ya kurahisisha maisha ya kila siku.

Machine hizo zikipelekwa sokoni ni utajiri mtupu kwa familia zao.
 
Tena hapo Kariakoo usipokaa sawa na hiyo simu watachukua.

Ungeweka jina la hao unaoamini wamefichwa majina yao.

Historia huwa ipo mahali inaanzia,

Yule mwendazake alivyo komaa historia iandikwe ni nini kilifanyika, si mliona hajui na hafai.

Historia ina mwanzo,
Even Bible ilipoanzia siyo kwamba nyuma kulikuwa hakuna kitu, ila ilianzia pale.
 
Back
Top Bottom